Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Nathan Jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
1,437
1,875
Ukihudhuria mahafali yao vyuo tajwa hapo juu; UDSM, IFM, SUA, MZUMBE si rahisi kusikia wanatangaza wanafunzi wenye first class wengi, utakuta wanne au watano hawazidi kumi mara nyingi.

Lakini ukienda UDOM utakuta first class wapo karibia 70 kwa course zote.

Sababu nini?
UDSM na IFM hawana walimu competent kama UDOM au walimu wao wanagawa marks ovyo? Au hakuna utaratibu wa kubana sana wanafunzi kama vyuo vingine?

UPDATE:
Wakuu mpaka sasa humjajua mantiki ya uzi wangu? Hapo ugreat thinker wenu uko wapi?

Hii nimeileta makusudi sana kuona mtazamo wa watu na mawazo ya watu juu ya ku urgue kwenye masuala ya msingi, kukosoa mtoa mada kwa data, kuleta uthibitisho mbali mbali,

Badala yake waliotoa uthibitisho na kuchangia kama wasomi ni wachache sana,

Lakini sababu ya kwani ni nimeanzisha uzi huu?

1. Kuangalia ni Watanzania wangapi bado wana mawazo potofu kwenye masuala ya kuamini chuo , bila kuangalia chuo kina deal na nini, ni yaani ulinganishe DUCE na Muhimbili? Automatically hata marks zao hazitaendana maana kuna baadhi ya course hazishabihiani hata kulinganishwa si vema.

2. Nimetaka kujua je hawa tunaowaita wasomi hapa JF wameshapunguza kusifia vyuo walivyosoma bila kufanya utafiti juu ya Vyuo vingine?

3. Bado kuna ulimbukeni wa kudhaniwa chuo kikuu ni kimoja tu UDSM, vingine ni usindikizaji?

4. Pia nilitaka kuona kama kuna atakaye leta maelezo thabiti juu ya CV za walimu au wahadhiri wa vyuo husika kwa sifa zao, bila tu kukaa kubishana kama watoto wa chekechea

5. Nilitegemea kuona kuna mapendekezo kadhaa juu ya nini kifanyike kuokoa elimu yetu ,yaani ni upuuzi kujisifia umetoka UDSM wakati kimataifa ni ya 17,300 kwa ranking.

Ni hayo tu

KUNA WATU WAMEANZA KUBEZA ELIMU YANGU AU MNATAKA NA VYETI KABISA?

KATORO PRIMARY SCHOOL 1992 - 1998
Nikafaulu tulitoka wawili kata nzima elimu bado ni elimu kwenda TABORA BOYS 1999 - 2002. Mwanaume nikakung'uta PTS 12. Nikajoin MINAKI HIGH SCHOOL 2003 - 2005 EGM. Nikakung'uta 6 PTS kwenda zangu B.COM IN CORPORATE FINANCE UDSM

Alafu mtu una elimu ya kuunga unga unajilinganisha na mimi. Uzi huu nimeuleta makusudi kutrick point fulani ambayo vyuo vingi vinagawa marks za free. Hatimaye tunazalisha wasio competent kazini

Nathan JR
 
Hujui UDOM wewe yaani vimitihani wanavyotoa hata mtoto mdogo anajibu ni mitihani lege lege, ukitaka iundwe Bodi ya Mitihani ya Vyuo Vikuu na mtihani wapige mmoja na UDSM, IFM, IRDP au SUA utaona maajabu,
Wewe utakuwa unazungumzia UDOM ya Central African Republic. UDOM ya Tanzania na haswa Idara niliyopo First Class ya Kwanza na pekee baada ya miaka 10 ilipatikana mwaka jana. Lakini sasa, wana UDOM wenye GPA za 2.5 wanawashinda wenye GPA za 4 kutoka vyuo vingine vikiwepo ulivyovitaja inapokuja suala la interview. No Research No Freedom to Speak. By the way huwa Degree classifications hazitangazwi kwenye mahafali. Acheni kusumbua chuo pendwa cha watu.
 
Ok so mtoa mada kasema uongo hakuna First Class 70 wala nini. Ahsante Mdau.
 
Ukiona watu wanafeli sana ujue hao hakuna kitu ni chenga tu, kama watu wanafaulu hao ndo wenyewe sasa.
Elimu yetu tunaipima kwa ufaulu, kama una GPA kubwa wewe ndo mkali na kama una GPA ndogo wewe ni kilaza hata kama umesoma chuo gani, kwahiyo kama hao UDOM wanapiga ma GPA first class hao ndo wakali.
 
Ukihudhuria mahafali yao vyuo tajwa hapo juu; UDSM, IFM, SUA, MZUMBE si rahisi kusikia wanatangaza wanafunzi wenye first class wengi, utakuta wanne au watano hawazidi kumi mara nyingi.

Lakini ukienda UDOM utakuta first class wapo karibia 70 kwa course zote.

Sababu nini?
UDSM na IFM hawana walimu competent kama UDOM au?
Right, Kampala University kuna mwaka walitoa First Class 20! (rekodi ya dunia) Wanafundisha sana, Lakini Chuo kimefungiwa kwa kukosa sifa! Maajabu!
 
UDSM hata kama uko vizuri wanakufelisha kusudi mkuu. Wanaamini kufelisha ndo ubora wa chuo
Mh hii ipo kweli? Hakuna process au uhuru wa kuappeal? Kama unajua umefaulu then kafelishwa je hakuna utaratibu wa kuappeal ili usahishiwe na mwalimu mwingine?
 
Kwanza kabisa UDOM kuna wanafunzi mafuriko ya kutosha. Hapa kama unajua basic maths utajua kwamba tukija kwenye hesabu za uwiano chuo cha IFM chenye wanafunzi 10 ukapata First Class 1 na UDOM penye wanafunzi 1000 ukapata First Class 100 ni kitu kile kile.
 
Ukiona watu wanafeli sana ujue hao hakuna kitu ni chenga tu, kama watu wanafaulu hao ndo wenyewe sasa.
Elimu yetu tunaipima kwa ufaulu, kama una GPA kubwa wewe ndo mkali na kama una GPA ndogo wewe ni kilaza hata kama umesoma chuo gani, kwahiyo kama hao UDOM wanapiga ma GPA first class hao ndo wakali.
Mkuu umenikumbusha Chuo cha Teophil Kisanji. Kwa staili hii vyuo vya private vitapiga hela balaa.
 
Kwanza kabisa UDOM kuna wanafunzi mafuriko ya kutosha. Hapa kama unajua basic maths utajua kwamba tukija kwenye hesabu za uwiano chuo cha IFM chenye wanafunzi 10 ukapata First Class 1 na UDOM penye wanafunzi 1000 ukapata First Class 100 ni kitu kile kile.
Na UD yenye wanafunzi more than 8000 walipaswa kuwa wanatoa more than 800 First Class
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom