Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana jamvi nimewasalimu. Leo naja na nyuzi ya kiitikadi kidogo tuweze kupeana ufafanuzi.
HAYATI MORINGE SOKOINEKibongo bongo Hayati ni Mwalimu JK. Sijawahi sikia mwingine
Hayati Abeid Aman Karume... Naona ni wanasiasa tu ndo wanaitwa hayati, kama ingekuwa ni umaarufu hata akina marehemu Kanumba wangeitwa hayati.
Hayati Abeid Aman Karume... Naona ni wanasiasa tu ndo wanaitwa hayati, kama ingekuwa ni umaarufu hata akina marehemu Kanumba wangeitwa hayati.
Wana jamvi nimewasalimu. Leo naja na nyuzi ya kiitikadi kidogo tuweze kupeana ufafanuzi.
Nashukuru kwa shule maana hizi za kuiga tunaiga hata tusilolijua. Kwahiyo naweza kumwita mme wangu badala ya honey nikasema Yaa hayati wangu? Si ataniporomoshea matusi kumwita mfu?Yote haya maneno mawili asili yake ni kiarabu
Marhoom (marehemu) aliekufa, mfu
Hayati :- my life au uhai wangu
Unaweza kumsifia umpendae na kusema Yaa hayati au Umri
Sasa kwa kiswahili hayati halina uhusiano na kifo na sijui liliingiaje
Sent from my SM using Tapatalk
Hahahaha Walahi nimecheka sanaNashukuru kwa shule maana hizi za kuiga tunaiga hata tusilolijua. Kwahiyo naweza kumwita mme wangu badala ya honey nikasema Yaa hayati wangu? Si ataniporomoshea matusi kumwita mfu?
Sawa kabisaHayati ni maalum kwa viongozi au watu ambao wameacha atahri chanya kwenye Jamii zao. Mfano Hayati Nyerere, Sokoine, Karume na wengine ambao wamepewa heshima hiyo na taifa. Hayati linatokana na neno hay... kwa maana chenye uhai. hivyo hao wanaopewa jina hilo wanaonekana kwa matendo yao bado wanaishi/ yanaishi
Marehemu ni mtu yeyote aliyekufa. japo asili ya neno hili si lazima litumike kwa marehemu tu. hii ni kwa sababu neno marehemu linatoka katika jina Rehema na kila mja anahitaji na ategemea rehema za Mungu Mwenyezi (kwa waaminiao). ila kwa mazowea ni kuwa marehemu ni aliyekufa tu.
Desease? Au decease person?!
Moja ina s nyingine c
Na hiyo yenye c lazima iwe na d mwisho, past tense....aliekwisha kufa.
Sent using Jamii Forums mobile app