Ni nini lengo la Sheria ya kuzuia siasa nje ya Jimbo?

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,041
1,160
SHERIA YA KUZUIA SIASA NJE YA JIMBO NI KUJENGA UKANDA, UKABILA NA UBAGUZI KWA TAIFA.

Naona kuna sheria inatungwa, bahati mbaya au nzuri,au mbaya zaidi,inatungwa kipindi ambacho wizara ya sheria inaongozwa na maprofesa wawili,mmoja waziri,mwingine katibu mkuu,wote matunda ya University of Dar es salaam.

Sheria hii ina lengo la kuzuia siasa nje ya jimbo ambalo muhusika ni mbunge, kwa maana hiyo,muhusika atafanya siasa ndani ya eneo lake.

Kama sheria hii itapita, zile ndoto za Mzee Nyerere kufuta ukabila na ubaguzi wa kimaeneo hazitatimia,sasa sheria ndio itakuwa inatuelekeza jinsi ya kubaguana na maafisa wa serikali,hasa polisi ndio watakuwa wanahakikisha mtanzania wa eneo Fulani akomee hukohuko na hana ruksa ya kuongea na kujadili maendeleo ya Tanzania na wenzie wa maeneo mengine.

Mgogo wa Dodoma aliyepata ubunge hataruhusu mkurya wa Tarime aungane naye kuhubiri uzalendo na umoja wa kitaifa dodoma, dodoma wagogo tu ndio watakuwa wanahutubia wagogo wenzao,na ili kukoleza,wanaweza hata kuhutubiana kwa kabila la kigogo kwa kuwa watu wa iringa wahehe, kisheria wamezuiwa kushirikiana na watanzania wenzao wa dodoma katika mambo ya kisiasa.

Pia wakerewe nao watahutubiana ukerewe huko huko na wakerewe wenzao,wakerewe wakimuona mchaga kaja kuwasimulia uzuri wa Tanzania, basi polisi watamzuia na watamwambia hili sio jimbo lako ondoka,huku wanaongea wakerewe kwa wakerewe.

Tulianza na shule za kata, wanafunzi hawavuki kata, sasa wabunge (na pengine hata madiwani) watabaki kuwa wa maeneo yao.

Mzee Nyerere alikuwa na mfumo wa kumtoa mwanafunzi chato na kumpeleka iringa akasome,lengo ni kumfanya achangamane na asahau siasa za parokia, ajihisi mtanzania na sio mtu wa Njombe,mwanza,sumbawanga,hao,marangu.

Lakini tunakoelekea sasa kabla ya kufanya mkutano wa hadhara,ukitoa taarifa polisi,unaulizwa,
"Wewe ni wa wapi "
Huulizwi kama wewe ni mtanzania,ukijibu wewe ni mfipa wa Katavi unafukuzwa,unaambiwa hapa inaruhusiwa mikutano ya wamasai,mbunge wa hapa ni mmasai,ondoka,hapa tayari tunabaguana kwa mujibu wa sheria,watawala wanajenga mifumo ya kuhakikisha tunabaguana kijimbo,kikata(kwa madiwani),kimkoa,kiwilaya,wa huku havuki kwenda kule.

Wakiwa bungeni wabunge wanachangia bajeti ya taifa ambayo hawazuiwi kuchangia kuhusu sehemu yeyote ya Tanzania,wanachangia kuboresha bajeti ya Tanzania bungeni na wana haki ya kuhoji utekelezaji wa bajeti hiyo sehemu yeyote ya Tanzania,hii inamfanya ajione yeye ni mbunge wa BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,si mbunge wa jimbo tena,anawajibika kwa nchi nzima.

Pia mbunge ana haki mbili,ya kiubunge kwa maana kwa nchi na wapiga kura na pia ana haki ya kiraia,chama cha siasa kimempa uanachama,sheria inazuia chama kisifanye kazi sehemu moja tu ya jamhuri,pia chama lazima kipate wanachama kwa mikoa zaidi ya kumi,

Mbunge anapotembea anatembea na haki hizi mbili,ya kueneza chama,na pia anatembea na hadhi ya ubunge,chama kilichompa ubunge kimesajiriwa nchi nzima,ana jukumu la kukieneza nchi nzima kwa kofia ya uanachama na pia ya ubunge.

Nawasihi maprofesa wasiingie katika mtego wa kuharibu CV zao kwa kujenga ubaguzi.

Tunataka wachaga wahutubiwe na wakinga,wakinga wahutubiwe na wasukuma, n.k.
 
Very poor thinking logic. Nani kakuambia wabunge wa majimbo wanachaguliwa kwa sababu za ukabila? Halima Mdee ni mzaramo? Lema ni Mmeru? Wenja alipokuwa mbunge wa Mwanza alikuwa ni msukuma? Kiseri ni mkurya lakini ni mbunge wa Manyara na kadhalika.

Mbunge wa jimbo anachaguliwa na wakazi wa jimbo kati ya watu wanaowaona wanaweza kuwawakilishia matatizo yao bungeni bila kujali ni wa kabila gani. Watanzania hawana ukabila na kila jimbo lina makabila mbali mbali. Wanachagua yule anayekidhi vigezo vyao na si vingine.
 
Back
Top Bottom