Ni nini tofauti ya maneno haya katika biblia? 'Mungu' na 'mungu' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini tofauti ya maneno haya katika biblia? 'Mungu' na 'mungu'

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Jumakidogo, Mar 14, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikisoma biblia na kukutana na neno Mungu likiandikwa ama kwa kuanza na herufi kubwa au herufi ndogo. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini neno hili huandikwa hivyo. Yaani unaweza kukuta limeandikwa 'Mungu' katikati ya sentensi kwa kuanza na herufi kubwa au unaweza kukuta pia limeandikwa 'mungu' katikati ya sentensi kwa kuanza na herufi ndogo. Hii imetumika hivi ikiwa na maana gani? Au hii ninayotumia imechapwa ikiwa na makosa ya kibinadamu? Pia kuna neno 'Bwana' na 'bwana' Nadhani wengi wetu tunajua vizuri kuandika katika lugha yetu ya kiswahili. Lakini hili limenipa utata kidogo. Angalizo; sitarajii ubishi na ushabiki wa kidini katika hili. Nimeuliza tu kwa ufupi nategemea majibu kutoka kwa wajuaji na hasa wanaoijua biblia ipasavyo.
   
 2. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  mungu ya ivi weka reference kucheck
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kama unaisoma sana biblia sidhani kama kuna haja ya kuwa na thread ndefu kutokana na ref nyingi. We soma hasa kwenye agano la kale utakutana nazo nyingi. Vinginevyo labda hii ninayo tumia mimi ina makosa.
   
 4. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hakuna utata wala makosa hapo kwa maana "Mungu" na "Bwana" hutumika anapozungumziwa Mungu wa kweli na "mungu" na "bwana" huzungumziwa anapotajwa mungu asiye wa kweli (Wa kishetani ambaye naye hupenda kujiita bwana katika himaya zake) au bwana wa kidunia yaani bosi nyapara au mume.
  Kwa hiyo "Mungu" si sawa na "mungu" au "miungu" na "Bwana" si sawa na "bwana" Ndiyo maana dinafsi siipendi na wala siiamini kabisa salamu ya "Bwana asifiwe" kwani
  ni vigumu kutofautisha nibwana yupi anayezungumziwa. Hivi kuna ugumu gani kutamka bayana Bwana Yesu Kristo Asifiwe au Tumsifu Yesu Kristu?
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Loh! Ushukuriwe. Nimekupata kwa namna murua kabisa.
   
 6. D

  DOMA JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mungu maana yake ndiye Mungu wa kweli lakini mungu ndiye pia huitwa mungu wa dunia hii ikimaanisha shetani
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Asalaam Aleykum. (Amani iwe juu yenu).
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umeniacha Hoi na hoi, kwa hiyo kuna Mungu na kuna mungu!
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hiyo avatar yako imeniacha hoi.... inafanana na mungu na sio Mungu....
   
 10. kiagata

  kiagata Senior Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Bwana J,pole sana na utata unaopata au uliopata katika kusoma Biblia.Jina/neno Bwana likiandikwa kwa herufi kubwa tupu yaani BWANA hili linamhusu mwenyezi kama waisrael walivyomtamka jah'weh au yehova. Ila ukikuta limeandikwa kwa herufi ndogo Bwana/bwana linamaanisha kiumbe mwingine mwenye mamraka anaweza kuwa nabii,maraika,shetani au hata mwanadamu.
  Na katika neno MUNGU au Mungu/mungu halina tofauti kama linavyojionyesha hapo juu,upande wa Mungu na upande wa mwanadamu.
  Wakati mwingine shetani anaitwa mungu wa ulimwengu;-MFANO.1. Yesu aliwambia wanafunzi wake shetani mungu wa ulimwengu huu amewafumba macho hata msiweze kuamini na kuokolewa.(nukuu toka agano jipya).
  MFANO.2 MUNGU akamwambia Mussa,wewe utakuwa mungu kwa Farao na Haruni ndugu yako atakuwa Nabii kwa Farao ili awape ruhusa waisraeli watoke Misri.(Hii ni baada ya Mussa kudai kuwa ana aibu na mdomo wake ni mzito kuongea.(nukuu toka agano la kale).
   
