Ni ruhusa kwa Madaktari zaidi ya mmoja kumsikiliza/kumhudumia mgonjwa..????

JimCarrey

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
214
124
Nina rafiki angu wakike ameenda hospitali leo akiwa anasumbuliwa na maumivu wakati wa haja Kubwa. Alipoingia chumba Cha daktari akawakuta madaktari wa5 Kati Yao wa3 ni wakiume na wa2 ni wakike wote wakiwa chumba kimoja.....!!!!!! Aligoma kuwaeleza wakambembeleza basi akawaelezea.... Waka mwambia alale kitandani na avue nguo zake za ndani wamchunguze..... Aliogopa ila hakua na jinsi ilimbidi alale na dokta mmoja akamchunguza kwenye njia yake ya haja Kubwa na akabaini kua anauvimbe kwa ndani na kumwambia aende j5 kwa upasuaji....!!!! Alivonieleza nilisikitika sana, nafikiri haikua haki.... Angeweza kugoma na kuwaomba wapungue sababu yeye mwenyew alitamani kufanya hivyo ila alikosa maamuzi
 
wale ni madaktari!sasa haki mpaka ya kukataa ktibiwa kisa wako wengi mmh!tena wajinsia tofauti,kwann acngewaza kwamba wakiwa weng kwenye uchunguz ndyo itakuwa vema!?(madaktari wako mazoezini ila wanakuwa na mkuu akiwaelekeza'internshp')j5akienda asiogope mkuu!atatibiwa na wala co kudharirishwa,daktari kazin hawazi unachowazia ww,anaishika 'o' yako akili ikiwa kimatibabu wala co vingne
 
Daktari haogopwi, hata wangekua kumi eleza tatizo lako, wameapa kutunza siri za wagonjwa, na hata hao wanawake, hakuna kipwa kusikia wala kuona wanaona sana hao. Hakuna tusi mbele ya Daktari wewe taja wazi wazi tu, wala huna haja mavi kuita choo, utakua unajizingusha tu. Yote kwa yote hakuna kosa hapo, sasa siku ya operation wanaweza ongezeka wakafikia mpaka 15 wakiwa na wanafunzi wao, sembuse hao wazoefu wa kusikia na kuona magonjwa ya watu.
 
Sijaona tatizo....
Ingawa ingekuwa vyema kistaarabu wengine wangesepa.... hata mgonjwa anahitaji kuwa comfortable
 
Nina rafiki angu wakike ameenda hospitali leo akiwa anasumbuliwa na maumivu wakati wa haja Kubwa. Alipoingia chumba Cha daktari akawakuta madaktari wa5 Kati Yao wa3 ni wakiume na wa2 ni wakike wote wakiwa chumba kimoja.....!!!!!! Aligoma kuwaeleza wakambembeleza basi akawaelezea.... Waka mwambia alale kitandani na avue nguo zake za ndani wamchunguze..... Aliogopa ila hakua na jinsi ilimbidi alale na dokta mmoja akamchunguza kwenye njia yake ya haja Kubwa na akabaini kua anauvimbe kwa ndani na kumwambia aende j5 kwa upasuaji....!!!! Alivonieleza nilisikitika sana, nafikiri haikua haki.... Angeweza kugoma na kuwaomba wapungue sababu yeye mwenyew alitamani kufanya hivyo ila alikosa maamuzi
Kwani inatakiwa utibiwe na madaktari wangapi? Mbona kwenye operation wanakuwa zaidi ya mmoja? Au nayo siyo tiba?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom