Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,024
- 9,273
Siku nyingi nimekuwa nikisikia kauli kadha wa kadha, mathalani "mavazi haya ni kinyume cha maadili ya mtanzania", au kitendo alichokifanya juma cha ni "kinyume cha utamaduni wa Mtanzania". lakini sijapata kusikia kauli ya "wizi wa pesa ya umma ni kinyume cha Utamaduni wa mtanzania", au kusaini mikataba mibovu ni "kinyume cha utamaduni wa mtanzania" sasa mimi najiuliza je utamaduni wetu kama tunao ni upi?. je sisi watanzania values zetu ni zipi?. kama tunazo hizo values je Tunazikuza(kuziongeza) kadri muda unavypita au bado tunaendeleza stutus quo?.
je wakati wa mkoloni tulikuwa na values zipi na miaka 47 baada ya uhuru tunazo zipi?.
mimi ninadhani values za jamii ni kioo ambacho maendeleo yoyote tunayoyataka na kuyatafuta kwa udi na uvumba lazima ya reflect, kama hatuna values za maana ni vipi tutaendelea?
mjadala uko wazi