Ni pasaka ya Tanzania Je wewe utavuka salama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni pasaka ya Tanzania Je wewe utavuka salama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ame, Apr 23, 2011.

 1. A

  Ame JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Pasaka ki historia ilianza pale wana wa Israel walipo kuwa katika maandalizi yao ya kwenda nchi ya ahadi baada ya kukaa miaka 400 wakiwa utumwani Misri. Manabii walisha tabiri kabla kuwa baada ya miaka hiyo wana wa Israel wata ondokana na maisha ya mateso na adha nyingi walizokuwa wakipata kwakuwa watumwa wa watu wa Misri. Ilikuwa ni nabii Daniel aliyekumbuka huo unabii akaamua kufungua vitabu vya kumbukumbu na kugundua kuwa muda huo ni muda ambao wana wa israel walipotakiwa kutoka na kwenda nchi watakayo pewa na bwana. Wakati nabii akipiga magoti kuuliza ahadi ya Mungu on the other side Mungu alikwisha mtanguliza kiongozi wao katika training kule machungani baada ya kukataa kukaa nyumba ya Pharaoh na ku enjoy huku ndugu zake wakiteseka. Picha gani unaipata hapa? si vyema kusherehekea sikukuu hizi bila kujua historia zake.

  Lakini miaka zaidi ya 2000 baada ya unabii wa nabii Isaya wana waisrael wanaletewa mtu mwingine kwa jina la Yohana akiwaambia tubuni maana ufalme wa Mungu umekaribia. Yohana kama Nabii Daniel anaelewa majira na wakati ambapo wana wa Israel hata baada ya kuwa katika nchi yao ya ahadi wameingia tena katika utumwa mwingine mbaya zaidi wa viongozi wao yaani Mafarisayo na masadukayo ambapo walitumia amri kumi za Mungu Musa alizopewa mlima Sinai kama moja ya njia ambazo waisrael wataendelea kula maziwa na asali katika nchi yao waliyopewa na bwana. Kinyume chake hizo amri zikageuka kuwa mizigo mizito waliobebeshwa waisrael huku viongozi wao wakifaidi kula maziwa na asali bila kuzigusa hizo amri kumi katika maisha yao zaidi ya kuyahubiri na kusimamia ndugu zao kuzifuata bila kuvunja hata moja.

  Ndipo Mungu mwenyewe akaamua kushuka kuacha utukufu wake kuja kulipa garama la deni mwanadamu alilopaswa kulilipa ili awe huru kwani alijiweka mateka mwenyewe na kuamua kuongozwa na shetani (Evil ways) kwakutumia sheria gandamizi zenye kumwibia mali zake; kuharibu utukufu wake na hata kumua pale ambapo anaona inastahili pasi na huruma. Yesu kama Musa anaifuata njia ile ile ya kuwakomboa wanawa Israel lakini safari hii wanawa Israel wanamkataa yesu na kuingia mkataba mwingine na ibilisi kumuua mkomb ozi wao. Nihadith ndefu lakini acha niifupishe kwa kuangalia safari ya Yesu kumkomboa mwanadamu. Alichagua kufa kifo cha msalaba kwanini? Nasema alichagua maana kama kufa kifo chochote angekufa akiwa mchanga Herode aliodhamiria kumuua ama nyakati tofauti alipozongwa nakutaka kuuawa lakini wakati mwingine alitoeka katikati yao. Pia kwa kawaida ya wayahudi mtu akihukumiwa kifo cha msalaba ambacho ni adhabu ya hali ya juu na yenye kufanya ufe taratibu ukiwa na maumivu makali sana na pia kwa desturi yao ni ishara ya kulaaniwa. Kwakuwa mtu huyu alipaswa kutokufa kabla ya kuangikwa msalabani ili asife kabla hajapata hasa utamu wa kifo cha msalaba haikumpasa mtu huyo kupewa adhabu yoyote bali kusindikizwa hadi kwenye kituo cha adhabu. Kinyume chake Yesu alibebeshwa msalaba; alipigwa mapigo arobain na kufanyiwa kila aina ya ubaya na bado aliweza kukamilisha safari yake mpaka pale Golgotha na kusema neno la mwisho IMEKWISHA!

