Ni nini sababu ya tofauti kubwa za mishahara ya watumishi wa serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini sababu ya tofauti kubwa za mishahara ya watumishi wa serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by shaluu, Nov 26, 2011.

 1. s

  shaluu Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umefika wakati sasa kwa wabunge kuliweka mezani swala la tofauti za mishahara ya watumishi wa serikali, hapa namaanisha mshahara wa mtumishi wa TRA, TANAPA,BOT una tofauti kubwa sana na mishahara ya watumishi wa halmashauri,walimu na idara nyingine kama kilimo na hii tofauti ni kubwa hata kama mna viwango sawa vya elimu............................mimi naamini kuwa serika li ikiweza kuweka uwiano hata malalamiko yatapungua.Kwa nini ibara ya 23 ya katika inakiukwa? ..............kila mtu anapaswa kupata ujira unaolingana na kazi anayofanya.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Labda kwa sababu sehemu ulizozitaja hapo juu wao wanahusika kwa namna moja au nyingine kukusanya mapato ya Serikali tofauti na kama walimu au watumishi wengine wa Serikali. Pia, kwa ufahamu wangu ofisi ulizozitaja ni "AUTHORITY" ambazo zina mamlaka ya kujipangia wenyewe viwango vya mishahara na posho. Wenye ufahamu zaidi wataendelea kuchambua. Watumishi wengine ni watumiaji zaidi wa makusanyo yanayofanywa na hizo mamlaka.
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh kama umesoma kichwa changu. Nimepita mikoa 2 Leo ofisi zakaria TRA nzuri kweli. Nikapitia police, shuleni na hospital ofisi ziko mbovu kweli.
  USAWA UKO WAPI?
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu hizo ni miongoni mwa dalili za tawala za kifisadi. Ufisadi ukitopea kwenye jamii ni kawaida mno kukutana na mifumo kama hiyo.

  Inapotokea serikali hiyo hiyo kuwa na tofauti kubwa ya mishahara miongoni mwa watumishi wake tena kwa vijisababu visivyo na mashiko inatia mashaka na inaudhi. Lakini, hayo mazingira yanatengenezwa makusudi ili watu fulani fulani wapate ulaji katika taasisi hizo. Fuatilia taratibu za ajira na aina ya watu walioajiriwa BoT, TRA, na "agencies" nyingine, utachoka. Lakini, hivi mpaka lini?
   
 5. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hal hii ni kweli kabisa kuna haja ya kuangalia mishahara kulingana na Elimu na utendaji kazi bila kujali unafanaya kazi mahali gani ndani ya serikali moja
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Jaman,me sioni kama tra wanalipwa pesa nyingi za kutisha,niliwah kuona salary slip ya mhasibu mmoja wa tra ambae ni graduate,ilikua inaonyesha basic salary ni laki 4.5,take home ni kama laki 3 na ushehe hvi ambayo ni sawa na watumish wengne walioko halmashauri
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,247
  Likes Received: 10,428
  Trophy Points: 280
  inachekesha kuona daktari wa halmashauri analipwa sawa na mganga wa tanapa wote hawa hawazalishi wanatumia tu.
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu kama sijakusoma vile. Au mimi ndo sijaelewa mada!
   
 9. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa nahusika kupanga viwango vya salary ingekuwa, in decending order

  1.Walimu....2.Madaktari/wauguzi....3.madereva.............na kumalizia ingekuwa wabunge........rais!

  Nina sababu za msingi kwa hii hoja yangu.
   
 10. R

  Rockabie Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KImsingi mishahara haitaweza kulingana kabisa lakini kikubwa nnachopenda kukiona ni tofauti iliyoko ipungue kwa kuzingatia kuwa mazingira wanayoishi watumishi hawa wote kwa maana ya mahitaji havitofautiani sana.kwa mfano haiingii akilini mkuu wa idara alipwe milion2 wakati subordinate wake ambaye anaweza kuwa na elimu zaidi yake na ndiye mtenda kazi mkuu analipwa laki5, wakati huo huo huyo mkuu wa idara ana vikao na safari zisizoisha zenye posho.
   
 11. D

  Deo JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  [h=2]Ni nini sababu ya tofauti kubwa za mishahara ya watumishi wa serikali?[/h]Waraka wa serekali uliowekwa wakati wa fisadi nkapa kuwa ni kosa la jinai kuujadili waraka unaohusu mishahara ya watumishi na unawekwa siri, nikosa la jinai ukiuweka hadharani.

  Ufisadi mtupu wa kimfumo wa nkapa
   
 12. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ninachofahamu ni kwamba, tanapa, tra na wengine, ni goverment parastatals, yaani ni mamlaka huru ndani ya serikali kuu. Mamlaka hzi hata dawasa, zinakusanya mapato kulingana na wigo wake, niliwah kumsikia jk alipowatembelea dawasa kuwa kama wanaweza kuwa na mapato mazuri basi wanaweza kuboresha maslahi ya wafanyakz wao. Hvy mamlaka hz zina salary scale tofauti na idara nyingine kwa sbb wanajitegemea. Huwez kusikia wanaomba ruzuku serikali kuu, huwezi kusikia wanaandika barua utumishi wakiomba kuajiri watumish nk. Mapato yao yanaruhusu
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sina cha kuchangia mkuu ila hii kwangu mimi ni one of the very usefull thread. Thank you for that. nawasihi wale wenye ufahamu mzuri wa hii ishu jinsi inavyoendeshwa watujuze.
   
 14. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TRA hawategemei mshahara, mishahara yao ya kawaida, sema sasa kuna vitengo vile ambavyo rushwa ndo inakopitia huko, huko ndo kuna neema. Mtu unshangaa ameanza kazi TRA jana, baada ya miezi 2 anaporomosha ghorofa, mfano mzuri ni watu wa mizani, acha kabisa!

  [​IMG]
  Il Gambino.
   
 15. S

  SINA Senior Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 167
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unachokisema ni kweli lakini kuna maeneo si sahihi kwa mfano muundo wa wizara ya Afya wao awaingizi pesa lakini wana mishahara mikubwa ukilinganisha na walimu au wahandisi. Kinachoangaliwa Tanzania ni nani yupo kwenye system kwa wakati huo na atawabeba watu walio kwenye fani yake hilo ndilo tatizo kubwa. Ukiangalia kama TANESCO wana mishahara mikubwa na bado wanapata ruzuku toka serikalini. Time will tell
   
Loading...