Ni sababu ipi mtu huitwa marehemu na mwingine kuitwa hayati?

Ngwango

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
356
272
Wana jamvi nimewasalimu. Leo naja na nyuzi ya kiitikadi kidogo tuweze kupeana ufafanuzi.
 
Yote haya maneno mawili asili yake ni kiarabu
Marhoom (marehemu) aliekufa, mfu
Hayati :- my life au uhai wangu
Unaweza kumsifia umpendae na kusema Yaa hayati au Umri
Sasa kwa kiswahili hayati halina uhusiano na kifo na sijui liliingiaje

Sent from my SM using Tapatalk
 
Wana jamvi nimewasalimu. Leo naja na nyuzi ya kiitikadi kidogo tuweze kupeana ufafanuzi.

1 - Alie fia ktk imani ya kishirikina imani ya kuamini Mungu zaidi ya mmoja, ( miungu) au huyo mmoja hakamiliki kwa umoja wake lazima awe na matawi kama mtoto baba sijui mjukuu, huyo akifa huitwa Hayati. kwa tafsiri ya Maiti

2 - Alie kufa akiamini ktk imani ya Mungu mmoja hakuzaa wala kuzaliwa hana mtoto na hafanani na chochote huyo akifa huitwa Marehemu. Kwamaana ya kumuombea duwa ya kurehemewa na huyo Mungu mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayati anaitwa mtu baada ya kuzikwa na Mara nyingi kama ameacha kitu chochote ambacho jamii iliyobaki inanufaika nacho.

Marehemu ni kabla hajazikwa. Ila sasa hawa wanaoitwa marehemu hata baada ya kuzikwa ni kama hawajaacha chochote katika jamii.

Note: hii ni kutokana na uelewa wangu hivyo si lazima iwe kweli.

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
 
Hayati ni yule mtu maarufu kisiasa hasa ngazi za urais na uwaziri mkuu au katika kanisa Papa na kardinali marehemu ndio akina sie
 
Hayati Abeid Aman Karume... Naona ni wanasiasa tu ndo wanaitwa hayati, kama ingekuwa ni umaarufu hata akina marehemu Kanumba wangeitwa hayati.
Wana jamvi nimewasalimu. Leo naja na nyuzi ya kiitikadi kidogo tuweze kupeana ufafanuzi.

Hayati:- Mtu maarufu, mwenye hadhi katika jamii ambae kafariki
Marehemu:- Mtu yeyote ambae kafariki

Ki msingi kwa mantiki hakuna utofauti wa kimaana wote ki ujumla wameaga dunia isipokuwa tu labda kabla huyo mtu hajafariki alikuwa na hadhi gani katika jamii.
 
Yote haya maneno mawili asili yake ni kiarabu
Marhoom (marehemu) aliekufa, mfu
Hayati :- my life au uhai wangu
Unaweza kumsifia umpendae na kusema Yaa hayati au Umri
Sasa kwa kiswahili hayati halina uhusiano na kifo na sijui liliingiaje

Sent from my SM using Tapatalk
Nashukuru kwa shule maana hizi za kuiga tunaiga hata tusilolijua. Kwahiyo naweza kumwita mme wangu badala ya honey nikasema Yaa hayati wangu? Si ataniporomoshea matusi kumwita mfu?
 
Kwa sababu majibu yameshatolewa ngoja niongezee.

1) KILA HAYATI NI MAREHEMU.

SIO KILA MAREHEMU NI HAYATI.
 
Nashukuru kwa shule maana hizi za kuiga tunaiga hata tusilolijua. Kwahiyo naweza kumwita mme wangu badala ya honey nikasema Yaa hayati wangu? Si ataniporomoshea matusi kumwita mfu?
Hahahaha Walahi nimecheka sana
Ukilitamka kiswahili hapo utaharibu kila kitu

Sent from my SM using Tapatalk
 
Hayati ni maalum kwa viongozi au watu ambao wameacha atahri chanya kwenye Jamii zao. Mfano Hayati Nyerere, Sokoine, Karume na wengine ambao wamepewa heshima hiyo na taifa. Hayati linatokana na neno hay... kwa maana chenye uhai. hivyo hao wanaopewa jina hilo wanaonekana kwa matendo yao bado wanaishi/ yanaishi
Marehemu ni mtu yeyote aliyekufa. japo asili ya neno hili si lazima litumike kwa marehemu tu. hii ni kwa sababu neno marehemu linatoka katika jina Rehema na kila mja anahitaji na ategemea rehema za Mungu Mwenyezi (kwa waaminiao). ila kwa mazowea ni kuwa marehemu ni aliyekufa tu.
 
Sawa kabisa
Ndio maana unaweza kumwambia alie hai "Mungu akurehemu"

Sent from my SM using Tapatalk
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom