Ni rahisi kupita kwenye tundu la sindano kuliko kuajiriwa tanapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni rahisi kupita kwenye tundu la sindano kuliko kuajiriwa tanapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakende, Aug 18, 2012.

 1. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Katika siku chache zilizopita TANAPA (Tanzania National Parks) wameibuka kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa wao si wala rushwa, wala kuajiri kwa kujuana. Kama kuna secta chafu Tz zinazonuka rushwa na kujuana basi TANAPA ni namba moja. Kuna idadi kubwa ya wafanyakazi ndani ya TANAPA ambao ni wa ukoo mmoja, pia kuna wafanyakazi wengi ambao ni ndugu wa vigogo walioko makao makuu ya TANAPA Arusha. Kama huna kigogo ndugu yako pale TANAPA makao makuu Arusha uwezi pata kazi hata kama ungekuwa umefaulu kwa kiwango gani. Hawa jamaa uwaingiza gharama za kujiandaa kwa usaili watoto wa Watanzania wenzao huku wakijua kuwa kuna walioandaliwa kupata nafasi hizo. Kuna wafanyakazi wengine ambao hata hawakusoma maswala ya uhifadhi lakini wameajiriwa TANAPA

  Napenda kutumia nafasi hii kuwatahadharisha TANAPA kuwa waache mara moja propaganda zao za kujisafisha mbele ya Watanzania kuwa eti wao wako open katika kuajili. IWAPO HAWATAACHA HIZO PROPAGANDA TUTAANZA KUWATAJA VIGOGO WA TANAPA AMBAO WAMEINGIZA NDUGU ZAO NDANI YA TANAPA, MMOJA WA KIGOGO NI YULE ALIESTAAFU UHIFADHI MKUU KWENYE HIFADHI FULANI HUKO ARUSHA KISHA AKAPEWA MKATABA MAKAO MAKUU YA TANAPA NA AKAFANIKISHA KUAJILIWA KWA MWANAE MWAKA JANA
   
 2. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Du kweli noma
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tatizo halipo kwa wanaofanya recruitment, tatizo la tanapa lipo kwa wakubwa wa nchi hii! recruiters wanafuata maelekezo!
  kutangazwa kwa nafasi za kazi tanapa ni kiini macho tu!
   
 4. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,939
  Likes Received: 1,476
  Trophy Points: 280
  Very true Mungi,kwenye mashirika kama Tanapa memo ni nyingi!
   
 5. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Taja majina kwani imeshatokea wao ni wala rushwa.
   
 6. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnasubiri nini kuwataja?. Sisi tumesomea Uhifadhi tunasota mtaani ajira hakuna kumbe wengine wanapeana kindugu tu?.
   
 7. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnasubiri nini kuwataja?. Sisi tumesomea Uhifadhi tunasota mtaani ajira hakuna kumbe wengine wanapeana kindugu tu?.
   
 8. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnasubiri nini kuwataja?. Sisi tumesomea Uhifadhi tunasota mtaani ajira hakuna kumbe wengine wanapeana kindugu tu?.
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Pole sana mleta uzi kwa kero yako kuhusiana na ajira!

  Sema kwaupande wangu mimi sijapata kero kama yako, bali yangu mimi ni kuhusiana na hili zoezi walililolianzisha la ujazaji wa malipo kupitia TANAPA PREPAID CARD ya viingilio kuingia kwenye hifadhi za Tanazania National Park kupitia kwenye Bank ya CRDB!

  Kero yangu mimi sio CRDB Bank la hasha! kero yangu mimi kuu ni kuhusiana na hifandhi ya Arusha National Park! Unapokwenda kuweka malipo kulingana na wageni wangapi unaowapeleka kwenye hifadhi hii kupitia CRDB Bank na baadaya hapo unampatia dereva wako Card hiyo yenye kiasi cha dola za kimarekani sio kiasi cha shilingi hapana! nasisitiza tena sio shilingi za Kitanzania hapana! nazungumzia Dola za Kimarekani! baada ya hapo dereva anapofika kwenye geti la kuingilia kwenye hifadhi ya Arusha Natioanal Park na kufanya malipo hayo kupitia kwenye Card hiyo, wahusika baada ya kupitisha Card hiyo kwenye vyombo vyao kuhakiki kua Card ile ina hela wanadai kuwa Card hiyo haina hela na tena Card hiyo inadaiwa kiasi fulani, sio mara moja na sio mimi tu, kuna wakala wengi wa utalii kama mimi ambao wameshapatwa na kero hiyo mara nyingi na tumeshaandika barua kwenye vyombo husika bila kupata mafanikio yoyote hadi sasa.

  Ninachojiuliza mimi na wenzangu ni kua, kwanini isiwe kwenye mageti mengine kwenye hifadhi kama Serengeti,Lake Manyara,Tarangire??? halafu ndugu wadau wenzangu kwenye sekta hii matatizo kwenye hifadhi hii ya Arusha National Park hayakuanzia hapa kwenye zoezi hili, baada ya serikali na mamlaka husika kuanzisha zoezi hili kulipia kupitia TANAPA PREPAID CARD!

