Ni Rais gani mwingine aliyekuwa kwenye hotuba zake anawaambia wahutubiwa watamkumbuka?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Hotuba nyingi za JPM alikuwa anapenda sana kutuambia sisi wanyonge kuwa tutamkumbuka! Hakuwa akisema tutakumbuka aliyofanya yeye mazuri.

Ni sawa na kawaida kwa mfano Mwl anapowafundisha wanafunzi kusema mtakumbuka niliyowafundisha lakini hasemi kuwa mtamkumbuka yeye kama yeye.

Nimefuatilia hotuba za watangulizi wa JPM hata huwezi kukuta neno wamejisema wao kama wao kuwa "TUTAWAKUMBUKA". Je Mama yetu Samia Suluhu naye atakuwa anatukumbusha kwa kutuambia kwa maneno yake kuja kumkumbuka huko mbeleni?

Na je hatuwakumbuki watangulizi wa JPM pamoja na kutosema kwao kuwa tutawakumbuka wao kama wao? Just observation!
 
Alifanya yote kwa kujitoaa.

Maneno ya wanasiasa wenzake wa upinzani yalikuwa yanawapotosha wananchi kuwa yeye ni mbaya.

Ndio Maana alitaka watu wasimpuuze ili baadae wasije jutia kwa yeye kutokuwepo...!

"Nimesacrife maisha yangu kwa ajili yenu"

Alijua yeye ni mgonjwa ndioa maana alijitoa sana. Ila wabaya hawana jema.

Angeamua tu kigaia mali ndugu zake. Na kujineemesha maana hana muda. Alikataa hata kuongezewa muda.
Bahati watu walimuona muigizaji.
 
Trump aliisaidia nchi yake kwa kutochukua mshahara,Yeye Meko alitumia nini cha kwake?

Miradi ni kodi zetu na mikopo toka ndani na nje.Kipindi chake kiasi cha deni kimepanda maradufu,watumishi ndio hivyo tena miaka 6 hajawaongezewa mshahara.

Nisaidie zuri moja la kumkumbuka
 
Kama ambavyo niliambiwa kuwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tokea mwaka 1993 alishaambiwa na Madaktari wake huko Ulaya kuwa angeishi tu ndani ya miaka Mitano kutokana na Saratani yake ya Damu ( Leukemia ) kufikia hatua mbaya.

Hivyo basi naanza Kushawishiana kuwa huenda hata Hayati Rais Dkt. Magufuli nae kutokana na tatizo lake la muda mrefu la Moyo alishaambiwa miaka Kumi iliyopita kuwa asingeishi miaka mingi na ndiyo maana mara nyingi alikuwa akisema Akifa Watanzania tutamkumbuka sana na tumeshaanza Kumkumbuka hata kabla hajaanza Maisha yake Kaburini Kesho tarehe 26 March, 2021.
 
Inawezekana kweli?
Yeye alijua kafanya makubwa na lazima mumkumbuke kwa sabb hakuna atakaejitoa kama yeye.. Kusisitiza hivi alijua anastahili kuwa mfano mzuri kwa wajao sasa sijui kama wanaomlaumu kaum y wengi au vp
 
Hotuba nyingi za JPM alikuwa anapenda sana kutuambia sisi wanyonge kuwa tutamkumbuka! Hakuwa akisema tutakumbuka aliyofanya yeye mazuri.

Ni sawa na kawaida kwa mfano Mwl anapowafundisha wanafunzi kusema mtakumbuka niliyowafundisha lakini hasemi kuwa mtamkumbuka yeye kama yeye.

Nimefuatilia hotuba za watangulizi wa JPM hata huwezi kukuta neno wamejisema wao kama wao kuwa "TUTAWAKUMBUKA". Je Mama yetu Samia Suluhu naye atakuwa anatukumbusha kwa kutuambia kwa maneno yake kuja kumkumbuka huko mbeleni?

Na je hatuwakumbuki watangulizi wa JPM pamoja na kutosema kwao kuwa tutawakumbuka wao kama wao? Just observation!
Marehemu Abeid Aman Karume alikuwa akisema hayo na sio hivyo tu alikuwa daima akisema kiasi gani cha fedha zanzibar inazo katika benki ya dunia na kama zikigawanya kila mzanzibari atapata kiasi gani.
 
Yeye alijua kafanya makubwa na lazima mumkumbuke kwa sabb hakuna atakaejitoa kama yeye.. Kusisitiza hivi alijua anastahili kuwa mfano mzuri kwa wajao sasa sijui kama wanaomlaumu kaum y wengi au vp
Mpaka kuomba kukumbukwa!
 
Au mabeberu wame-hack pacemaker!
Ingawa ni vipi hawasemi ingawa miaka yote ilikuwa siri nzito na hakuna alokuwa anajua kama marehemu anasumbuliwa na moyo. Maana watu wangelijua basi asingelikubaliwa na wapinzani na hata CCM wenyewe kugombani urais, kwa sababu sahrti moja la kugombea urais ni kuwa mgombea awe na afya njema. Ndio maana nashangaa siku tu iliyotanganzwa kufa amefariki kwa maradhi ya moyo, kikaratasi ya gazeti la miaka nenda kilipatikana na kurushwa mitandaoni na watu wasiojulikana!!!!
 
Back
Top Bottom