Ni njia gani sahihi ya Kumtaarifu Mtu ' aliyefiwa ' na Mzazi au Mpenzi au Tegemeo lake au Mtu wake wa karibu sana?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,545
108,861
Mimi nina tabia moja kwamba nikijua kuwa fulani amefiwa na bado hana taarifa wakati Watu wengine wakijipanga jinsi ya Kumwambia / Kumtaarifu ili wasimuumize huwa namwambia moja kwa moja kuwa ' Oya Umefiwa na fulani ' kiasi kwamba hata akilia, akizimia na akiwehuka ghafla atajua mwenyewe lakini kuna Mtu kasema kuwa hapo nafanya vibaya.

Ameniambia kwamba Kiutaratibu ' Mfiwa ' huwa anatakiwa Kwanza Kupimwa ' Saikolojia ' yake ya wakati huo na kwamba yupo katika hali gani ili basi pale utakapompa tu hiyo taarifa aweze Kuipokea na Kuihimili. Ila Mimi GENTAMYCINE naona kama huo nao ni ' Unafiki ' tu kama ' Unafiki ' mwingine na kwamba Mtu ' akifiwa ' tu haijalishi yupo katika hali gani au nini anatakiwa aambiwe tu Ukweli kwani hata akifichwafichwa na Kuambiwa baadae bado ' Marehemu ' hatorudi tena kuendelea kuwa Hai kama Sisi.

Kuna Mtu ' Kitaa ' amefiwa na Mwanae tokea Alfajiri ya leo na mpaka sasa Watu wenye taarifa bado tu ' wanajadili ' jinsi ya Kumfahamisha kwani wanaogopa kutokana na kwamba huyu Mzee alikuwa akimpenda na akimtegemea mno huyu ' Marehemu ' Mwanae basi wakimwambia haraka wanaweza kuishia ' Kuzika ' Watu wawili ( yaani Baba na Mwanae )

Mimi nilichowaambia ni kwamba naingia Kwanza Kuoga muda huu na kwamba kama nikimaliza zangu tu Kuoga na nikakuta bado tu ' wanajadili ' jinsi ya Kumwambia / Kumtaarifu Baba yake Mimi GENTAMYCINE nitaenda moja kwa moja Nyumbani Kwake kisha nitapiga zangu Hodi, nitamsalimu na sitomchelewesha na hapo hapo nitamwambia kuwa Mpendwa Mwanae amekufa kama siyo amefariki kisha nafungua Mlango wake narudi zangu Ghettoni kujiandaa kwenda zangu Kushuhudia jinsi Timu yangu ya Liverpool FC inavyokuwa ' Bingwa ' leo huko nchini Uingereza katika EPL.

Mtu ameshafiwa na Mwanae mnamchelewesha tu ' Kumpasha ' zake. Yaani Waswahili sijui tuna tabia gani.

Nawasilisha.
 
Aisee nilivyo ona hiyo title ya uzi nikajua tayari umesha toa roho muhusika yule mwenye dalili za kukucheat.
 
Back
Top Bottom