Ni rahisi zaidi kupata mwenza sahihi mtandaoni kuliko kwenye dunia halisi!!

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,612
6,153
Kuna dhana kwamba, huwezi kupata mpenzi sahihi mtandaoni! Dhana hii inatokana na imani ya baadhi ya watu kwamba, wanawake wengi wanaotafuta wenza mtandaoni ni ama wahuni au matapeli, na wanaume wengi wanaotafuta wanawake mitandaoni lengo lao ni ngono tu na si vinginevyo.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba, wapo wanawake na wanaume wanaojiheshimu kweli kweli lakini wanatumia mitandao kupata wenza wao. Wanaamua kutumia mitandao si kwa lengo la kumpata wa kuridhisha tamaa zao za kimwili bali kwa lengo la kupata mwenza makini wanaoweza kudumu nao.

Kuna sababu kadhaa zinazowafanya watu watumie mitandao kutafuta wenza wao lakini kubwa ni ule ukweli kwamba, ulimwengu tuliouzoea unahamia Dunia Mtandao kwa kasi ya kutisha! Aidha, kutokana na watu kuwa na pilika nyingi za kimaisha, tunajikuta miongoni mwetu tunakosa muda wa kujichanganya ana kwa ana na jamii halisi na kujikuta tunajichanganya zaidi na jamii ya mtandaoni.

Mbuzi Ula Kwa Urefu wa Kamba Yake! Kwa mtu ambae pilika za maisha zinamfanya ajichanganye zaidi na dunia ya mtandaoni, huyu njia muafaka kwake kupata mwenza ni kutumia mitandao kwa sababu ndio ulimwengu wake!

Swali la msingi ni: Je, ni kweli unaweza kupata mwenza sahihi mtandaoni?

Jibu ni ndiyo. Jibu ni ndiyo kwa sababu zile zile nilizotaja mwazoni kabisa mwa mada hii. Kwa mwanamke; mwanaume anayeamini wanawake wa mtandaoni ni malaya tu, wala usishangae ile unaanza ku-chat nae tu, ndani ya muda mfupi anaanza kuongea habari za ngono kama vile kuomba Phone Sex! Na kwavile mitandaoni hatuonani, basi wengi wetu huwa tunashindwa kabisa kuficha tabia zetu halisi!

Hivyo basi, kwa mwanamke aliyeingia mtandaoni akiwa na nia thabiti ya kupata mwenza sahihi, hapo hapo atagundua kwamba aliyeanza ku-chat nae ni mwanaume wa hovyo kwa sababu mwanaume makini hawezi kuongelea masuala ya ngono ile mmekutana tu mtandaoni!

Lakini endapo mwanaume huyo huyo ungekutana nae ana kwa ana kwenye dunia ya kawaida, kuna uwezekano mkubwa angeficha makucha yake kiasi kwamba ungeamini yupo serious until it’s too late! Kwenye dunia ya kawaida wengi hawapo REAL kuelezea hisia za mapenzi bali wanaigiza.

Hata kwa wanaume, nako ni hivyo hivyo! Ni rahisi sana ile unaanza ku-chat na mwanamke tu, ndani ya muda mfupi anaanza kukuomba pesa ya lunch au mambo mengine kama hayo! Kwa mwanaume anayetafuta mwenza serious, hiyo inatosha kumpa tahadhali kwamba ana-chat na “mwanamke” wa aina gani! Tena watu kama hao wakati mwingine unaweza kukuta unayechati nae wala sio mwanamke bali ni mwanaume anayejifanya mwanamke ili ukiwa boya akuibie!

Je, uzoefu wako ni upi kwenye mahusiano ya mtandao? Endapo utataka ushauri au kuwa na swali lolote, utawasiliana na Dating Tanzania kupitia Support.
 
Kabla sijafungua uzi huu nilibet....."jamaa kuna mtandao atakuwa anaupigia debe" nafungua nakuta ni kweli! Yaani nikose mpenzi kwenye daladala, sokono, msibani, kanisani, nk nije kumpata kwenye id feki? Lipia tangazo lako
 
Kabla sijafungua uzi huu nilibet....."jamaa kuna mtandao atakuwa anaupigia debe" nafungua nakuta ni kweli! Yaani nikose mpenzi kwenye daladala, sokono, msibani, kanisani, nk nije kumpata kwenye id feki? Lipia tangazo lako
Hayo ni maoni yako na hukatazwi kutofautiana hata na dunia mzima, unakaribishwa kwa mawazo mengine zaidi na zaidi endapo hutajali!
 
Tofauti yao ni nini wakati Huyu wa mtandaoni tunaishi nae kwenye dunia halisi ?
 
Kumbuka hao hao hao waliopo mtandaoni ndiyo hao hao waliopo mtaani. Utofauti ni kwamba mtandao unakusanya watu wengi kutoka sehemu mbali mbali lkn mtaani unajikita ktk eneo mmoja. Ila kigezo cha kupata mpenzi mwema siyo rahisi kwasbb weng hawaamini mapenzi ya kwenye mtandaoni nikiwemo mm. Unaweza ukapata au usipate ni kama unavyotafuta mtaani.
 
Hakuna kinachoshindikana, nafurahishwa na watu wanaotoa ushuhuda wa kukutana na watu wa ndoto zao! Nina kila sababu ya kuamini wale wanaotoa ushuhuda, ingawaje kiukweli ni wachache sana, hawa ni wale waliokutana na watu wakatengeneza serious relationship ambayo ndiyo lengo letu hasa! Siamini mwanamke aliyekutana na mwanaume kwenye mtandao wetu kisha wakaishia Guest House; sidhani mtu kama huyo anaweza kutoa ushuhuda!
 
Ninapokutongoza maana yake nahitaji penzi lako, sasa nikutongoze alafu ukae mwaka mzima ili iweje we ni dadayangu? Yaani nijipeleke kibla kabla sijakukula nitangaze ndoa? Ntakuwa sina akili..
 
Hii mitandao kumpata mtu sahihi ni ngumu sana wengi ni watu walioshindikana au wenye tamaa za kimwili kwa wanaume au kwa wanawake sehemu ya kupata pesa au sehemu ya kupata ndoa maana huko walipo wameshindikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mitandao kumpata mtu sahihi ni ngumu sana wengi ni watu walioshindikana au wenye tamaa za kimwili kwa wanaume au kwa wanawake sehemu ya kupata pesa au sehemu ya kupata ndoa maana huko walipo wameshindikana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana Mkuu, wala si kwamba waliopo mitandaoni wengi ni wale walioshindikana! Mitandaoni ni kama kwenye dunia halisi tu! Walioshindikana wapo, kwa sababu wanatoka kwenye dunia halisi! Wenye tamaa za kimwili wapo, kwa sababu na wenyewe wanatoka kwenye dunia halisi ambako wenye tamaa wamejaa kila kona! Lakini na watu sahii pia wapo kutokana na mabadiliko ya kimaisha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom