Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,115
- 35,126
Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu ametoa changamoto kwa CCM na wadau wengine wa siasa kuwezesha mdahalo baina yake na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, mheshimiwa Rais John Magufuli.
Wadadisi wengi wa kisiasa wanasema katu na kamwe hilo jambo halitaweza kutokea hapa nchini katika kipindi hichi kwa kuwa kinadharia mgombea mmojawapo hapo hana uwezo wa kushawishi kwa hoja, sio muumini wa kukosolewa na wala sio mtu mwenye kujiamini katika mazingira ya ushindani wa kisiasa majukwaani. Hivyo mdahalo utakuwa ni kama kumkaanga kisiasa.
Wengi tunapenda kuona wagombea wa urais wakipitishwa kwenye tanuru la mijadala mizito ikiwemo midahalo kabla ya wananchi kuamua kuwachagua. Na hii ingeweza kuwa fursa nzuri kwa Magufuli na Lissu kupimwa uwezo wao kisiasa kupitia mdahalo.
Hivi ni kweli CCM haiko tayari kukubali mgombea wake wa Urais 2020 kukupambanishwa katika mdahalo?
Nasubiri kuona CCM ikija ku-prove wrong kuhusu hili.