Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kama kichwa changu cha habari kinavyosema ni Rais Magufuli peke yake anayeweza kuwahakikishia na kuwarudishia imani watanzania ili waende kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura wa serikali za mitaa
Unaweza kujiuliza je atawahakikishaje watanzania?
Swali hili jibu lake ni hili, ni Rais Magufuli ndiye aliyewavunja moyo wapiga kura wa nchi hii hadi wamekata tamaa ya kuona zoezi zima la kupiga kura kama kichekesho, kwa kuona hata kama utapiga kura, lakini matokeo yake yanajulikana, ni "lazima" atangazwe mwanaCCM kuwa ameshinda uchaguzi huo.
Kauli na mienendo ya Rais Magufuli ndiyo ambayo imewafanya watanzania wakate tamaa kabisa na zoezi la kupiga kura nchini Tanzania
Tujiulize nchi ambayo imekuwa ikipiga hatua kidemokrasia hadi mwaka 2015 wakati anaingia madarakani Rais huyu ambaye kwa kauli zake na vitendo vyake vinaonyesha dhahiri kuwa ana nia ya kuua upinzani nchini na nchi irejee kwenye mfumo wa chama kimoja
Tunajionea namna mtawala huyu anavyojitahidi kuwajaza makada kindakindaki wa CCM kwenye Tume ya uchaguzi ya Taifa, akiwemo Mkurugenzi wake Dkt Wilson Mahera, licha ya mhimili wa mahakama kuwapiga marufuku wanachama waandamizi wa vyama vya siasa kutoteuliwa kwenye chombo hiko kinachosimamia uchaguzi.
Ni yeye Rais ambaye akinukuliwa huko siku za nyuma akiwaambia wateule wake kuwa nimekuteua na kukupa gari ya kifahari ya kutembelea, nyumba nzuri ya kuishi na mshahara mnono, halafu nisikie unamtangaza mpinzani kashinda katika eneo lako! Utakuwa umejifukuzisha kazi!
Kwa hiyo anatakiwa Rais Magufuli alihutubie Taifa na kuwahakikishia watanzania kuwa uchaguzi ujao wa serikali za mitaa utakuwa huru na haki na atubu kwa watanzania kuwa yale maneno na matendo yake aliyokuwa anayatoa alikuwa amekosea na ni uvunjifu wa Katiba wa waziwazi kabisa
Kwa kuyasema hayo na awasihi watanzania wamiminike kwa wingi kwenye vituo vya kujiandikisha, nina hakika baada ya tamko hilo watanzania watafurika kwenye vituo vya kupigia kura.
Lakini kinyume cha hapo, ikiwa Rais hatapenda kujishusha na kujisahihisha na kuona kuwa maneno yake na vitendo vyake ndivyo vilivyosababisha watanzania wavunjike sana moyo wa kujiandikisha basi itakuwa sawasawa na kutwanga kwenye kinu kilichojaa maji!