Ni nini matokeo ya sumu ya visasi vinavyotengenezwa sasa kwa mustakabali wa taifa letu hapo baadae?

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Naiona sumu ya visasi ikiendele kumea na inakua kwa kasi kubwa na
Kila mtu akipata madaraka au nafasi ya kuongoza cha kwanza anawaza nianze kumkomoa nani aliye nikomesha zamani na kila aliyepata madaraka anawaza nianze kumkomesha nani aliye nikomoa zamani, laaah!

Marais hawawazi kuleta maendeleo tena bali wanawaza ni nani na nani walio kuwa hawako upande wangu kabla sijawa rais nianze nao hao kwanza maana nina mamlaka ya kufanya lolote na nina majeshi yananilinda wakati wote

Mawaziri nao hawazi kuhangaika na matatizo ya wananchi wala hawawazii kuliunganisha taifa nao wanawaza nimkomoe nani ili kupitia yeye rais anione anisifie kama mchapa kazi hodari, hahahaaaaaaaa!

Wakuu wa mikoa na wilaya nao ndio kabisaa hawawazii kabisa kuliunganishwa taifa na wananchi bali kila mmoja ana yawaza masaa yake 48 ya kumuweka ndani mtu anayatumiaje na wako bize wanapambana kutafuta nani wakumuweka ndani masaa 48 ili yatumike ,looooooooo!!

Wakurugenzi na viongozi wengine wa level hizo nao hawawazii kuliunganisha taifa bali wako bize kutafuta mikwala na vijembe vya kuwatisha watumishi walio chini yao

Vyama vya siasa kila kimoja hakiwazii kuliunganisha taifa bali kila chama kiko bize kutafuta mbinu za kukichonganisha kingine na kuwagombamisha na wengine, kila kimoja kinawaza namna gani nitakikomoa chama kingine , laaaaah!

Polisi na kundi lao nao hawawazii kabisa kuliunganisha taifa bali kila mmoja anawaza ni mbinu gani niitumie kamnasa fulani na hata asipo kuwa na hatia ni mbinu gani nitumie kumtia hatian

Najiuliza maswali haya:

1. Hali hii ina ashiria nini huko mbeleni endapo kila mtu atakuwa na kisasi kwa yale aliyo fanyiwa.

2.visasi hivi vikikomaa kabisa vikatoa na matunda kama taifa tutakiwa na aina gani ya watu

3. Hii mbegu ya visasi hii inayo endeleo kukua kwa kasi ya 4G kwa sasa ni nani atakuja kuiondoa ndani ya mioyo ya watanzania hawa

5. Nini kifanyike kuliunganisha taifa pamoja kabla halija fika kubaya zaid ambapo kwa darubini yangu naliona anguko kubwa la sifa kuu ya tanzania kuwa nchi yenye amani na upendo?

NAWASILISHA.
 
Akuanzae mmalize.

Alianzwa yeye leo anawamaliza.

Naye atamalizwa huko mbeleni.

Ni kanuni mojatu.

AKUANZAE MMALIZE!!!
 
Hi Ni Kazi Ya Pogba Ndyo Baba Mwanzilishi Wa Visasi,hatima Yake Tutakuwa Taifa La Watu Wa Visasi Namwishowe Tunakuwa Km Somalia
 
Kila mtu atakufa,ilo la muhimu sana watawala wetu walijue.Tutukane,tuvunjie nyumba zetu,tunyime uhuru wa mikutano ya kisiasa,vunja Katiba uwezavyo,zuia maandamano lakini hata wewe UTAKUFA TU.
 
Naiona sumu ya visasi ikiendele kumea na inakua kwa kasi kubwa na
Kila mtu akipata madaraka au nafasi ya kuongoza cha kwanza anawaza nianze kumkomoa nani aliye nikomesha zamani na kila aliyepata madaraka anawaza nianze kumkomesha nani aliye nikomoa zamani, laaah!

Marais hawawazi kuleta maendeleo tena bali wanawaza ni nani na nani walio kuwa hawako upande wangu kabla sijawa rais nianze nao hao kwanza maana nina mamlaka ya kufanya lolote na nina majeshi yananilinda wakati wote

Mawaziri nao hawazi kuhangaika na matatizo ya wananchi wala hawawazii kuliunganisha taifa nao wanawaza nimkomoe nani ili kupitia yeye rais anione anisifie kama mchapa kazi hodari, hahahaaaaaaaa!

Wakuu wa mikoa na wilaya nao ndio kabisaa hawawazii kabisa kuliunganishwa taifa na wananchi bali kila mmoja ana yawaza masaa yake 48 ya kumuweka ndani mtu anayatumiaje na wako bize wanapambana kutafuta nani wakumuweka ndani masaa 48 ili yatumike ,looooooooo!!

Wakurugenzi na viongozi wengine wa level hizo nao hawawazii kuliunganisha taifa bali wako bize kutafuta mikwala na vijembe vya kuwatisha watumishi walio chini yao

Vyama vya siasa kila kimoja hakiwazii kuliunganisha taifa bali kila chama kiko bize kutafuta mbinu za kukichonganisha kingine na kuwagombamisha na wengine, kila kimoja kinawaza namna gani nitakikomoa chama kingine , laaaaah!

Polisi na kundi lao nao hawawazii kabisa kuliunganisha taifa bali kila mmoja anawaza ni mbinu gani niitumie kamnasa fulani na hata asipo kuwa na hatia ni mbinu gani nitumie kumtia hatian

Najiuliza maswali haya:

1. Hali hii ina ashiria nini huko mbeleni endapo kila mtu atakuwa na kisasi kwa yale aliyo fanyiwa.

2.visasi hivi vikikomaa kabisa vikatoa na matunda kama taifa tutakiwa na aina gani ya watu

3. Hii mbegu ya visasi hii inayo endeleo kukua kwa kasi ya 4G kwa sasa ni nani atakuja kuiondoa ndani ya mioyo ya watanzania hawa

5. Nini kifanyike kuliunganisha taifa pamoja kabla halija fika kubaya zaid ambapo kwa darubini yangu naliona anguko kubwa la sifa kuu ya tanzania kuwa nchi yenye amani na upendo?

NAWASILISHA.

Ni Mheshimiwa kusema ameshindwa kuongoza TAIFA awaachie wenye uwezo.Imetosha kutugawa
 
Hakuna kitu kibaya Duniani hapa kama chuki,visasi haya yalikuwa Rwanda mwisho wa siku mliyaona,zile zilikuwa ni hasira na kibaya zaidi watawala wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kustaafu,anaweza akaja mtawala mwingine awe wa upinzani au hicho hicho chama tawala akaja na sera zake sijui watafanyaje,hii nchi mwalimu nyerere alituunganisha watanzania tukawa wamoja,tukapendana,mchaga anaweza kununua shamba kigoma akaishi bila tatizo,au mmasai akaoa mbondei na wakaishi kama ndugu,watoto wetu kutoka Tanga anakwenda kusoma huko mara na wanajichanganya bila tatizo ila sasa hivi awamu hii ya tano ishaanza kuipasua nchi,tena kwa kasi kubwa hii watanzania tusiikubali kabisa tukiruhusu haya yatakayotokea hapa naapa tutatafutana hapa,wataanza kutafuta suluhisho hapa,yote haya ni ya nini? Wanaofanya hivi waache huu mchezo hatari haraka sana tena waende kanisani,na misikitini wakatubu dhambi hii wanayoifanya itakuja kuwatafuna
 
Akuanzae mmalize.

Alianzwa yeye leo anawamaliza.

Naye atamalizwa huko mbeleni.

Ni kanuni mojatu.

AKUANZAE MMALIZE!!!