  Mambo mawili nataka tuangalie hapa; hakuna kitu cha kimungu kinaweza fanyika duniani kabla ya nadharia hiyo kuwa kwanza katika ulimwengu wa kiroho yaani design na the real picture mpaka utimulifu wake. Pia hii blue print ikishatengenezwa na kupitishwa na expert wa mbinguni hakuna kitu cha tofauti kitatokea nje ya mpangilio uliopo katika ulimwengu wa roho ambao ndiyo permanent image ya kitu husika. Ukiangali pasaka ya leo ambapo yesu aliteswa akafa kazikwa na kisha kufufuka ilikuwa ni utimilizo wa unabii wa Isaya miaka zaidi ya 2000 kabla ya tukio. Ukisoma njia ya msalaba aliyopita Yesu hakuna hata moja ambacho nabii huyo hakukidocument vipi wana wa Israel washindwe kutambua hayo nao walikuwa wakisoma kitabu chao hicho cha torati na waalimu wao wakuu ndiyo waliokuwa wapinzani wakuu wa ujio wa Yesu na kuwa sehemu ya utimilisho bila kujua kile walichokitenda kilikua kinatimiza unabii wa Isaya?

  Naaishia hapa kwa kusema ni pasaka ya Tanzania je wewe ni miongoni mwa watakao vuka ama ndiyo hasa pamoja na kuwa mwelewa wa sheria za tanzania ukawa sehemu ya utimilifu wa unabii wa Tanzania kuvuka bahari ya Ufisadi? Mimi kama mhubiri ninawakumbusha kwamba JF kama nabii amekuwa akichora ramani yote ya safari ya ukombozi lakini hao hao members and guests wengine watakuwa sehemu ya utimilifu wa unabii huu. Ikiwa wewe ni mzaliwa wa kwanza katika nyumba ya ufisadi uwe na uhakika na kifo chako maana ni garika na sisi lazima tuile pasaka ya bwana. Wale wateuliwa wote inawapasa kuweka alama ya damu katika miimo ya nyumba zenu ili mwangamizi atakapopita asizidhuru nyumba zenu.

  Nawatakia pasaka njema!

  http://www.youtube.com/watch?v=KFrB9mni4Ug&feature=player_embedded
   
 2. A

  Ame JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2014
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwa muda wa miaka mitatu sasa unabii huu uliwekwa humu JF; mwenye macho haambiwi tazama. Ni swala la muda tu haijlishi ni lini lakini kwa hakika mafisadi kifo chao ni lazima na Tanzania njema lazima izaliwe.... Kila siku inatengeneza njia kuelekea hiyo njema!

  Baba wa Bwana wangu Yesu Kristo wanazareth, nakushukuru kwakua mambo haya uliwaficha wenye akili na busara ukawafunulia watoto wachanga! Uhimidiwe utukuzwe kwakua umesikia sauti ya mja kazi wako! Apear Lord that I may disappear!

  Glory, power, honor and majesty are yours forever and ever; AMEN!
   
 3. A

  Ame JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  ......naona tunaelekea kuzuri...Pharaho hajaamini kabisa kama wana wa Israel ndiyo hao wametokomea....katuma magari yake ya moto na askari wake kwa makumi elfu kuwarudisha wana wa Israel; waoooh......'Why cry to me move forward backward never asema Bwana wamajeshi mpiganaji hodari shujaa wa karne mzee wa miaka mingi' ..vita ya ukombozi ina garama yake the only good news is He paid all that we may conquer......Some one is about to be crowned, i cant wait to see!
   
 4. KATASAN'KAZA

  KATASAN'KAZA JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2015
  Joined: Jul 24, 2013
  Messages: 2,771
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Nape nape.....!
   
 5. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2015
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Itakuwa vizuri sana kama tutafanikiwa kuondokana na kadhia ya ujinga na ushenzi wa ccm.
   
 6. A

  Ame JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Stand still, sing praises the war is waged but the war is not yours is of the Lord "Jesus Christ of Nazareth" ..... The voice in the wilderness cries; Pharaoh, Israel is my son even a first born let him go that he may serve me, if you wont will kill your first born...."

  Glory be to your Holly and Glorious name God now days revealed to us as JESUS!
   
 7. A

  Ame JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Jesus! The tripartite equation is about to be balanced....


  Watu wapo vitani bila kujua command inatoka direction ipi.....

  Glory honor power majesty be unto your name Jesus forever more!

  http://youtu.be/1OPNvDPLaP8
   
Loading...