Ni sababu zipi ziliwafanya hawa washindwe kufufua Viwanda?

Mwijage, Kakunda wakiri kushindwa kufufua viwanda​

WEDNESDAY JUNE 23 2021​


Summary

Mawaziri wa zamani wa viwanda na biashara leo Jumatano Juni 23, 2021 wamekiri bungeni mjini Dodoma kuwa walishindwa kufufua viwanda.
By Habel Chidawali
More by this Author

Dodoma. Mawaziri wa zamani wa viwanda na biashara leo Jumatano Juni 23, 2021 wamekiri bungeni mjini Dodoma kuwa walishindwa kufufua viwanda.

Charles Mwijage ambaye ni mbunge wa Muleba Kaskazini na Joseph Kakunda (Sikonge) kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.

Mwijage akichangia hotuba ya muswada wa fedha ameitaka Serikali kuachana na mpango wa kufufua viwanda kwani yeye alivishindwa.

"Mpango wa kufufua viwanda achaneni nao fikirieni vitu vipya, mimi nilijaribu katika wakati wangu lakini nilishindwa kwa hiyo msipoteze muda kufikiria ufufuaji wa viwanda," amesema Mwijage.

Wakati Mwijage akiendelea kuchangia, alisimama Kakunda kwa ajili ya kumpa taarifa ambapo mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimpa nafasi ya kuzungumza.

" Mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji (Mwijage) kuwa hata mimi nilijaribu kufufua kiwanda kule Lindi lakini nilishindwa, kwa hiyo mchango wake ni sahihi kabisa," amesema Kakunda.
Mwijage alikuwa na viwanda 300 kumbe vilikuwa vya mdomoni?
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
jingalao njoo uone ule upuuzi ulikuwa unalishwa na dhalimu uone waliokuwa mawaziri wanasema ulikuwa usanii. Hapa ndio utajua dhalimu alifanikiwa kuwabrainwash wajinga wa aina yako.
 
Back
Top Bottom