Ni rahisi kutenda wema kuliko ubaya na wema hauozi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Rafiki yangu kipenzi amefiwa na aunty yake. Gharama za kumsafisha marehemu mpaka kijijini alikozaliwa zilikuwa kubwa na familia haijiwezi sana. Huyu rafiki yangu alikwenda msibani na aliuliza michango iliyopatikana aliambiwa imepungua milioni 2 kukodi gari la kupelekea msiba kijijini.

Huyu rafiki alijitahidi na kupata milioni tatu. Aliwakabidhi akiwaambia hiyo moja isaidie kuendeshea msiba.

Alinieleza kuwa hii pesa na mwenyewe aliikopa lakini haijalishi mradi tatizo limepata usuluhishi. Alinieleza marehemu alikuwa jirani yao wakiwa wadogo. Alifiwa na mumewe muda mrefu na maisha yake siku za mwisho hayakuwa mazuri sana. Alikuja mjini kuishi na mdogo wake mpaka mauti yanamkuta.

Alinieleza jinsi marehemu alivyokuwa mkarinu wakiwa wadogo. Kuna siku alitoka boarding school kufika nyumbani mama yake amekwenda kwenye msiba kijijini kwao. Marehemu alimwambia awe anakwenda kula nyumbani kwake mpaka mama yake akirudi. Anasema aliona aibu, muda ukipopita yule mama alimfungia chakula na kipande cha mkate. Anasema alifanya hivyo kwa wiki nzima mpaka mama yake anarudi. Alimpa mkate wa kifungua kinywa kwa kesho asubuhi na chakula cha moto cha kula jioni.

Kwa kipindi chote yule mama akiwa kwa mdogo wake, weekend rafiki yangu huyu aliwapelekea kitweo na kila Christmas alimnunulia vitenge na khanga za sikukuu.

Yule mama hakujua kuwa mwanafunzi aliyempa chakula atakuja kumfaa sana mbele ya safari.
 
hii story ni very heartwarming ,,,asante kwa kushare nasi na kutukumbusha kuhusu kutenda wema,,
kwa maana kuna wakati unapita unasahau hata yale mema,,
From what we get, we can make a living; from what we give, however, makes a life.
 
Umeubariki sana moyo wangu. Neno la mungu linasema; Panda mbegu zako juu ya uso wa bahari. No wonder ipo siku utakula tunda usilojua lilipandwa na nani. Hata maiti imeheshimika kwa sababu alitenda mema katika uhai wake
 
Hivi unajua ukimsaidia mtu km huyoo ndio unafurahi, yaani unasema angalau na yy ameona msaada wangu, na hii pia inamfanya akumbuke kua hakukosea, huhisi hata kupungukiwa.

Kuna watu wengi sana wanalelewa na majirani n.k n.k, ukiuliza inakuwaje anakuambia 'niliishi vizuri sana na baba/mama yako, alikua rafk yangu',
kwaio unakuta anakusaidia akikumbuka urafki wake na mzazi wako.
Kuna wema mwingne mtu akikufanyia, hata km una roho katili iliyoje lazima utageuka nyuma.
 
Wema ...
Wemaaa...
Hauozi...tenda wema wende zako....
Wema huu huu ... mda mwengine unaponza!...majuto yake hayaishi daima maana hauozi!
 
Story hizi kuzisoma ni njema sana na zinatia faraja. Ila kuziishi zahitaji moyo wa ziada

Wakati mwingine wema una tu drain hadi undugu unauona mzigo

Pamoja na uhitaji wako , unajinyima , unahailisha ya kwako, unajidhabihu kwa ajili ya wengine lakini unaishia kuchekwa kuwa huyu ni fala tu.

Bahati mbaya ni Kama mfano huu ulioletwa kwenye Uzi huu, mtu alijitoa na anashuhudiwa kuwa alikua mtu mwema ila inaonekana amekufa akiwa duni ila kalipwa fedha ya jeneza na sanda na ng'ombe wa kuchinja. Kwangu huu ni ubatili na maisha yanaonekana hayana maana kabisa.
 
Kuna Dada mmoja ni mtu wa Bukoba wakati Mimi ni Mmaasai. Alikuwa CDO halmashauri ya wilaya flani, kipindi hicho nilikuwa nazungukazunguka kuomba misaada kwenye ofisi za serikali kwani Baba yangu alikufa mda mrefu ( aliniacha nikiwa na miezi 8 tu), na Mama yangu ni Mzee na masikini...

Sasa ikawa kila nikienda ustawi wa jamii, mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ananipiga tarehe Mara njoo kesho, njoo kesho hadi inafika ijumaa alafua ananiambia tena njoo j3, ikawa ni hivyo mda mrefu Sana. Huyo Dada akakerwa na tabia ya bosi wakekunihangaisha kila siku. Na kipindi hicho nilikuwa naishi kijijini ambako ni 7km kutoka mjini, manake Kwenda na kurudi ni 14km kila siku! Akaamua kunipokea yeye kwa mfuko Wake binafsi akanisomesha kwa kunilipia karo na matumizi. Alipokuja kuhamishwa kituo akawa ananitumia ela kwa M-PESA (kumbuka huyu ni mke wa MTU na yeye ana watu wanaomtegemea). Nilipomaliza O-level nikafaulu, akaniunganishia rafiki yake ambaye na yeye alinitambulisha kwa marafiki wake wengine, wakanichangia pesa nikaenda form five kwa amani.. Kwa sasa Niko chuo mwaka wa kwanza.

Kwa kweli huyo Dada, kwa vyovyote lazima nije kum- surprise angalau afurahi kwaajili yangu. Mawasiliano yanaendelea na mwaka huu mume wake ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa wilaya flani kule kigoma.

Popote ulipo Gladness Rugaimukamu, Mungu wa mbingu na nchi akupe miaka mingi yenye kheri duniani, akufundishe njia inayokupasa uendee na awafedheheshe adui zako siku zote za maisha yako, Amen.
 
Mungu ampe afya njema Gladness
 
Inapendeza sana...

Ina unaambiwa tena wema uende zako usisubiri malipo...

Huyo jirani alitenda wema sasa ameenda zake, malipo anayapata kwa wema wake alioutenda...

Cc: mahondaw
 
Story hizi kuzisoma ni njema sana na zinatia faraja. Ila kuziishi zahitaji moyo wa ziada

Wakati mwingine wema una tu drain hadi undugu unauona mzigo

Pamoja na uhitaji wako , unajinyima , unahailisha ya kwako, unajidhabihu kwa ajili ya wengine lakini unaishia kuchekwa kuwa huyu ni fala tu.

Bahati mbaya ni Kama mfano huu ulioletwa kwenye Uzi huu, mtu alijitoa na anashuhudiwa kuwa alikua mtu mwema ila inaonekana amekufa akiwa duni ila kalipwa fedha ya jeneza na sanda na ng'ombe wa kuchinja. Kwangu huu ni ubatili na maisha yanaonekana hayana maana kabisa.
Mara nyingi ikitokea msaada kwa familia panga SMART goals. Msaada uwe
Specific
Measurable
Achievable
Realistic
Time Limit

Unaweza kusaidia kumjengea sehemu ya kujistiri na unapanga kuwa katika miaka miwili nitakuwa nimemaliza au kumsomesha mtoto unajua kuwa baada ya miaka kumi nitakuwa nimemaliza
 
Back
Top Bottom