Ni rahisi kuiba pesa Bank za Tanzania. Makampuni ya Ulinzi Boresheni Ulinzi jamani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,771
2,000
Nimeona nandike hili kwa nia njema ili wenye Makampuni ya Ulinzi walifanyie kazi kwa ajili ya Usalama wa pesa za watu.
1. Walinzi wengi wa Makampuni haya ni washkaji sana na wamezoeana na watu kiasi kwamba huwa wanakuwa na Bench lao sehem wamekaa. Naizungumzia Bank moja katikati ya Jiji.jamaa hawa wa ulinzi huwa wanakuwa wamekaa kwenye Bench hilo huku wakipata kahawa, asubuh chai na mihogo inayopitishwa hapo njian. Unakuta wana earphones masikion na simu mikononi. Hili ni kosa la kiusalama.

2. Gari inayopeleka pesa mahali hapo route yake inafahamika na siku zake zinafahamika.lakini kabla pesa hazijapelekwa jamaa huwa wanapitia tawi flan wanashusha mzigo halafu wana mazoea ya kunywa uji au supu sehemu hiyo huku wakizungunga zunguka silaha zinaning'inia mabegani. Hili ni kosa la kiufundi sitawaambia kwa nini.

3. Walinzi wa bank hiyo huwa ni watu wasio na shaka hata ukikaa pale nje masaa matano unatizama sehemu waliyopo au movement wala hawajal kukufuatilia au kuja kuuliza unafanya nini muda wote huo. Hili ni kosa pia

4. Walinzi wote wanakaa sehemu moja tu kwenye lango kuu tena kwenye benchi pasipo kujali kuna backdoors.

5. Walinzi huwa hawahangaiki kwenda ndani kuangalia ni nini kinafanyika kwa maana wao ni kama wanalinda mlango tu. Hili ni kosa la kiufundi pia.


Hizo sababu tano nimeziweka wazi lakini kuna ambazo siwezi ziweka wazi kwa sababu wenye nia mbaya wasizitumie. Ila hizo tano nimeziweka wazi ili wenye kuhusika na ulinzi wazifanyie kazi haraka sana kwa ajili ya usalama wetu. Pia walinzi wawe na roho ya udadisi na umakini masaa 24.

Nimetimiza wajibu wangu. Kulisaidia taifa langu.
 

NZURI PESA

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
5,973
2,000
halafu kwanini taasisi ya fedha ilindwe na walinzi wa makampuni binafsi(tusaminiwe)?
ukitazama hata sare zao utajua tu kuwa jamaa mchovu hata malipo yake ni kizungumkuti halafu wanakabidhiwa majukumu mazito kama hayo na Askari wetu wa umma wapo inashangaza kwakweli sijui ni nini?
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,678
2,000
Pamoja na udhaifu huo, natamani siku moja ujaribu kufanya tukio la kuiba hapo benki alafu njoo utupe mrejesho.
 

sheremaya

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
2,857
2,000
Hiyo nayo ni mbinu ya ulinzi kama ulikua hujui hapo adui hasogei ng'ooooo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom