Ni rasmi sasa VODA inafukuza wateja

Angalau kifurushi cha 7,000/= kwa wiki kina afadhali kidogo.

Ila kifurushi hiki nilichojiunga kikiisha naachana nao.
 
dah nikajua labda kwangu ndo kuna shida...ni siku ya 3 sasa modem ya voda GSM sijui nini icho?yani wamepolomoka vibaya sana na wanaboa kishenzi,internet yao imekua mbovu balaa
kesho mapema nahamia airtel sijui vifurushi vyao vikoje?interent je?

nchi za wenzetu afrika tu wameweka miundombinu dhabiti ya net hakuna mafua haya,afu serikali hii ya bongo ndo inazidi kurudi nyuma ktk sekta nyeti ya mawasiliano WHY?

mamlaka butu ya mawasiliano, wizara feki na serikali hoi
 
Mkuu na mimi nimeisoma leo nafikiri hizi fedha nilizoweka ndo za mwisho. Naamia Airtel jumla.

Airtel nao majanga tu,

Hapo kabla ilikua ukilipa 999/- unapata
dakika 61,
SMS 5,000 na
GB 1.

But now unapata dakika 40
SMS _ _ _
300 MB
 
ni kweli..
voda hakufai tangia tar 14 dec...kama darfur vile..
nimejiunga na kifurushi cha buku nikapewa masekunde meeengi voda to voda na sekunde sitini kwenda mitandao mingine..huu ni utani hakika..
dawa yao ni kuwakimbia tu..mwisho watashika adabu..
 
Kuanzia jana sina hamu tena na Vodacom nipo kivulini na kilaini changu changu cha tigo nasongesha maisha.
 
Kazi ni kwako kuhama au kuendelea kunyonywa.

Kazi ni kwako kuhama au kugomea kabisa simu (tiGo, Voda n Airtel).


Na msisahau kuwa na umeme nao ndio hivyo hivyo. Nadhani 2015 imekaribia.
 
Mimi hii simu iliyobeba Voda ikifa basi. Kwanza huwa naiacha nyumbani kama Landline.
 
wamebadili vifurushi ambavyo ulikuwa ukijiunga unapiga mitandao yote, lakini sasa ukinunua vifurushi hivyo unapiga voda-voda tu, huku kwenda mtandao mwingine unakatwa hela nyingi kama zamani zile! Hii ni msiba kwetu sisi walala hoi. Na kwakweli sasa inanilazimu kuuhama huu mtandao!

mkuu pengine umeshindwa kuvielewa hivyo vifurushi na umejikuta una potosha alaf tusi sahau hii ni biashara.

Walicho fanya voda ni kufanya mabadiliko kidogo kwenye muda wa kupiga mitandao mingine ukilinganisha na voda -voda.

Mfano vifurushi vya masaa24

tsh400=900sec(voda-voda)+45sec(mitandao mingine)+100sms+50mb.

Tsh500=1200sec(voda-voda)+50sec(mitandao yote)+250+100mb

tsh1000=3000sec(voda-voda)+60sec(mitandao mingine)+300+100mb

ukijaribu kuangalia vifurishi hivi utagundua kuwa sec zilizokuwa zina tumika mitandao yote kwa sasa zina tumika voda-voda na bado wametoa sekunde kwa mitandao mingine.

Si kweli kuwa hupigi mitandao mingine bali muda wa kupiga umepunguzwa, na hii ni biashara.
 
Wamebadili vifurushi ambavyo ulikuwa ukijiunga unapiga mitandao yote, lakini sasa ukinunua vifurushi hivyo unapiga voda-voda tu, huku kwenda mtandao mwingine unakatwa hela nyingi kama zamani zile! Hii ni msiba kwetu sisi walala hoi. Na kwakweli sasa inanilazimu kuuhama huu mtandao!

Mwenyewe nimebaki na mshangao.

Hii ndio Kaburu Matata Iya...
 
Rostam Aziz yuko mbioni kuihama nchi na hivyo anafanya vituko vya mwisho kabla ya kufunga kampuni ya Voda mazima. Si mmesikia pia yuko kwenye harakati za kuuza Habari Corporation kwa wakenya?
 
walianza kupandisha bei mfano kile kifurushi cha 3500 kikawa 4200, mara dakika wakapunguza toka 140 mpaka 100.
sasa naona imewatokea puani na tutawahama wengi tu.
 
line ya voda ni ya kupokelea simu tuu. usithubutu kuweka pesa ni sawa na kuitupa baharini
air-tel wako vizuri. hata air tel money wako vizuri
 
Airtel ni nomaaa,hawana wizi huo,hawa voda kwenye net wanajitahidi sana,wakizingua kwenye vifurushi vya net nawahama mazima narudu nyumbani mazima airtel dingi lao
 
Back
Top Bottom