Ni nini matokeo ya sumu ya visasi vinavyotengenezwa sasa kwa mustakabali wa taifa letu hapo baadae?

Naiona sumu ya visasi ikiendele kumea na inakua kwa kasi kubwa na
Kila mtu akipata madaraka au nafasi ya kuongoza cha kwanza anawaza nianze kumkomoa nani aliye nikomesha zamani na kila aliyepata madaraka anawaza nianze kumkomesha nani aliye nikomoa zamani, laaah!

Marais hawawazi kuleta maendeleo tena bali wanawaza ni nani na nani walio kuwa hawako upande wangu kabla sijawa rais nianze nao hao kwanza maana nina mamlaka ya kufanya lolote na nina majeshi yananilinda wakati wote

Mawaziri nao hawazi kuhangaika na matatizo ya wananchi wala hawawazii kuliunganisha taifa nao wanawaza nimkomoe nani ili kupitia yeye rais anione anisifie kama mchapa kazi hodari, hahahaaaaaaaa!

Wakuu wa mikoa na wilaya nao ndio kabisaa hawawazii kabisa kuliunganishwa taifa na wananchi bali kila mmoja ana yawaza masaa yake 48 ya kumuweka ndani mtu anayatumiaje na wako bize wanapambana kutafuta nani wakumuweka ndani masaa 48 ili yatumike ,looooooooo!!

Wakurugenzi na viongozi wengine wa level hizo nao hawawazii kuliunganisha taifa bali wako bize kutafuta mikwala na vijembe vya kuwatisha watumishi walio chini yao

Vyama vya siasa kila kimoja hakiwazii kuliunganisha taifa bali kila chama kiko bize kutafuta mbinu za kukichonganisha kingine na kuwagombamisha na wengine, kila kimoja kinawaza namna gani nitakikomoa chama kingine , laaaaah!

Polisi na kundi lao nao hawawazii kabisa kuliunganisha taifa bali kila mmoja anawaza ni mbinu gani niitumie kamnasa fulani na hata asipo kuwa na hatia ni mbinu gani nitumie kumtia hatian

Najiuliza maswali haya:

1. Hali hii ina ashiria nini huko mbeleni endapo kila mtu atakuwa na kisasi kwa yale aliyo fanyiwa.

2.visasi hivi vikikomaa kabisa vikatoa na matunda kama taifa tutakiwa na aina gani ya watu

3. Hii mbegu ya visasi hii inayo endeleo kukua kwa kasi ya 4G kwa sasa ni nani atakuja kuiondoa ndani ya mioyo ya watanzania hawa

5. Nini kifanyike kuliunganisha taifa pamoja kabla halija fika kubaya zaid ambapo kwa darubini yangu naliona anguko kubwa la sifa kuu ya tanzania kuwa nchi yenye amani na upendo?

NAWASILISHA.

kunogesha post yako weka mifano hai kabisa isiyo na chenga, maana hata nia nzuri ya rais na serikali inaweza kutafsiriwa vibaya

ukishindwa evidences, omba muda wafute huu uzi, sio wa msomi ni wa muuza kahawa, hata project yako ya mwisho aidha wakati unafanya degree, diploma au hata certificate haukufanya vizuri
 
kunogesha post yako weka mifano hai kabisa isiyo na chenga, maana hata nia nzuri ya rais na serikali inaweza kutafsiriwa vibaya

ukishindwa evidences, omba muda wafute huu uzi, sio wa msomi ni wa muuza kahawa, hata project yako ya mwisho aidha wakati unafanya degree, diploma au hata certificate haukufanya vizuri
muulize manji akueleze maana ya kisasi, kama hataki kukueleza muulize kitilya aliyekataa kutoa tax exemption ya gari , au muulize maalim seif aliyekataa kutoa mkono tuu
 
Chuki imeoteshwa na vijana Wa chadema na wafuasi Wa chadema waliyojipa kupambana na Mkuu Wa nchi!!hatuwezi kukubali siasa chafu na lagai ndani ya taifa letu
 
Back
Top Bottom