Ni nini Tin namba, kwa nini wafanyakazi hawana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini Tin namba, kwa nini wafanyakazi hawana?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shedafa, Aug 29, 2012.

 1. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwa maelezo Tin namba ni utambulisho wa mlipa kodi, sasa mbona wafanyakazi hawana au hawalipi kodi?. Inaonekana kama ni maalum kwa wafanya biashara tu, lakini unapohitaji huduma za kiserekali hata kama ni mfanyakazi unaulizwa tin namba. Je, hii inamaana wafanyakazi hawalipi kodi?
  Ufafanuzi tafadhali
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Wanalipa sana tena wao ni kwa % ya mshahara tofauti na Mfanyabiashara ambapo asilimia 70 wanakwepa.
  ni Dsm, Mwanza ,Arusha labda Mbeya na Tanga ndio wanaolipa Kodi hasa TRA
  Uwe na gari, Pikipiki hata km ni Mfanyakazi utalipa Kodi kupitia Tax idintyifying number
   
 3. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sasa kwa nini hawana tin namba?. Kwa inavyoonekana njia hii ya kuwa na tin ndio inatambulika kuwa ni kodi na wala si nyingine yoyote. Chukulia mfano wewe ni mfanyakazi na una kibanda chako unataka kukilipia kodi, itakulazimu kufuata mlolongo mrefu kama mfanya biashara ili kupata tin namba. Kwa nini wafanyakazi wasipewe tin namba moja kwa moja kwa kuwa wanakatwa kodi katika kila pato wanalopata?, hii si kuonyesha ni jinsi gani wasivyothaminiwa?
   
 4. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu TIN ni namba
  Ya utambulisho ya mlipakodi,mfanyakazi ni mlipakodi ndio,je analipa moja kwa moja?jibu ni hapana kuna withholding agent ambaye ni mwajiri wako yeye lazima awe na TIN coz analipa kodi ile aliyokukata
  Huna haja ya TIN kama umeajiriwa tu na huna shughuli nyingne yoyote ya kuingiza kipato zaidi ya ajira hakuna sababu ya kuwa na TIN kwa sababu moja tu mfanyakazi hana haja ya TIN kwa ajili ya makato yake ya kodi kwenye mshahara...sasa unapokuwa na shughuli nyingne hapo sasa ni lazima uwe na tin maana yake hata kama una gari la jina lako ni lazima uwe na TIN ili TRA ikutambue kama mlipakodi wa moja kwa moja...kuhusu kupanga foleni na kufuata utaratibu ni sahihi otherwise unataka preferential treatment...
   
 5. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu sisi watumishi tuna cheque namba mkuu, tunalipa kodi sana hakuna kukwepa. Cheque namba ikiguswa tu inaathiri moja kwa moja salio mkuu tofauti na wapiga biznez mpaka mtafutwe na TRA,

  Cheque namba ogopa sana hii kitu.
   
 6. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwanza naomba nieleweke kuwa nami ni mwajiriwa vilevile. Nikirudi kwenye mada, sipingi haya maelezo yenu kinachonipa taabu ni faida linayopata kundi moja na kundi jingine kutopata wakati majukumu yanafanana. Wote tuwalipa kodi, pengine wafanyakazi ndio tunaolipa vizuri zaidi na kodi ya kuaminika zaidi. Inapokuja kwenye huduma hatutambuliwi kuwa tu walipa kodi kwa nini?, mfano ni kwa nini wakati tunapotaka huduma za serikali kama wakati wa kushughulikia gari, nyumba na n.k. hiki kinachoitwa cheque namba kisitumike?. Maana ya rahisi ni kuwa hatulipi kodi, hivyo inabidi kujiandikisha kuwa walipa kodi. Hii haijakaa sawa, naomba ufafanuzi zaidi.
  Nawakilisha!.
   
 7. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Ni kweli haijakaa sawa
   
 8. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Point of Clarification;
  TIN means~Taxpayers Identification Numbers.

  Thus huna haja ya kuiita "TIN namba"; ukisema TIN inakuwa imejitosheleza.
   
 9. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Asante Pinokyo!
  Ungeza na mchango wako basi kwenye mada!
   
 10. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naona umekuwa mgumu kuelewa...jibu ni hivi kama ww umeajiriwa na huna shughuli nyingine yeyote huna haja ya TIN kwa sababu moja tu..mwajiri wako anawasilisha malipo kwa niaba yako hivyo huitaji TIN hayo mambo ya cheque namba ni uzushi tu hakuna swala kama hilo..kama malipo yanafanyika kwa cheki basi cheki lazima iwe na namba na kila cheque ina namba yake...wewe unachohitaji ni preferential treatment ukienda ofisi za TRA kwa kuwa ni mfanyakazi well hicho kitu hakuna kwa sababu wapo watu au makampuni yanayolipa kodi kubwa zaidi yako na wanapanga foleni...fanya ubongo wako uwe laini uweze kuelewa hiki ninachokwambia,..
   
 11. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Du mkuu umeamua kunishikia kisawasawa, hata sijui unataka nielewe nini hapa!. Haya tutafika. Labda nikuulize shwali dogo tu, wewe unaona sawa ukiwa kama mfanyakazi unataka kulipia gari lako unaulizwa tin na wala hawajali kama wewe umeajiriwa na unalipa kodi?. Wakati mfanyabiashara akitaka kulipia gari lake wala haitaji cheque namba anatoa tin yake tu?, ukizingatia kuwa tin ni mfumo wa kodi kwa wafanyabiashara na wafanyakazi wana mfumo mwengine!.
   
 12. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
   
 13. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
   
 14. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni sawa..ni utumiaji mbovu wa maduhuli ya serikali iwapo kila mfanyakazi apewe tin then akaweke kabatini..ukiwa na gari na limesajiliwa inamaana tayari una tin
   
 15. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu mgumu wa kuelewa wewe!. Shida yangu ni mfanyakazi atambuliwe kama ni mlipa kodi kama anavyotambuliwa mfanyabiashara basi, iwe kwa kumpa Tin au kwa namna nyingine. Wewe unagombania maduhuli sijui nini, yote ya nini. Kama wewe unaona ni matumizi mabaya kinachofanyika sasa ni nini, mfanyakazi anapewe tin anakwenda kuiweka kabatini kama unavyosema hamna kinachookolewa hapa. Sana sana kinachofanyika ni kumfanya ajione hana thamani kwa kumsotesha kwenye foloni pengine siku nzima, wakati kama ni suala la kulipa kodi analipa. Ingekuwa rahisi angepewa automatic, kingetumika kitambulisho cha kazi kuonyesha ni mlipa kodi basi.
   
 16. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,133
  Likes Received: 7,382
  Trophy Points: 280
  Haija-specify Kama huyo taxpayer ni mfanyabiashara au mfanyakazi.
  So muuliZa swali yuko right.
   
 17. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Amini amini nakwambia, yawezekana huyo mfanyakazi unayemji analipa kodi kubwa kuliko TBL kama utatafuta thamani ya hiyo kodi toka kwa mlipaji! Kwa hiyo hoja ya huyu GT ni ya msingi kuliko majibu rahisi unayotoa.
   
 18. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  nimekuwa nikujaribu kuedit post yangu ya kwanza katrika huu uzi ila naona inanisumbua katika kuedit post yangu mod wananiambia sina permission, hivyo imenibidi niikopy na kupaste kwenye hii post mpya ili niwee kutoa darasa lenye link inzuri
  income tax act 2004 S. 133 inaelezea kuwa
  "
  (2) Every resident person who carries on a business anywhere and non-resident person who carries on a business in the United Republic shall apply, in the prescribed form, to the Commissioner for a tax identification number within 15 days of beginning to carry on the business.(3) All persons shall show their tax identification number, if they have one, in any claim, notice, return, statement or other document used for the purposes of this Act.
  (4) Subject to any written direction by the Commissioner to the contrary, every institution specified in the First column of the Fourth Schedule shall require a taxpayer identification number from any person applying for the matters or engaged in the transactions listed in the second column of the Fourth Schedule.
  hiyo ndiyo primary use ya TIN, Swali linakuja je mfanyakazi ni mfanyabiashara? Jibu kimoyomoyo.
  Swali linakuja; kwa nini unapotaka kusajili gari unaulizwa TIN?
  Kujibu hili swali inabidi tuende kwenye jedwali la 4 la sheria hii ya kodi ambayo inatoa matumizi ya ziada ya TIN
  FOURTH SCHEDULE
  ______
  (Made under section 133(5))
  ______
  TRANSACTIONS FOR WHICH TAXPAYER IDENTIFICATION NUMBER IS REQUIRED
  1. Commissioner General of the Tanzania Revenue Authority
  Registration of ownership or transfer of vehicles under the Road Traffic Act, 1973 and licensing of motor vehicles under the Transport Licensing Act, 1973
  2. Commissioner for Lands
  Registration of title upon transfer of ownership
  3. Central and Local Government
  Trade licence
  4. Business Registration and Licensing Authority(BRELA)
  New registrations
  5. Registrar of Patents and Trade
  Service Marks New registrations
  6. Ministry of Industry and Commerce
  Trade licensing and industrial licensing
  7. Ministry of Natural Resources and Tourism
  Licensing
  8. Ministry of Energy and Minerals
  Licensing
  9. Commissioner for VAT
  New registrations(VAT Reg)
  10. Commissioner for Customs and Excise
  Importation of goods; customs clearing and forwarding
  11. All Government Ministries, Government Agencies, Local Government Authorities, Financial Institutions, Cooperative Societies and public bodies
  All contracts, including contracts of supply of goods and services
  NB MAANDISHI YOTE YENYE “BLUE” NDIYO YANAKUPA WEWE SABABU YA KUWA MA TIN, NA MAANNDISHI YENYE “BLACK” NI TAASISI ZITAKAZOHITAJI TIN YAKO.
  HIvyo basi hii inaashiria kuwa hakuna sehemu katika sheria inayosema mfanyakazi awe na TIN tu kwa sababu analipa PAYE, hata wakati wa kujaza ile fomu ya kuomba TIN ukiandika sababu ya kuomba TIN ni tofauti ni zilizoko kwenye jedwali la 4 la kodi ya mapato ya mwaka 2004 RE 2006 huwezi pewa, na lengo la kuwa na TIN ni kuhakikisha kila mtu anayestahiki kulipa kodi analipa, na katika wafanyakazi wa serikali na sekta binfsi anayebanwa si mfanyakazi ni mwajiri na ndiyo maana hujawahi kusikia mfanyakazi amefuatiliwa na TRA kwa kutokulipa PAYE.hivyo wanatumia mwajiri kuhakikisha mfanyakazi amelipa kodi bila kukwepa, nah ii imeainishwa kwenye sheria hii ya kodi kuanzia sehemu ya 84 hadi 87 ambapo PAYE inamezwa na withholding tax


  Hakuna mfanyakazi anayepewa kodi na kujilipia kodi! Kodi (PAYE) ni mojawapo ya witholding tax ambayo S.84-86 ya sheria ya mapato inaelezea utaratibu wa ulipaji wake. Kodi hii inakusanywa na mwajiri kwa niaba ya TRA mwajiriwa anatakiwa kuiwasilisha tra ndani ya siku 15 baada ya mwezi husika wa kodi hyo kuisha.(kumbuka wafanyakazi wapo wa serikali na sekta binafsi na mashirika za serikali.)
  Swali linakuja kwa nini wafanyakazi hawapewi Tin kwa sababu tu wanalipa kodi?
  Jibu ni rahisi
  kuwa mfanyakazi tu sheria haikuruhusu kuwa na TIN hvyo basi huwezi kuomba tin eti kwa sababu wewe ni mfanyakazi.
  usiku mwema, maswali yatajibiwa kesho.
   
 19. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeshindwa kugonga like natumia simu ila well said...hapa shedafa asipoelewa ataku

  Atakuwa ana kichwa kigumu balaa!!!
   
Loading...