Ni njia ipi bora ya kuifanya biashara changa iweze kustawi kwa kasi?

Ukitaka biashara yako ikue kwa HARAKA zaidi,

Ukishatoa matumizi yote,
Kwa sikU Hutakiwi kutumia zaidi ya 10% ya faida yote uloingiza kwa sikU

Inamaana,
Kwa mfano umeuza laki 1, na ukapiga hesabu zako ukakuta faida yako Ni elfu 10.

Basi
Kama umeingiza faida ya 10,000 kwa sikU,
Hupaswi kutumia zaidi ya 1,000 kwa iyo sikU husika Kwenye matumizi yako yote ya binafs na familia.
Mkuu inategemea na Aina ya biashara mwingne biashara mauzo 3m faida haifiki hata laki
 
Mkuu inategemea na Aina ya biashara mwingne biashara mauzo 3m faida haifiki hata laki
Shukran mkuu!

Kama utakuwa na mchanganuo wa aina za biashara, zinazolipa kwa haraka na zinazolipa taratibu, unaweza dropisha hapa nifatilie kwa karibu Sana!
 
Uzi mzuri,Njia pekee ya kukuza biashara ni kujua Pesa inatengeneezwa katika hatua gani?Kwa mfano kama biashara yako ni kuuza na kununua basi lazima uhakikishe unajua ni katika hatua gani ya mchakato wako wa kununua na kuuza ndo unatengeneza pesa.Je unatengeneza pesa kwa kuwa na mzigo mkubwa(stock) au kwa kuwa na taarifa sahihi(information) au kwa kuwa na connection(Mtandao)

Kwa mfano unaweza kuwa dalali wa kuuza viwanja,mashamba nyumba na magari lakini wewe mwenyewe usiwa na nyumba,wala chochote anachokuwa nacho ni taarifa tu.

So ili nikupe ushauri mzuri ni lazima nijue unafanya biashara gani na unatengeneza pesa katika hatua gani ya mchakato wako wa kibiashara
 
Back
Top Bottom