Ni rahisi kufanya tendo la aibu lakini ni vigumu kufuta aibu hiyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni rahisi kufanya tendo la aibu lakini ni vigumu kufuta aibu hiyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jun 6, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunao wajibu wa kujisikiliza wenyewe kabla hatujawasikiliza watu wengine, tunalazimika kujitazama wenyewe kabla marafiki na maadui hawajatutizama. Serikali yetu ninayoipenda imenipatia aibu mara nyingi sana. Imenisababishia maumivu makali moyoni na aibu isiyofutika kwa sababu watendaji wenye dhamana ya kutanzua vitendawili rahisi wamekuwa wakitoa majibu makubwa au wanafanya mambo ya ajabu ambayo wao wenyewe hawayaelewi.

  Akili ilyopikwa ikapikika ikipata aibu mara moja humwambia mhusika kuwa 'nimejifunza'. Maana ya kauli hii ni kwamba nikipata hali kama hii nitakukumbusha juu ya aibu iliyokufika jana, na kwamba aibu ya jana inakuepuasha kupata aibu nyingine.

  Watendaji wa serikali mbona hawajifunzi kuepuka aibu ya kushindwa kutoa tafsiri sahihi kwenye mambo madogo yanayopitia mezani kwao. Kwa mtaji huo serikali itaendelea kujifunga magori kila kukicha na CDM itaendelea kuvuna umaarufu kwa bei ndogo sana

  UJINGA WA MPINZANI WAKO NDIO MTAJI WAKO WA USHINDI.

  CDM tumieni fursa hiyo sasa mkishindwa hamna wa kumlaumu. MABEKI WAO WANAWAPIGIA PASI ZA KUFUNGA MAGOLI AMKENI FUNGENI MAGOLI MENGI HATA WAKIAMUKA WATASHINDWA KUYARUDISHA. Nionavyo mimi timu yenu shindani, haiamki kesho na hata pale ambapo tunadhani imeamka inapiga mpira kuelekea kwenye lango lao ambalo halina golikipa
   
Loading...