Miaka 20 na ushee tuko kwenye tawala za visasi,chuki na ubaguzi sijui tutakuwa wageni wa nani.Kibaya hata wale tuliodhani wataona hawaoni wanajali matumbo yao tu.Ona Viongozi wa Dini,Bunge,Polisi,Mahakama,Jeshi letu wote wanajali matumbo hawaijali kesho ya Taifa
 
Hakuna kitu kibaya Duniani hapa kama chuki,visasi haya yalikuwa Rwanda mwisho wa siku mliyaona,zile zilikuwa ni hasira na kibaya zaidi watawala wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kustaafu,anaweza akaja mtawala mwingine awe wa upinzani au hicho hicho chama tawala akaja na sera zake sijui watafanyaje,hii nchi mwalimu nyerere alituunganisha watanzania tukawa wamoja,tukapendana,mchaga anaweza kununua shamba kigoma akaishi bila tatizo,au mmasai akaoa mbondei na wakaishi kama ndugu,watoto wetu kutoka Tanga anakwenda kusoma huko mara na wanajichanganya bila tatizo ila sasa hivi awamu hii ya tano ishaanza kuipasua nchi,tena kwa kasi kubwa hii watanzania tusiikubali kabisa tukiruhusu haya yatakayotokea hapa naapa tutatafutana hapa,wataanza kutafuta suluhisho hapa,yote haya ni ya nini? Wanaofanya hivi waache huu mchezo hatari haraka sana tena waende kanisani,na misikitini wakatubu dhambi hii wanayoifanya itakuja kuwatafuna

Kama kiongozi Mkuu wa Taifa anasimama na kusema wanaopaswa kufanya biashara hapa ni wazawa wa eneo hili tu sasa sijui wengine wakakae wapi ni aibu kubwa kuwa na Kiongozi wa hulka ya JPM
 
Mtahangaika sana na akili zenu ndogo hizo

Hahahahahahhahah mwenye akili ndogo unamjua lakini??Ni yule anayepiga makofi hata kwenye upumbavu wakati anaujua ni upumbavu bado kwa sababu ya upumbavu anapigia makofi huo huo upumbavu.

Pole sana nenda kasome Uhuru na Maendeleo by JKN ili akili yako ikurudie
 
Mimi nachukia kuwa taifa lenye amani! Hivi faida yake ni nini? Tukikosa amani kidogo tutaheshimiana na kusikilizana vizuri. Rejea yaliyotokea Zanzibar mpaka kukawepo serikali ya umoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja ya msingi wala sio kuhangaika ,kwa mwenye akili anajua hoja ya msingi hapa nini muafaka wa visasi hivi na si vinginevyo.
 
Nimekua nikiangalia kule North Korea, ambapo Kim Jon Un alishinda uchaguzi kwa 100%,

Nikaangalia pale Rwanda ambapo Kagame alishinda kwa asilimia 98% nikaangalia
Maeneo mengi Zimbabwe, nk sehemu mbalimbali Madikteta hua hawapotezi kwenye uchaguzi. Na ushindi wao Mara nyingi unakua hauna mashaka mashaka.

Kimsingi kama wote tunakubaliana kua Mkuu ni Dikteta basi tujue kua atashinda kwa ushindi Mkubwa sana hapo 2020.

Hii inatokana na watu kumuogopa, na hofu ya kuitwa wasaliti, hivyo hata wasiokupenda wanalazimika kujikomba ili waaminike.

Hapa nchini vyombo vya kiulinzi vimeonekana kuwashughulikia wapinzani kwa gharama kubwa. Lengo ni kufunika ndoto ya Nguvu ya upinzani kujipanga na kushinda uraisi mwaka 2020.

Vyombo vya dini na vinginevyo vimeonekana kutokujaribu kukemea au kulaani chochote kinachoendelea ni kwasababu ya hofu.

Mimi ni mmoja wapo nilietamani Tanzania ipate Dikteta.

Japo sikua natarajia kwa namna niionavyo.

Ninachoamini, utawala huu utapiga hatua kadhaa za kimaendeleo (mbali.na demokrasia) kwasababu tu Unaogopwa.

Ninayonheshima kubwa kwa wapinzani lakini mpaka sasa Chadema kipo peke yake kikichuana na CCM.

"Siiyuueffu" tayari wameshaonesha muelekeo kua watakua wapinzani WA cdm chini ya profesa Lipumba.

CCM ni kama kunguru atakae kua akidonoa sisimizi WA pande hizi mbili.

Na Lipumba kwakua ana baraka zote za CCM na dola yake, hatahangaika sana na Serikali hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom