Nimeangalia picha ya watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa Jk kama Rais wa Tanzania. Picha hizo zilinishtua pale nilipoona watu wamevaa mavazi ya CCM na kubeba bendera za CCM. Nikajiuliza, hivi watu wanaelewa kwamba wako wapi na wanafanya nini? Viongozi kutoka nchi zingine wanatutambua kama Watanzania na wamealikwa kuja kushiriki sherehe za kuapishwa rais wa Tanzania (hata kama anatokana na CCM), bendera ya CCM inatambulisha nini? Mbona Jk hakuwa amevaa nguo za CCM? Au watu wameishiwa na nguo hivyo wanavaa hizo za mgao wa CCM? Au ndo yale matatizo ya kusombwa na malori kwenda kwenye kampeni za CCM bila kufikiri kampeni zimeshaisha.
Hayo ni matatizo makubwa ambayo yanapaswa kurekebishwa katika vichwa vya watu hasa kwamba tuone utaifa wetu unazidi Vyama vyetu. Tukiweza kufika mbali kidogo tunaweza kutambua kuwa maslahi ya taifa ni makubwa kuliko ya Chama.