Ni rahisi kuwa mbunge nchi hii kuliko kuwa mfagiaji wa bunge!!

Yudatade Edesi Shayo

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
2,903
4,306
Moja kati ya mambo yanayo fikirisha sana ni vigezo vilivyo wekwa kwa mtu kuwa mbunge,eti kujua kusoma na kuandika,ila ili uwe mfagiaji wa mbunge lazina uwe na cheti cha form four na certificate ya office attendants!!ajabu kabisa.

Kama tujuavyo bunge ni chombo cha kutunga sheria,kupitisha budget pia kufanya uchambuzi wa mambo yanayo gusa jamii kwenye nyanja za uchumi na sekta zote.je kigezo cha kusoma na kuandika kina weza kumpa tu uwezo kufanya critical analysis kuhusu mambo ya nayo gusa utii wa mgongo wa taifa linalotaka kuwa na maendeleo!!

Lakini dereva wa mbunge atatakiwa kuwa na cheti cha form four,sijuii cheti cha mechanics kutoka veta,cheti cha NIT ,sijuii cheti cha VIP.....mfuta vumbi tu nakupanga viti naye ana mlolongo utadhani anakwenda kutunga sera au ilani huko bungeni!kuna haja ya kufanya mabadiliko ili taifa lipate wabunge wasomi wenye uwezo waku jenga hoja kuhusu maslahi mapana ya nchi angalu hata diploma basi.

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom