Ni nini Uganda wanafanya vizuri kwenye Soka hata kufanikiwa kwenda FAINALI under 20?

Ni kipi Watanzania tujifunze!

Mamlaka husika msijifungie ndani kula mihogo. Uganda karibu sana hapa.

Nendeni mkajifunze.
Mzee toka tz watolewe sijafatilia hii michuoano, haya nijuze uganda kachukua kombe?
 
Nje kidogo ya mada, waganda wamekomaa mnoo tofautisha na hawa madogo wanaoshindia chipsi yai hapo kinondoni ..
 
Kwwnza tuanchane na matokeo makubwa Sasa kwenye mpira ( kusajili wazee kwa kigezo cha uzoefu) ..tuache kupenda mteremko kwenye soka...Simba na Namungo zinatamba kimataifa kutokana. A uwepo wa wachezaji wengi wakigeni..haswa Simba .mfano katika first eleven ya simba ya uhakika..ambapo timu inaweza kushinda game ngumu..wachezaji wa kigeni wanakuwa zaidi ya 6-7 kwa wakati mmoja...

Hio haiji kwa makusudi. Bali ni ubora ubora ubora..wachezaji wengi wakitanzania wajidanganya na kudanganyika na ,mafanikio mafupi ya kusajiliwa ligi kuu..wengi hawataki kufikiria nnje ya boksi ..wengi wanaishi maisha ya maigizo..wengi ni hovyo. Hawakupita kwenye mifumo rasmi ya kukuza mchezaji..wengi hawajui basic skills za kuwa mchezaji..hawajitambui ...akili zao zimejaa ngono ,simba na yanga Basi.

Viongozi wa soka wako kwa maslahi yao..wanajiwaza wao kwanza..wanasajili wachezaji..wakiweka Sharti la kulipwa commission na wachezaji...wengi ni madalali wasiojua soka..wengi ni wachumia tumbo na wasio jua maana na faida za kuwekeza kwenye soka la vijana...wengi hawajui lolote kuhusu soka..zaidi ya mihemko yao ya soka.

Kiujumla soka la Tanzania ni sawa na mziki wa singeli
 
Back
Top Bottom