Ni nini kilifanya tuite hivi?

mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,921
3,549
Habari wanaJF,

Ningependa kufahamu ni vigezo gani vilitumika kuziita baadhi ya nchi majina ambayo hayafanani na asili yake?

Mfano-
England-Uingereza
Portugal-Ureno
Netherland-Uholanzi

Tofauti na nchi nyingine kama vile
German-Ujerumani
America-Marekani
China-China
Japan-Japan
Brazil-Brazil
Etc....

Karibu tujuzane.
 
Kuhusiana na ureno nilipata kusikia zamani wale wapelelezi walikuja Africa kina Vasco da Gama na wengine walikuwa wakijitambulisha kwa kireno kuwa wametoka katika Ufalme wa Ureno kwa kusema.."Reino de Portugal" Sasa waswahili wakashika hilo neno la kwanza Reino..basi ndo ikawa chanzo cha jina Ureno..
 
Asili ya jina la Kiswahili ni neno "إنجليزي injilisi (matamshi ya Kimisri: ingilisi)" katika lugha ya Kiarabu na kwa namna ya Kibantu sauti ya "l" ikawa "r"; Waarabu walipokea jina kutoka kwa Kihispania "Ingles" ambalo ni neno lao kwa Mwingereza.
 
Kuhusiana na ureno nilipata kusikia zamani wale wapelelezi walikuja Africa kina Vasco da Gama na wengine walikuwa wakijitambulisha kwa kireno kuwa wametoka katika Ufalme wa Ureno kwa kusema.."Reino de Portugal" Sasa waswahili wakashika hilo neno la kwanza Reino..basi ndo ikawa chanzo cha jina Ureno..
Shukrani mkuu,
Vipi kuhusu Netherland mkuu?
 
Vipi kuhusu Netherland mkuu?
Netherlands ni matamshi tu na mabadiliko ya neno baada ya kukopwa kutoka lugha fulani na kuacha athari za kimatamshi na maandishi.

Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la Netherlands . Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini".
 
S

Shukrani mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom