Ni rais jimmy carter tu

Oikos

Senior Member
May 5, 2011
198
111
Katika marais wote waliotangulia katika taifa la Marekani, ni rais Jimmy Carter tu ndiye aliyekuwa anamkakati wa kuona ukabulu unakoma Afrika ya Kusini na usawa unashamiri duniani.

Hakuna viongozi wengine wowote waliofuata ambao walikuwa na nia hiyo. Rais Jimmy Carter akihojiwa na Aljazeera masaa machache yaliyopita alisema kuwa yeye alilelewa na house girl mwafrika wakati alipokuwa mdogo huko Atlanta, Georgia.

Na hivyo aliwapenda Waafrika tokea zamani na alipokuwa Gavana wa Georgia alitangaza hadharani kuwa unyanyasaji wa Waafrika hauna nafasi katika jimbo lake.

Ndio maana alipochukua utawala, rais wa kwanza mwafrika kualikwa katika ikulu ya Marekani alikuwa Julius Nyerere! Alifanya hivyo kutambua mchango mkubwa wa rais wetu wa kwanza katika ukombozi wa Afrika.

Sera za Marekani kabla ya rais Jimmy na hata baada yake zilikuwa kwamba kila nchi yenye mahusiano na nchi za kikomunisti ni adui wa taifa hilo.

Kazi aliyofanya rais Kambarage ya ukombozi wa Afrika, ilistahili pongezi kubwa mno toka kwenye jamii ya kimataifa ila kuegemea kwa "ho nhi nhu" kulituponza!!!

Nawasilisha
 
Uongo, si Nyerere. Rais wa kutoka Africa wa kwanza kualikwa na Jimmy Carter alikuwa ni Anwar Sadat wa Egypt.

Rais wa kwanza wa kutoka Afrika kualikwa na Rais wa USA aliposhika madaraka ni Kikwete alipoalikwa na Obama.
 
kwa mbalii,kuna elementi ya ubaguzi hapo! Hivi egypt iko afrika ama uarabuni? Je inashiriki kwenye jumuiya za afrika?
 
wewe ni shehe ubwabwa.
 
Uongo, si Nyerere. Rais wa kutoka Africa wa kwanza kualikwa na Jimmy Carter alikuwa ni Anwar Sadat wa Egypt.

Rais wa kwanza wa kutoka Afrika kualikwa na Rais wa USA aliposhika madaraka ni Kikwete alipoalikwa na Obama.

Sadat ni mwarabu siyo mwafrika kama alivyotanabaisha mwanzisha mada..
 
kwa mbalii,kuna elementi ya ubaguzi hapo! Hivi egypt iko afrika ama uarabuni? Je inashiriki kwenye jumuiya za afrika?

Pole sana. Inaonesha huijui hata Africa ni nini na Uarabuni ni nini. Hata Bujumbura kuna Uarabuni.
 
Uongo, si Nyerere. Rais wa kutoka Africa wa kwanza kualikwa na Jimmy Carter alikuwa ni Anwar Sadat wa Egypt.

Rais wa kwanza wa kutoka Afrika kualikwa na Rais wa USA aliposhika madaraka ni Kikwete alipoalikwa na Obama.

wewe ni udini tuuuu.
 
Back
Top Bottom