Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,221
- 26,031
Amani iwe nanyi wadau!!
Leo naomba niulize hili swali kwenu wanajamvi maana kwa kweli mie nimetafakari hadi nimeshindwa kupata majibu.
kuna shida gani kwa Chama cha Mapinduzi juu ya Mipango miji??? Ukitembea Tanzania nzima, karibu asilimia 85 ya makazi ya watanzania ni makazi holela. Tatizo ni nini? Kama Tatizo ni kukosekana kwa pesa au wataalamu wa kupima ardhi na Makazi ndo tuseme,
1. Je CCM wameshindwa kabisa hata kusema hakuna ruhusa ya mtu kujenga mahali huku akizuia njia au barabara na kuziamulu serikali za mitaa kumvunjia mtu yeyote aliyejenga mahali kwa kuziba njia na barabara?
2. Je serikali ya CCM wameshindwa kabisa hata kuziamuru serikali za mitaa na vijiji kusimamia suala la watu wanaouza ardhi zao kuhakikisha kuwa wanapopima viwanja au mashamba wahakikishe wanaweka barabara zenye ukubwa wa kutosha kuwezesha hata gari mbili kubwa kupishana kwa kuzingatia endapo majanga yatatokea?
3. Je serikali kupitia wizara ya ardhi na Makazi wameshindwa kutoa hata mwongozo juu ya jinsi gani ujenzi wa mitaani uwe?? Na kusambaza mwongozo huo kwa serikali za mitaa kwa usimamizi?
Hii nchi kusema kweli imefika hatua inasikitisha. Ukimsikiliza waziri wa Ardhi ni kama ameshushwa leo Tanzania na hajui kuwa hili ndo Tatizo kuu linaloikabili Tanzania ya leo.
Ukitembea mitaani kuanzia Dar, Mwanza, Mbeya , Arusha , Iringa , Pwani, Zanzibar , Tabora, Kigoma na maeneo mengi ya Tanzania unaweza kusema nchi hii nzima haina watu wenye akili au hata waliotembea na kufika duniani huko kuona kukoje? Watu wamejijengea hovyo tu na wanazidi kujijengea hovyo tu. Unapita Ada estate kumepimwa ila mtaa wa nyuma kinondoni shamba kuna sehemu hata pikipiki haipiti kwa kujengwa vibaya.
Mbaya zaidi kwenye hili imefika hatua mpaka kinatokea kizazi cha watu ambao wao wanaona ufahali kujisifu kuishi maeneo ya hovyo( wanaita uswahilini au uswazi).
Hivi leo niwaulize CCM na makada wao mliopo humu kina GUSSIE Crimea YEHODAYA Barbarosa , HAMY-D Ritz chagu wa malunde Bia yetu Mudawote Kitila Mkumbo Mwigulu Nchemba Team JPM johnthebaptist Tatizo ni nini??? Imekuwaje kwa miaka yote hii mmekuwa madarakani na mmeshindwa kufanya jambo dogo tu kama hili?