`Ni pigo kubwa kwa Tanzania wahisani kupunguza bajeti' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

`Ni pigo kubwa kwa Tanzania wahisani kupunguza bajeti'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 16, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CUF)  Wabunge na viongozi wa vyama vya siasa, wamesema uamuzi wa wahisani kupunguza mchango wao kwenye bajeti ya serikali ya mwaka 2010/11, ni pigo kubwa kwa Tanzania kwa vile utaathiri huduma za jamii nchini.
  Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, alisema hali hiyo imesababishwa na serikali kupuuza malalamiko ya wadau kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato ya nchi.
  “Kama wadau tumeilalamikia sana serikali kwamba, kasi yetu ya ukusanyaji wa mapato haitoshi, Watanzania wanalipa kodi, lakini hawajui inachofanya, tumejitahidi kuiambia serikali hapa kuna mapato na pale kuna mapato, lakini haikusanyi. Matunda ni hayo,” alisema Dk. Slaa, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema).
  Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CUF), alisema uamuzi huo unasababishwa na mambo mengi, ikiwamo tabia ya serikali kuchukua hatua, ambazo zinachangia kufukuza misaada ya wahisani nchini.
  Alisema kwa mfano sheria ya kutaka makampuni yanayotoa huduma ya mawasiliano kulazimisha wajiorodheshe kwenye soko la hisa na kuuza hisa zao, inavunja moyo kwa vile hisa ni mali ya mtu, hivyo huwezi kumlazimisha kuiuza.
  Jussa, ambaye pia ni Mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alisema sababu nyingine, ni kutokuwapo na usimamizi mzuri katika masuala ya fedha na kupuuza mapendekezo ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya kutaka kuziba mianya ya upotevu wa mapato.
  Alisema sababu nyingine, ni tabia ya serikali kuvunja mikataba hovyo ya mashirika ya umma kwa tuhuma za ufisadi, kitendo ambacho alisema kinaangusha kiwango cha nafasi ya Tanzania katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
  “Ni pigo kubwa kwa Tanzania, kwani uamuzi huo wa wahisani utaathiri bajeti yenyewe na huduma za jamii,” alisema Jussa.
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alilaumu mfumo wa serikali kuendesha nchi kwa kutegemea ufadhili wa wahisani.
  “Hakuna taifa lolote duniani linaendelea kwa kutegemea ufadhili. Hivyo, tutumie kwa uangalifu rasilimali zetu na tusiruhusu wachache kumiliki uchumi wa nchi,” alisema Mbatia.
  Vyombo vya habari jana vilikariri taarifa ya wahisani ikieleza kuwa katika mwaka huo (wa 2010/11), watatoa Dola za Marekani milioni 534 sawa na (Sh. bilioni 721), ambazo ni pungufu kwa Dola za Marekani milioni 220 (sawa na Sh. bilioni 297) walizotoa mwaka 2009/2010.
  Wahisani wa bajeti ya serikali ni Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Canada, Denmark, Jumuiya ya Ulaya (EU), Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswisi, Uingereza na Benki ya Dunia (WB), ambao mwaka jana walichangia Sh. trilioni 1.9 katika bajeti ya serikali kupitia miradi ya maendeleo na mifuko ya kisekta.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...