Mapank
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 4,074
- 5,911
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza "Ni nini kinafanya Kenya kukusanya mapato zaidi ya Tanzania?" Kwa muda nimekuwa mfuatiliaji wa Budget wa nchi za Jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI. Katika ufuatiliaji huo nimekutana na maswali ambayo nimekuwa siyapatii majibu. Kwa kutumia nchi mbili KENYA na TANZANIA.
Nchi hizi mbili zimekuwa washindani wakubwa kiuchumi katika ukanda wa AFRIKA MASHARIKI. Maajabu ni wenzetu KENYA hawajabahatika kuwa na rasimali nyingi kama wenzao TANZANIA. Ila kupitia mamlaka yao ya mapato KRA wamekuwa wakikusanya mapato mengi kuliko majirani zao TANZANIA kupitia mamlaka yao ya mapato TRA. Mfano ni mwezi wa December 2020 TRA walijipongeza kwa kukusanya TZS 2.088 trilioni na wenzao KRA walikusanya TZS 3.4 trilioni katika kipindi cha mwezi Desemba, 2020.
Kwa upande wa idadi ya watu TANZANIA inakadiriwa kuwa na watu million 60 wakati KENYA wanakadiriwa kufikia million 53. Ni nini kinasababisha huo utofauti wa mapato?