picture-picha
image-taswira
Picture je??? - au ni mchoro
"photo" ni kisawe cha "picture" ambapo yote yanatafsiri ya neno la Kiswahili "picha".
Mchoro neno lake la Kiingereza ni "drawing" na kisawe cha drawing ni "sketch". Nadhani huu ndio uelewa wangu, wenye kufahamu zaidi watasaidia.
Anaejua jamani mana huwa nachanganya tu matumiz yake.
Okey so kisawe ndio nn kwa kiingereza maana umeniacha hapo
synonym
Photo au photograph ni picha iliyotokana na chombo cha kuchukulia picha m.f Camera
Picture inaweza kuwa photograph au mchoro wa kitu ulioandaliwa kwa mkono.
Image ni taswira halisi ya kitu au blue print ya kitu inayoonyesha undani wa kitu kilichokusudiwa m.f Picha za X ray, CT scan au michoro ya ramani ya majengo iliyochorwa kwa karatasi maalum zenye kupitisha mwanga.
Kisawe ni neno la Kiswahili fasaha lenye maana ya neno au maneno yaliyo na maana yenye kufanana au kukaribiana, mfano neno "mwanamke" ni kisawe cha neno "msichana".
Kisawe (Kiswahili)= Synonym (English).
Karibu.