Ni psychological problem au nature au ni kawaida? Msaada jamani

Ulilelewa na wazazi/mzazi wakali sana
ambao walikuwa chochote wanachosema huruhusiwi kupinga wala kujadili
na ukionesha kupinga tu cha moto unakiona so ili uwe safe ulikuwa unakubali tu
ili kuepusha shari..

kwahiyo sasa unaogopa tu watu kukuchukia ukipinga kitu
unataka sana kupendwa na kila mtu
Duuu hapa ndo nilipokwama na inanicost pakubwa
 
simple....tafuta kioo kaa chumbani pekeako kisha ongea mfululizo maneno yoyote yale kwa muda wa dk 10-15. kila siku asbh na jion . trust me utakuwa bora . pia jichanganye na watu wapya kila siku na jaribu kuongea neno yaan usitoke bila kuchangia kitu. fikirisha akili yako .
ajaribu hii mbinu itamsaidia.!
 
The first step ku deal na inferiority complex (Tatizo ambalo naamini unalo ama ulikuwa nalo)
Hatua ya kwanza ni kujikubali yaani usijilinganishe na watu try to appreciate what yourself. Pili una tatizo la Anti Social njia ya ku deal na hili jaribu sana kujichanganya na watu tofauti tofauti itakusaidia kwa kuanza anza na hayo.
 
naona ni spiritual problem
utakua una uwezo mkubwa wa kujenga hoja sasa huo uwezo umekamatwa rohoni as a result umekua muoga
jaribu kutafuta watumishi walio wazito kiroho wakusaidie
Tufafanulie kiundani zaidi ni kivipi, imekakaaje hii... ukiachana na haiba pamoja na mazingira ya mhusika in general hii naona mpya.

Tudadambulie plz katuwakilisha kijana mwenzetu huyu.
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye point....Mimi ni kijana mwenye umri kati ya miaka 25-27.

Nina shida moja kama siyo tatizo ambalo linanisumbua sana na ningependa kama kuna uwezekano niachane nalo kabisa japo nimejarb lakini nimeshindwa kwa mimi kama Mimi..

Nimekua na woga sana kama siyo hofu kiasi kwamba mbele za watu hasa ambao sijazoeana nao kwa mda mrefu..kwa mfano nimeajiriwa katika taasisi fulani yapata miezi mitatu tangu niajiriwe, lakini shida inakuja kama wenzangu wakiwa wanapiga story naogopa hata kuchangia.

Kwenye vikao vya ofisini ndio kabisa siwezi hata sema neno...hii imenisababishia mpaka najiona siwezi chochote....na nimekua mtu wa kukubali kila hoja itolewayo...yaani kama tunazungumzia kitu flani na watu wanachangia maada akiongea mtu yeyote Mimi hua naona yuko sahihi hata kama wenzangu watapinga..

Na akitokea mwingine akapinga yule wa mwanzo pia ninamuona tena huyu yuko sahihi...kiufupi nimekua cyo mtu wa msimamo..

Hali hii inanifanya hata hapa nilipo nishindwe kutembea nje..nimekua mtu wa ndani mda wote....

Ila cha kushangaza nataman sana kuwa msemaji mkuu kwa kila jambo tatizo nakua mzito kwa kila kitu..

Pia kingine kinachonishangaza kama mtu nimemzoea sana hua nakua huru kwa kila kitu..kwa mfano mwanamke wangu wangu hua nafanya vitu mpaka hunishangaa..husema "hivi huyu ndio ww kweli"..

Sasa wakuu nimekuja kwenu kuomba msaada kipi nifanye ili niweze ondokana na hii hofu maana nahisi inani athiri kisaikorojia.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom