Ni Rais gani aliyepita Tanzania aliyewahi kufanya sherehe ya kutimiza mwaka mmoja madarakani

Kitu kikubwa kinachonipa hofu watu wanasifia mpaka wanapitiliza Yani kasoro hazisemwi ni sifaaa sifaaaa sifaaa mpaka basi,Kama mama asipokuwa makini na kukumbuka alipotoka atafeli Sana.
Hao ni chawa walimpotosha magu akavimbiwa
 
Tukielekea katika siku maalum ya kilele Cha sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja wa utawala wa raisi wa awamu ya sita nchini Tanzania,Nina maswali kadhaa kwa wadau wa siasa nchini.

Je ni raisi gani wa TANZANIA aliyewahi kufanya sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja tu wa madaraka yake?

Je Kuna kipi kipya ambacho kimefanyika katika mwaka mmoja huu ambacho hakikuanzishwa na mwenda zake?

Tatu je mwaka mmoja unatosha kweli kujipima kwa utendaji wa nchi kubwa Kama Tanzania yenye wakazi zaidi ya milioni 60.

Je, wananchi wanaichukuliaje hii sherehe na inamaslahi gani kwa wananchi wanyonge Kama Mimi?

Je, kutapatikana fursa ya kufanya tathmini ya kina ya kujikosoa ili kufanya maboresho katika nyanja mbalimbali za kiutendaji Kama serikali au shughuli itakuwa imemezwa na Sera za kusifu kila kitu?

Naombeni majibu wadau ili tusaidie kupeleka mbele gurudumu la Taifa tujadili kistaarabu tukitanguliza maslah mapana ya Taifa na uzalendo

Hayupo

Tulianza na J.K. Nyerere, hakuwahi kufanya hivi!

Akaja, A.H. Mwinyi hakuna kumbukumbu ya kufanya kitu hiki!.

Akaja B.W. Mkopa, hakuna kumbukumbu ya kufanya kitu hiki!

Akaja Msogaboy J.M. Kikwete, hakuna kumbukumbu ya kufanya kitu hiki!

Yaani hata mbabe, mpenda sifa J.P. Magufuli hakufanya kitu hiki!!

LABDA NDIYO ULE USEMI WA; "...Kila zama na kitabu chake". Yaani huyu mama naye anataka aandike kumbukumbu zake!

Lakini mimi naona anakabiliwa zaidi na tatizo la "insecurity" kunakopelekea akose kujiamini kiasi cha kutafuta extra ingredients anazodhani zitampa ukamilifu wa uhalali wake

Hili ndilo tatizo lililomkabili Bwana John Pombe Magufuli kiasi cha kuanza kutumia mamlaka yake vibaya kwa kufanya mambo ya kijinga na kipumbavu just kutafuta recognition
 
Tanzania Sisi Ni Wapuuzi.

Tanzania Ndio Wa kwanza Tunatumia Hela Nyingi Kusherekea Mwaka Mmoja Wa Kiongozi Bado tuko Nyuma Sana

umaskini Hauta Tuachaaa Kamweee
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom