Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Mbona uandishi wako haufananii na unacho tuaminisha
nasupport asilimia mia moja ingawa umesema umepost kupima watu, but mimi nadiriki kusema Udsm ni kugumu aisee asiwaambie mtu, mimi nina akili nafahamu, ila nimetoka na lower second bcom Accounting ingawa nilikua na one zangu o level na advanced, yani chuo hata nisomeje nilikuwa nasoma kichizi ile second year na third ila naishia b plus hapo ndo nafaulu sana,tena hayo ni yale masomo mepesii kabisaa , ila mengine nilikua nachezea tu B plain na makarai, ila kuna jamaa mmoja kapiga tudarco hapo katoka na second upper yake wakati o level kapiga three na chuo hata alikua hasomi yupo bize na mishe kitaa, yani mimi ndo ningesoma sijui tudarco, ifm ,udom aisee ningepiga first class nna uhakikaaa , ila nataka nikajaribu hiyo ishu, nitaapply course nyingine ya undergraduate nichek itavokuwa
 
Elimu ya kuunga unga maana yake nini? Hao wanaounga wanafanya mitihani tofauti na wasiounga? Mtihani ni kipimo. Kama walifaulu mitihani hiyo neno kuunga halina mantiki yoyote.
Pole kama uliunga unga... unafika form four huapti alama tosha za kwenda A level. Unaenda certificate to diploma. Au unafanya qualifying test OPEN. ie foundation course. unapita. Then unakwenda University.. huko ni kuunga unga
 
Pole kama uliunga unga... unafika form four huapti alama tosha za kwenda A level. Unaenda certificate to diploma. Au unafanya qualifying test OPEN. ie foundation course. unapita. Then unakwenda University.. huko ni kuunga unga
Baadhi ya hao waliounga unga wamepata mafanikio makubwa Sana tofauti na wanaojisifia kuwa wameenda moja kwa moja.
 
Dr Mbura alikuwa anatufundisha Marketing, naskia pia alikuwa anapiga part-time udom, yule jamaa yuko fair sana ni lecture mwelewa alinikamata nimepigia quiz mtu ila hakunizingua, sasa angekuja mtu kama Dr.Minja au Dr.Siasa ndo mngeona true colors zao, so nadhani hao wanaokujaga udom ni among the cool ones.
We jamaa ungekuja Udom uone mziki wake. Sasa mbona malecture wa Ud ndo walikua wanatufundisha pia sisi?
 
Ukiachana na swala la udom kuwa na mitihani rahisi lakini ufaulu mzuri wa advance au olevel sio kigezo cha kafanya upate first class chuo.

Angalia petroleum engineering pale udsm watu wanakuja na division one za maana lakini mwisho wa siku hawatoboi kirahisi wanaanza 20 wanagraduate wawili au watatu. Ila kuna mtu katoka na three yake huko advance anaingia chuo na BAED yake anakupigia first class ya maana anapita hivi kwahiyo mi naona ugumu wa kozi tu.
Hapana sio ugumu was kozi,UDSM wanacomplicate Sana mambo,naungana natoa hoja labda Kama sikuelewa lakini no ukweli usiopingika kupata first class UDSMujue umepigana na mengi na bahati mbaya hata wao wenyewe walikuwa wanasema ( wakati huo nipo pale 2009) " Ulitaka kupata first class kirahisi nenda kasome tuvyuo twingine huko na sio hapa"
 
Hivi inakuaje mtu unajidai umesoma chuo kikuu lakini huwezi kutofautisha Lecture na Lecturer. Eti li Lecture mzuri!
Shame!
 
Wakati UDOM inanzishwa wahadhiri wengi walitoka UDSM, Mzumbe na SUA. So kwa upande wa wahadhiri wengi wametoka vyuo ulivyosifia.
Pia kumbuka vyuo vyote vina kasumba moja kua kufelisha wanafunzi wengi ndio ubora wa chuo hii kitu unatafuna wengi.
Cut point ya UDOM haitofautiani na vyuo vingine vya uma
 
UDOM ni kama Kampala University, First class huwa ni zaidi ya nusu ya darasa zima!
Kwa taarifa yako, UDOM mwaka huu 2019 hamna first class hata moja kwa college of education. Ktk college hii Kuna degree progms 11, na wanafunzi karibu 3,000...

Sijui hizo data mnazitoa wapi,
 
Ni vyema mkatupa hizo data in terms of numbers ili tufanye comparison ya hivyo vyuo. Mfano mtupe first class za kila chuo kwa mwaka huu na mwakajana tufananishe. La sivyo mtakuwa mnabishana hewan.
 
unajua ukiwa huna akili hta uwezo wako wa kufkr unakuwa mdogo zaidi UDOM capacity yake ni kubwa sasa utakaa ukinganishe result yake na Sjut yan chuo kichukue wanafunz 100,000 na kingine kichukue 10,000 then vyote vitoe GPA za 4 ziwe 70 hivi unaelewa hiki?
 
Ni upumbav tu wa hao malekchara hapo UDSM...NImepita hapo na nilikua nna fikiria hivyo(kwamba ambapo hazitoki 1st class nyingi ndo elimu bora) . Ila nipo huku dunia ya kwanza nilifanya bachela nyingine na vyuoni watu wanapiga distinksheni za kusaza ... Na ni kwenye hayo hayo masomo mnayoyarifaa kama magumu...(hili hata hata ukiwauliza hao ma Pro waliosoma nje watakwambia)

Ni mindset za maprofesa wetu juu ya sera ya chuo ndo mbovu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa unazungumzia UDOM ya Central African Republic. UDOM ya Tanzania na haswa Idara niliyopo First Class ya Kwanza na pekee baada ya miaka 10 ilipatikana mwaka jana. Lakini sasa, wana UDOM wenye GPA za 2.5 wanawashinda wenye GPA za 4 kutoka vyuo vingine vikiwepo ulivyovitaja inapokuja suala la interview. No Research No Freedom to Speak. By the way huwa Degree classifications hazitangazwi kwenye mahafali. Acheni kusumbua chuo pendwa cha watu.
Dah
 
vyuo vya kwetu
1-prof anacho kiamini wote tuamini
2-chalenji ya mwanafunzi na prof utakula ban kama JF kuoji sana
3-wanawake chuo watoboa kwa maprof maana kipindi cha toto kili wapita
4-ukiwa mjuaji chuo subiri disco la maisha
5-prof wanaendeshwa na vyama unaweza kukuta ni ccm alafu wewe ni mwana fulani
6-ma prof asilimia kubwa wanaona wameweza wewe chipukizi ujui wakati unaweza kuwa mchango au kuwa sehemu ya kukusogeza

hipo afrika
ukitaka kujua kwa nini wataalamu wanamalizia nje za nchi sio kwao tena tz
 
Hivi inakuaje mtu unajidai umesoma chuo kikuu lakini huwezi kutofautisha Lecture na Lecturer. Eti li Lecture mzuri!
Shame!

Vijana wanakwama wapi? Watajitetea kua sio lugha yetu! Aibu! Hawa ndio tunakutana na barua za maombi ya kazi wanaandika mijimaneno irrelevant kabisa alafu wanasema hawapati ajira
 
Back
Top Bottom