Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Wapo watu wamejitwalia mamlaka za kuwafanya walio chini yao kama wanyama. Mtu anapigwa na dola Hadharani then dola inasema alikua mgonjwa na anayetamka hayo yupo mbele ya TV na hakuna anakemea.
Tunadhulumu watu haki ya ajira na hakuna wa kutuambia kwamba Taifa ni letu sote. Hakuna anayewakumbusha viongozi kwamba mishahara inalipwa na waajiri ambao ni wananchi.
Tunalazimisha watu watusikilize ila tunasahau kwamba hata wao wana upeo mkubwa kuliko sisi na tunachowazidi ni mamlaka tu.
Waliotangulia kuongoza walitupotosha kwa kisingizio cha uzalendo na ulinzi wetu, wanaotutawala pia wanatufundisha uzalendo bila kujua kwamba uzalendo haufundishwi. Wapo walioitwa wazalendo leo hii ni watuhumowa, ni suala la wakati.
Tusikilizane, tusimamie Hali, tuwaadhibu wanaokwamisha ndoto zetu