Ni nini kingetokea kama JK angekataa Matokeo ya Kushinda kura za Urais?

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Mambo mengine tunatakiwa tuyafirikie kidogo hata kama kikatiba yamekaa tu bila kuwa na mantiki yoyote lakini tunayafuata tu kishabiki.

Mtakubaliana nami kuwa kama ukweli unatafutwa na kufuatwa, mambo hayawezi kwenda kama tunavyoona leo. Fikiria, Jk alichukua fomu ya kugombea urais, kura zikapigwa na kuhesabiwa na hatimaye tume ikamtangaza bila hata mgombea kusaini matokeo( kwa sababu tume haijali kama mgombea kasaini). Hivi ingekuwaje kama baada ya kutangazwa matokeo yule JK angetamka kwamba hatambui matokeo hayo kwa sababu anaamini kuwa yeye hakushinda. Je, hapo inakuwaje?


Kabla ya uchaguzi kila kona ya nchi rushwa ilipigiwa kelele hasa maeneo ya Arusha, lakini TAKUKURU wala hawaonekani. Zile mbwembwe zao wakati wa kura za maoni za CCM hazikuwepo tena. Sheria ya gharama za uchaguzi ikawekwa kapuni. CCM waligawa fedha kama nini achilia mbali vitu vidogo vidogo kama T-shirt, kanga na kofia.

Kabla ya tarehe ya uchaguzi yaani 31/10/2010 kulikuwa na madai juu ya daftari la uchaguzi kuwa wazi ili kasoro ziweze kurekebishwe lakini Tume ikakataa. Siku ya siku majina ya baadhi ya wapiga kura hayakuonekana na hakuna aliyeweza kuwasaidia. Sambamba na hilo suala lingine likawa kwamba wapiga kura ni wangapi? Tukaambiwa mara milioni 19 mara milioni 20. Siku ya siku waliopiga kura wakawa miloni nane (8). Je ina maana kweli waliopiga kura ni wachache hivyo?

Tarehe 31/10/2010 tulifanya uchaguzi lakini kabla ya uchaguzi tukasikia mambo mengi yakiwemo ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kuwa wahakikishe CCM inashinda. Kwa upande wa kura za madiwani na wabunge mambo yakaenda kama tulivyoona. Kwa wabunge ilibidi watu waende katika maeneo ambayo kura zinatangazwa. Katika baadhi ya maeneo matokeo yalitangazwa kwa sababu ya shinikizo la wapiga kura. Wakati huo huo hakuna aliyehangaika na kura za urais. Kura za urais zikawa zinatangazwa na Tume ya uchaguzi kama vile matokeo walikuwa nayo huko huko. Kilichotokea ni kuwa kura za urais katika Jimbo la Geita yakalandana na ya jimbo lingine na hatimaye Tume ikakiri kosa hilo na kulirekebisha. Je matokeo kama hayo yalitokana na kura za wananchi kweli.

Siku ya siku mshindi akatangazwa huku kila mtu akishangaa kwamba imekuwaje mbona kura sikumpa. Huyo si mwingine bali Jk. Mgombea urais kwa tiketi ya CCM ameshinda kwa kura....ambazo ni sawa na asilimia..... sidhani kama JK alihangaika kujua kuwa toka kila Jimbo la uchaguzi alipata kura ngapi. Sidhani kama aliziona fomu za matokeo zilizotoka katika majimbo. Kwake yeye alichojua ni kuwa hata kama wananchi wasingemchagua yeye angetangazwa tu na Tume ya uchaguzi na matokeo hayo hayatahojiwa mahali popote.

Msingi wa hoja yangu ni kuwa, kwa vile katiba ya Tanzania inasema kuwa matokeo ya kura za mgombea urais yatakapokuwa yametangazwa na Tume hayawezi kuhojiwa kwenye chombo chochote, hii kasoro hatuioni kabisa au ni nini? Kwa katiba ya aina hii hatuoni umbumbubu katika katiba?kifungu cha namna hii katika Katiba kina lengo gani? Kukiwa na kifungu cha namna hii katika katiba haina maana kuwa haki ya wananchi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka imeporwa kabla hata hawajakwenda kwenye sanduku la kura? Hivi tukifanya uchaguzi na wapiga tukawa na uhakika tumempigia kura ni mtu fulani lakini baadaye msimamizi anamtangaza mshindi tofauti na tuliyemchagua na mwisho wa yote hatuna mahali pa kuhoji, je sisi kama wapiga kura tufanya uchaguzi au tunaigiza?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom