Ni nini maana ya mishumaa na keki katika Birthday? Nani alianzisha?

Multdealer

JF-Expert Member
Oct 11, 2019
226
232
Utaratibu wa kuwasha na kuzima mishumaa pamoja na ukataji wa keki umekuwa ni wakawaida kwa muda sasa. Ningelipenda kuuliza kwa watakao kuwa wana ufahamu juu ya hili suala.

Nini maana yake?
Na nani ni muhasisi?

Mpaka tarehe 1/7/2020 covid_19 itakuwa ishapotea
 
Inaashiria uzima na kifo..kwamba unapowaka ni uzima na nuru kwako na unapozimwa ni ishara kwamba utakufa na nuru itapotea kwenye maisha yako. Hii tafsiri ni yangu tu.
 
HISTORIA inasema!
Watu wa zamani walitumia na kuamini kabla ya kupuliza mishumaa ya keki,
Una wish jambo, yaani maombi fulani ungependa yatokee...
Sasa ukishatamka upuliza...
Ule moshi unapaa hadi kwa mungu wao....
I'm done

TAFUTA MTU YOYOTE UMLAUMU...!
 
Wagiriki wa zaman walitumia round cake kuwakilisha mwezi na na wakaweka juu yake mishumaa wakiamini moshi utachukua maombi yao hadi kwa miungu yao
 
HISTORIA inasema!
Watu wa zamani walitumia na kuamini kabla ya kupuliza mishumaa ya keki,
Una wish jambo, yaani maombi fulani ungependa yatokee...
Sasa ukishatamka upuliza...
Ule moshi unapaa hadi kwa mungu wao....
I'm done

TAFUTA MTU YOYOTE UMLAUMU...!
Okeee sawa sawa,kumbe ki-imani ni suala lenye maana, japo sidhani Kama wengi huwa wananuia, wengi hufanya kwa mazoea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom