Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,782
Case study ya Mfanyabiashara Khamis Ntunzwe... Mtu aliyepitia madhila mengi mabaya na ya kuhuzunisha sana kisa tu aligoma kutoa hongo ya milioni 2 kwa watoza ushuru
Watoza ushuru hata misahafu inawatambua.. Ni wachafu ni wadhambi, si watu wa haki ama haki zao zina makengeza.. Ni watu katili na waliokosa utu...
Watoza ushuru wana utatu wao.. Utatu wao huu ni mtakatifu kama ule wa wakristo.. Utatu wao ni haramu kwa ajili ya kukamilisha upigaji?
1. Mtoza ushuru
2. Askari polisi
3. Dalali
Ogopa sana hiyo chemistry combination ya huo utatu.. Uki temper nao.. Umekwisha...
Nitamcheka na kumdhihaki yeyote atakayesimama kifua mbele ya kadamnasi na kujitapa kuwa Tanzania ni taifa linalosimamia haki na kuzigatia utawala wa sheria pamoja na kuheshimu haki za binadamu.. Wakati kuna madudu ya kutisha kwenye kesi moja tu kama hii ya Ntunzwe ukiacha ile ya yule kijana wa Moshi aliyedhulumiwa gari yake... Kesi zote mbili zinaihusu mamlaka yetu ya mapato na watendaji wake...
Juzi tumetoka kumzika kijana dereva wa boda. Alinyongwa na kupokonywa pikipiki yake isiyozidi thamani ya milioni 3.. Kwa hesabu za haraka wauaji watauza kwa milioni moja na kugawana laki 5 kila mmoja.. Ntunzwe kapoteza dada yake kwa kugoma kutoa hongo ya milioni 2.. Yani kama hao maofisa watoza ushuru wanne wangefanikiwa kupata hicho kiasi pengine wangegawana laki 5 kila mmoja
Hawa wana tofauti gani na wauaji wa boda boda!? Tofauti yao ni
Elimu
Mavazi
Dhamana yao kwenye jamii
Kipato
Ajira
Lakini linapokuja suala la pesa za haramu hawana tofauti kabisa... Wote ni wauaji wakubwa
Ntunzwe kajitoa mhanga.. Madhila yamekuwa mengi mpaka kaamua liwale naliwe... Kakoswakoswa kuhitimishwa uhai.. Je ni wangapi wamesalimika kama yeye baada ya kuingia kwenye mikono inukayo damu ya mumiani?
Walimwaga ugali, sasa yeye kamwaga kitoweo... Habari iko full episode YouTube.. The soonest itanaswa na wambea wa dunia BBC, DW nk.. Uozo na uvundo wa Mamlaka yetu ya mapato inayojivunia kukidhi viwango vya ISO vitaanikwa mchana kweupee.. Watendaji wake majangili wezi na wachumia tumbo... Kwa majina dunia itawafahamu..
Ogopa sana mtu anayejiamini, aliyeumizwa sana na mwishoni kukata tamaa.. Muogope sana.. Ntunzwe kafanya kilichowashinda wengi... Lakini ni baada ya kikomo cha uvumilivu kumfika pomoni...
Sasa kila kitu hadharani... Tutasimama na raia mmoja aitwaye Ntunzwe? Na serikali yote iabike kwa kushindwa na seven leaver.. Ama tutayavaa mabomu na kunyorosha rula ili ili dhana ya uwajibikaji ichukue nafasi yake na kila mmoja kubeba mzigo wake?
Ya kwamba Mamlaka ya mapato kwa adhabu tofauti tofauti iwawajibishe watendaji wake wajuu kabisa, wa kati na wa chini kabisa wasiopungua 15?
Ya kwamba jeshi la polisi liwawajibishe askari wake na viongozi wao waliokalia jalada la uchunguzi kwa miaka mitatu bila Maendeleo yoyote?
Ya kwamba chama cha wafanyabiashara Tanzania kimwajibishe Katibu wake kwa kutaka KUJARIBU kufanya patano haramu.. Hapa kukiwa na wafanyabiashara wakihusishwa na mmoja kutajwa kwa jina kabisa?
Ya kwamba huyu dalali Yono naye aachwe tu? Kesi hii ni mfano mmoja kati ya maelfu ya kesi wanazokumbana nazo wafanyabiashara Tanzania.. Na wengi huishia kukata tamaa kutokana na formalities nyingi na kutishwa.... Ntunzwe kapiga PABAYA mno.... Na kabamiza hasa.. Ana rundo la USHAHIDI wa nyaraka mpaka na sauti zilizorekodiwa...
Macho na masikio yote sasa ni Mamlaka za juu za nchi.... Je utatumika uzi kunyoosha mstari ama itatumika rula? Ntunzwe anastahili pongezi, pole na hongera... Hata akikoma kuwa leo kila kitu keshaweka hadharani....
Good morning Tanganyika!
Jr