Ni njia ipi nzuri ya kuuza vitabu/courses na muziki online nikiwa Tanzania?

Vladimir Nacobov

New Member
Jun 14, 2021
2
45
Pamoja na kwamba mimi ni mgeni humu lakini naomba kupata mawazo juu ya uchapishaji kazi za sanaa online hususani vitabu, njia ambayo inaonekana sasa kuwa mkombozi kwa watunzi wengi tofauti na zile zama za giza ambazo ilimpasa mtu apige kwanza magoti kwa makampuni makubwa ndipo kazi yake iweze kuchapishwa.

Swali langu ni hili, Ukiachana na Amazon ambayo inaonekana kuwa bado na ukiritimba mkubwa kwa lugha ndogondogo kama kiswahili pamoja na njia isiyo rafiki ya malipo, ningependa kufahamu Platforms mpya za hapa nyumbani bongo kama vile kina GET VALUE na baadhi ya wengineo kwa aliyewahi kuapload kazi yake huko, je changamoto zake na faida ni zipi?

Pia kwa aliyewahi kununua products humo au courses, kuna changamoto zipi alizokutana nazo? Vipi unaweza ukasoma kitabu au kusikiliza audio books sawasawa na vile mtu ununuapo kutoka Amazon na kwingineko?

Nimeamua kuuliza maswali haya maanake naiona fursa kubwa ya kibiashara kwa watunzi wa kazi za sanaa na hata zile za kitaaluma. Naomba kuwasilisha!
 
STORIKA STUDIO

Verified Member
Jul 3, 2015
587
500
Pamoja na kwamba mimi ni mgeni humu lakini naomba kupata mawazo juu ya uchapishaji kazi za sanaa online hususani vitabu, njia ambayo inaonekana sasa kuwa mkombozi kwa watunzi wengi tofauti na zile zama za giza ambazo ilimpasa mtu apige kwanza magoti kwa makampuni makubwa ndipo kazi yake iweze kuchapishwa.
Njoo PM
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom