Habari JF
Kumekuwa na Tabia ya kususia Chaguzi kwa baadhi ya Vyama hususani CHADEMA, kwa namna navyoelewa kususa haijawahi kuwa suluhu ya tatizo labda kipindi cha utoto tu napo wazazi walikuwa wanaweza kukupotezea tu.
Hivyo nikawaza kwa kina sana nikapata tafsiri zifuatazo zinaweza kuwa sahihi kuhusu hii susa susa.
1. Ni njia mojawapo ya kufitini baadhi ya viongozi wasiingie kwenye vinyang'anyiro na kuwa viongozi.
2. Wanahofia hakuna tume huru hivyo hakuna haja ya kushiriki uchaguzi huku washindi wanajulikana.
3. Viongozi wa vyama wananunuliwa ili uchaguzi uwe rahisi kama inavyofanywa na baadhi ya viongozi kujitoa.
4. Wanajua hawatashinda hivyo wanaona hakuna haja kushiriki.
Hivi nini maana ya hizi susia huku hatuoni suluhisho lolote linatafutwa? Na je, kuna mwanachama anayehitaji kugombea uongozi atabaki CHADEMA huku hajui kama watashiriki uchaguzi au la?