Ni Roho mbaya Kumchukia Ex - Wako Eti Kwakuwa Kapata Mpenzi Tajiri Kuliko Wewe !

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,172
Habari Wadau Wa MMU !

Leo Binafsi Nimeona Niongelee Suala Hili Maana Limekuwa Kilio - Lawama Na Kuombeana Mabaya Bila Hata Sababu Za Msingi.

- Kwanini Mtu Unamchukia Mdada Wa Watu Eti Kwasababu Kapata Jamaa Ambaye Angalau Kiuchumi Yuko Vizuri Kuliko Wewe ?! Unaita Eti Ni Msaliti,
Hivi Kwanini Watu Hampendi Mafanikio Ya Watu Wengine ?

- Hivi Assume Angekuwa Ndugu Au Dadako ,ungekuwa Tayari Kumwona Anaolewa Na Kapuku Tena Asiye Na Future Yeyote Kwasababu Wanapendana

- Mfano Wewe Uko Tayari Kumwona Dadako Anaingia Kwenye Mahusiano Na Teja Kwa Kuwa Eti Wanapendana?

- Hebu Jamani Tujaribu Kuwatakia Mema Dada Zetu - Kama Mdada Kapata Mtu Anayejiweza Na Kuokoka Kwenye Ugumu Au Msoto Wa Maisha Uliokuwa Unampa , Mtakie Mema Na Mwombee Chuki Kalii Hazisaidii

- Anyway Wanaume Tutafute Mtonyo Vinginevyo Kina Mengi Wataendelea Kutunyang'anya Watoto Wakali

- Hakuna Anaependa Maisha Magumu, Na Ninyi Kina Dada Nawasihi Mjitambue Mapema - Sio Kusubiri Mpaka Mzae Ndo Akili Ziwarudie

Happy New Year 2017
Ahsanteni
 
itakuwa kuna vitu unavikosa kwa huyo tajiri,sasa unalazimisha uwe nae tajiri mchache akukidhie....!!.hata mimi nakuchukia.....
 
itakuwa kuna vitu unavikosa kwa huyo tajiri,sasa unalazimisha uwe nae tajiri mchache akukidhie....!!.hata mimi nakuchukia.....
Tuwatakie Mema Waliokuwa Wapenzi Wetu Pale Wanapotoka Kwenye Msoto Mkuu Kiroho Safi Tu
 
Maisha yenyewe mafupi haya, huo muda wa kukaa namchukia mtu nautoa wapi. Once we are done then we are done for good, i wish you luck then we go separate ways.
 
Sasa ulipomtaja Mengi ndo umeanza kuharibu maana na yeye naskia amenyang'anya demu wa mtu!!!
 
Maisha yenyewe mafupi haya, huo muda wa kukaa namchukia mtu nautoa wapi. Once we are done then we are done for good, i wish you luck then we go separate ways.
Mmh Leo Kila Mtu Atakataa - Kuwa Akiachwa Analialia
 
Maisha yenyewe mafupi haya, huo muda wa kukaa namchukia mtu nautoa wapi. Once we are done then we are done for good, i wish you luck then we go separate ways.
Badala ya kuwaza kupata chumba chenye hewa na kitanda chenye raha angalau uongeze siku za kuishi.
 
Ndio hapo chacha!!!
Kama ukiendelea kunichukia na kuniombea mabaya ni juu yako, mie walaaaa. Maisha yanasonga.
Somo la maisha ni simple sana, tunafeli kwa kukopiana notes wakati assignments zetu ni tofauti.
 
Jinsi watu wanavyo exi shana ndo penye tatizo la yote haya.

Imagine demu anayemwacha mshkaj kwa nyodo kibao, matusi na dharau kisa bwana mpya, its obvious nafsi ya mwenzake itasononeka na ndo mwanzo wa kuombeana mabaya.

Wengine unaona kabisaa penzi linafika mwisho na kila mmoja wenu anakubali kwamba hapa sasa basi. Kiroho safi yaani.

Mi niliachana na demu wangu flani wa utotoni, hata leo ukiniuliza sijui sababu hasa ilikuwa ni nn, ila baadaye nilitoa mchango wa harusi bila shida, na nafsi yangu iko saafi na namwombea mazuri alipo ana atakapokuwa.

Cha kusisitiza hapa ni Kuheshimiana, unapompata mpenzi mpya fanya juu chini uachane na uliyenaye kabla hujaingiza watu kwenye ushindani usomaana na nyongo zisizoisha.

.....
 
Back
Top Bottom