BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,040
- 10,459
- Thread starter
- #41
Comment yako inagusa Sana nipende kushukuru wewe na Wana JF kwa ujumla wao mawazo yao yamenipa mwangaza wa nini Cha Kufanya thanks alot.Mkuu pole sana.
Kuna watu wanatoa maoni kiurahisi sana, nadhani hawajawahi pitia hiyo hali.
Una familia mjini, wewe ndiye unayetegemewa kwa kila kitu
Unatafuta kwa jasho kila kukicha unapmbana mambo yakae Sawa.
Ghafla unahisiwa kuwa mwizi unakamatwa, mambo yanaanza kuyumbia hapa.
Unakaa polisi, familia haina wa kuwaangalia wanaanza teseka kwa kutoelewa hatima yako.
Akiba na mtaji uliyonayo ndani inaanza kutumika na hakuna kinachoingia.
Unaingia gharama zaidi kufuatilia swala lako kisheria umalize.
Unarudi mtaani umepoteza muda, Pesa na umeumia kisaikolojia, na akiba imetumika mtaji nao unaingizwa kwenye matumizi ya siku wakati ukitafuta jinsi ya kurudi kupambana tena.
Unaanza kufuatiliwa na serikali kila hatua katika mapambano huna amani hupumui, kila unapogusa wapo na wewe.
Inauma sana siyo siri.
Imewahi nitokea.
Inakatisha tamaa na kukujengea hali ya kisasi kikali kwa wote wanaohusika.
Brother kitaboy umeongea ukweli kabisa.
Hii nchi ukiwa real Hustler utapigwa vita sana na utajikuta adui wa serikali.
Kama jambo halijakukuta usibishe kuonyesha uzalendo wa kinafki.
BabaMorgan pole sana, naelewa jinsi unavyojisikia...
Mwanaume aliye kwisha kusimama na anaendesha maisha yake, then ghafla anarudi kijijini, wazee siyo rahisi kabisa na ni maamuzi yenye maumivu makali sana ndani.
Bro umezaliwa wa kiume, tumezaliwa kupambana, hatuna budi kukubaliana na hali wakati fulani.
Wewe hujafilisika ila WATU ndiyo walioingilia maisha yako kutaka kuyavuruga.
Rudi kaka, ila kamwe usiwasahau waliokufanya wewe kuwa hivyo.
Malipo ni hapahapa duniani.
Inauma sana Bro, ila hamna namna kaka.
Naongea haya kutokana na uzoefu kwakuwa yalishanikuta.