  Hapo nyuma tulikua tunalipa Cash Dola kabla zoezi hili la Card kuanza, lakini cha kushangaza hata hapo nyuma tulipokua tunalipa Cash Dolla unapofika hapo kwenye geti la malipo wahusika pale walikua na mashine za kuhakiki kua Dolla zile ni fresh au ni Fake! Lakini kulikua na usumbu mkubwa ambao unapolipa hizo Dolla Cash halafu wanapitisha kwenye mashine zile za kuhakiki wanadai kua hela zile ni Fake! Ilishawahi kunitokea mara nyingi enzi hizo, ninaporejea mjini na kwenda kwenye maduka ya kubadilishiwa pesa nakuta hela zile sio Fake kulikoni hifadhi ya Arusha Natioanal Park????

  Card ambazo nilishawahi weka pesa halafu nikaambiwa ninadaiwa na papo hapo nikawauliza nadaiwa nini mkakata hela zangu na hawakunipa ushirikiano, nimeshakwenda mpaka CRDB Bank waangalie shida nini kwenye Card hizo wao nao wakaniambia mbona sisi kwenye Card hizi tunacheki kwenye Sisteem na hatuoni tatizo lolote! Kweli sina ugonvi na hifandhi ya TANAPA lakini kwanini iwe ni geti la ARUSHA NATIONAL PARK PEKEE KWENYE USUMBUFU HUU NA SIO KWENYE MAGETI YA HIFANDHI NYINGINE?????
   
 10. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mbona tunakatishana tamaa maana si wengine tumeitwa Arusha kwenye interview tarehe 29 mwezi huu
   
 11. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wewe nenda ukafanye interview kama kweli wameona uzi huu labda watakuwa wamejirekebisha
   
 12. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  We subiri nitawataja siku nikiamka vibaya
   
 13. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Pole sana
   
 14. z

  zamlock JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  alafu vigogo wa tanapa ni mabilionea na nguo zao wanazo vaa ni spesho oda zimeandikwa majina yao na baadhi hao vigogo nawajua wanao vaa nguo zi,eandikwa majina yao, ilo siku nitawataja hapa jf, ni watu wachache lakini wanafaidi lasilmali za taifa hili utafikiri zipo kwa ajili yao tu. Lakini inau,a sana na iko siku haya yatapita
   
 15. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,845
  Trophy Points: 280
  hii ndio tanzania bwana...yapo mengi sana yaliyojificha nyuma ya pazia......
   
 16. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mtoa mada umeshindwa kuelewa kuwa wanaajiri watu ambao watafanya nao kazi vizuri na kwa ufanisi. wote walioitwa kwenye interview wana sifa zinazokakiwa kwa kazi hiyo, huwezi tena kulalamika eti uliye enda nae interview kapata na wewe umekosa. Unaweza kulalamika kama kuna mtu aliitwa interview bila qualifications, lakini kamwe huwezi kulalamikia watu waliopata kazi baada ya interview. Kwenye interview mwajiri baada ya kuangalia academic qualification anajikita kudadisi ni mtu gani ambaye atafanya naye kazi bila matatizo na kwa ufanishi, wapo wale wenye ma Phd na ma Dr, Dr lakini inapokuja kwenye kazi ni balaa tupu! sasa wale ambao waajiri tayari wanawajua kupitia recommendations za walikowahi kufanya kazi au kupitia ndugu na marafiki wana nafasi kubwa ya kupata kazi na mara nyingi waajiri wanapomwajiri mtu ambaye hawana habari zake za kikazi wanachukua risk, je atafaa mazingira yao ya kazi au la!! Hii ndo hali halisi ya kuajiriwa duniani kote!! Hapa suala ni kuwa serkali itoe ajira kwa wingi ili kama hukufaa TANAPA basi upate pengine panapokufaa badala ya kukaa na kulalama kwa mambo yasiyo na msingi
   
 17. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aha, aha, ngoja nimalizie msosi nitarudi punde
   
 18. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  slowly...ROAD WORK AHEAD!
   
 19. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu, its like you are trying to make sense somewhere, but yet i can not get you exactly, however you appear defending those TANAPA guys. ila pamoja na maneno yako bado suala ajira kwa vigezo fulanifulani lipo kwenye taasisi za serikali. ni SARATANI ya muda mrefu. hata TANAPA sidhani kama wamesalimika na hili. CHA MSINGI HAPA, TUPIGENI CHINI HILI LI SERIKALI LA CCM, TUPATE WASAA MZURI WA KUREKEBISHA HILI LI-MFUMO. kwa li-mfumo watanzania tutalalamika kila siku na haya majamaa yataendelea kutanua tu, DUDE LENYE SHIBE BHANA MWENYE NJAA HALIMTAMBUI KABISA. Halafu mengi yao hata imani za dini hayana, hayana hata hofu ya Mwenyezi Mungu.
   
Loading...