Ni rumors/tetesi gani ulishawaisikia kuhusu wewe hadi zikakuacha umepigwa na butwaa?

stritglow

JF-Expert Member
Apr 7, 2018
622
1,750
Katika maisha tunakutana na watu wengi, na katika kujumuika huko na watu, either ni mashuleni, nyumbani, majirani, kwa ndugu, kazini, mtaani n.k, rumors/tetesi mbalimbali zinajengeka kuhusu wewe.

Mfano siku ya kwanza umejiunga na shule mpya, kulingana na jinsi unavoonekana, rumors zinasambaa shule nzima kwamba kwa jinsi ulivo unaonekana kipanga sana... Au umeanza kazi, kutokana na ukaribu wako na bosi, tetesi zinasambaa kwamba nyie wawili mnamahusiano...

As you can see most of these rumors are harmless na nyingi zinakuwa ni za uongo.

Lakini sometimes unasikia rumors kuhusu wewe, hadi unapata mshtuko kuwa ni wewe huyu huyu wanaemaanisha au kuna mtu mwingine.

Mfano.
Kipindi nilipokuwa mdogo, wazazi walikuwa wanahama sana kikazi, na walikuwa hawapendi notion ya kumpeleka mtoto boarding so tulikuwa tunahama nao most of the time.

Sasa siku mama alihamia dodoma kikazi, enzi hizo its just a small desert town. Hamna cha udom au mazagazaga mengine ambayo kidogo imefanya dodoma angalau ionekane inawatu sikuhizi.

Sasa mama akatafuta sehemu ya kufikia for the time being kabla hatujamove to a more permanent/better place. Hiyo sehemu ilikuwa nyumba kubwa tu, ambayo kila chumba mwenye nyumba amerent out kasoro sehemu ya jiko tu. Tulikuwa kama familia tatu kwenye hiyo nyumba.. Mtu na mke wake wali-occupy dinning na chumba kimoja cha kulala, mwngine alikuwa ame-occupy vyumba viwili vya kulala na sebule.. Na sisi tukawa tume-occupy chumba kingine cha kulala ambacho kilikuwa ni masterbedroom.

Humo tulikuwa mimi, wadogo zangu wawili na mdada wa kazi.

Tulikaa hapo for like a month or two then tukamove out to our own place.

Sasa a few years later wakati napiga story na mama ndo akakumbuka na kuniambia kuwa moja ya ile familia, yaani yule mke na mume, tuliokuwa tunaishi nao... Kutokana na jinsi walivyomwona mama, yaani mstaarabu, halafu tunaonekana mambo safi, lakini wote tunaishi kwenye kichumba kimoja and all that... Wakahisi pengine my mum was on the run from the authorities kutokana na biashara ya madawa ya kulevya soo akaamua aje ajifiche huko dodoma kwenye hicho kinyumba. Nilishangaa kwakweli, ila nikaishia kucheka tuu...

Anyways so kama heading inavosema ni tetesi gani ulishawaisikia kuhusu wewe hadi zikakushangaza...
 
Siku nilipohama shule, hii nilotoka tulikua girls kivyao na boys kivyao, huko nilikokwenda tumechanganywa darasani, sikua nasimama kujibu swali, najibu nikiwa nimekaa hata nyuma siangalii naogopa sjazoea mchanganyiko, kumbe nilikua naambiwa najisikia nakujiona,
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom