Ni nini siri ya Manispaa ya Ubungo ( Chadema) kutoathiriwa na " Hamia Hamia CCM" hadi Meya wake anastaafu kwa Heshima?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,776
Kijiografia manispaa ya ubungo inaanzia Kigogo round about hadi Kibamba kwa maana ya Kigogo, Mburahati, Mabibo, Manzese, Ubungo, Kimara,, Mbezi, Msakuzi, Kwembe hadi Kibamba.

Meya wa manispaa ya ubungo ni mh Jacob Boniface kupitia Chadema hivyo manispaa hiyo iko chini ya chama chake.

Meya Bonny ni miongoni mwa mameya wachache sana wa upinzani ambao wamepambana bila kuyumba dhidi ya chama tawala na hatimaye atastaafu kwa heshima baada ya kutangaza kutogombea tena udiwani.

Nini siri ya mafanikio ya Chadema ubungo kutoyumbishwa na " Zoa zoa ya CCM " na hatimaye wanamaliza salama majukumu waliyokabidhiwa?

Niwatakie Juma Takatifu lenye Baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwamba Boniface anunuliwe? Si walipanga kumuua wakachemsha? Saivi wamepona wahamie NCCR
 
Hata Iringa nao wametoka salama. Ni ujinga na upumbavu wa yule mkurugenzi mwendawazimu anayejua tumbo lake na la maccm ila wajuba nao walikuwa vizuri.
 
Msije mkafikiri wale walioangukiwa na mnara wa babeli wana dhambi kuliko ninyi, nawaambia tubuni maana msipotubu nanyi mtaangamia vivyo hivyo.
 
Hata Iringa nao wametoka salama. Ni ujinga na upumbavu wa yule mkurugenzi mwendawazimu anayejua tumbo lake na la maccm ila wajuba nao walikuwa vizuri.
Hahahaaaaa....... Kimbe kang'olewa kwa mabavu!

Wale wadimi na wakwamisi hawafai kabisa bwashee!
 
Back
Top Bottom