 11. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa ufafanuzi uliomwema ndugu yangu. BWANA Awe nawe.
   
 12. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  Tupe reference ni sehemu gani katika Biblia pa meandikwa ili tuweze kufuatilia na kutoa michango yetu.
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kuandika neno 'Mungu' au 'mungu', hakubadilishi maana, kwa sababu kuna lugha ambazo hazina upper or lowercase. Lugha ya kiingereza zamani walikuwa wakiandika kwa herufi kubwa kabla ya kubadilisha na kuandika herufi kubwa kwenye jina la mtu, na baadae wakaja kubadilisha na kufuata mfumo huu ambao tumeuzoea.


  Kuandika neno 'Mungu' kwa herufi kubwa, inasemekeana ni kwa ajili ya insult theists tu, na wao kwa kulipa kwao uandika kwa kuanza na herufi ndogo kwa madhumuni hayo hayo.


  Lakini unapozungumza au kutoa mahubiri ni vipi unaweza kulitofautisha neno 'Mungu' na 'mungu' kiukweli uwezi kutofautisha, kwa sababu yote yanatamkika kwa namna moja.


  Hapo juu nimedokeza kuwa kuna lugha ambazo hazina herufi kubwa na ndogo. Mfano lugha ya Kihebrania (Hebrew) na Kiarabu (Arab), ambazo ambazo kimatamshi zinashabihiana na uandikwa kwa kutokea kulia kuelekea kushoto, najuwa wengi watashangaa, lakini ndivyo zinavyo andikwa na hazitumii herufi kubwa na ndogo, ila tunapo tafsiri machapisho ya Kihebrania na Kiarabu basi tunafuata utaratibu tuliouzoea na kuandika kwa kutumia herufi kubwa na ndogo pale tunapo ona panafaa. Na tukihamisha maandishi kutoka kwenye lugha zetu aidha Kiswahili au Kiingereza, basi tutafuata taratibu zao kwa kuwa taratibu zao za kiuandishi ni tofauti na lugha zingine.


  Lugha zingine ambazo hazina herufi kubwa na ndogo ni Arabic, Hebrew, Hindi, Tamil, Chinese, Japanese, Gujarati, Thai... Kwa ufupi karibia lugha zote ambazo hazina asili ya herufi za Kilatini hazina herufi kubwa na ndogo...

  Na tunapozungumza hatutofautishi kati ya herufi kubwa na ndogo.
   
 14. d

  dav22 JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  aisee nimeisoma hii
   
 15. kiagata

  kiagata Senior Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Kaka habari,umenipa muda wa kufikiria upya kuhusu lugha za awali zilizotumika kuandika Biblia.
  Nitatafuta vitabu kuona kama kuna tofauti zaidi kuhusu mungu na MUNGU.
  Ila katika Biblia Takatifu ukianza kuifungua tu,utakutana na neno TUNZA.Neno BWANA/BWANA lionekanapo kuandikwa kwa herufi kubwa basi ni lile jina lenye KUMHUSU mungu mweza yote au Yehova kama walivyoita Wayahudi ktk lughaya kiaramu.Sasa hapa lazima tofauti iwepo kati ya herufi kubwa na ndogo kama sivyo basi hata kwa kukoleza wino katika neno husika.
   
 16. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mwanajamvi X-PASTER anaelekea kutumia maneno mengi ya ushawishi huku ndani mwake mmejaa ghiliba (fallacies) tupu! Maneno "MUNGU" na "mungu"/"BWANA" na "bwana" ya tofauti kwa namna yoyote ile. Neno lenye herufi kubwa linamaanisha MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI alhali 'mungu' linamaanisha miungu ambao kila mahali wametapakaa hadi ngazi ya familia. Hawa "gods" huabudiwa kwa namna ambayo haijulikani kwa wengi. Sasa mwanajamvi anapohusisha otografia ya maneno hayo na semantiki yao anakauwa hatendi haki. Labda tu atuhakikishie ikiwa yuko katika mahubiri ya kum-promote huyo "mungu" watu wengine wamkiri na kumuamini!!!!
   
Loading...