Ni nini hatma ya uswahiba wa JK na Rostam Aziz...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini hatma ya uswahiba wa JK na Rostam Aziz...?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PhD, Aug 20, 2010.

 1. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kama inavyofahamika kwa wengi, Ndugu Hussein Bashe ni kijana wa karibu sana na Rostam Aziz yeye ndio msimamizi wa miradi mikubwa pale Caspian na kwingineko kwa niaba ya RA, izingatiwe pia RA ndiye aliyefadhili kampeni za Bashe Nzega kwa muda mrefu.

  nachojaribu kuhoji ni hatua gani Rostam ataanza kuchukua dhidi ya JK baada ya kijana wake kuondolewa kwenye uchaguzi kwa kashfa za kutokuwa raia, lakini pia suala la uraia limewahi kujitokeza kwa Rostam mwenyewe je kwa sasa hawezi kuanza kujikinga kwa namna yoyote ile ili na yeye asije ambiwa sio raia.

  na je kama Rostam akianza kujikinga na kuchukua tahadhari ikizingatiwa kuwa maamuzi ya kamati kuu juu ya Bashe hayakumpendeza kabisa, huu utakuwa ndo mwisho wa uswahiba na JK, Je rostam akikosana na JK Nchi itakuwa salama?, TAFAKARI
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hakuna Tafakuri hapa, RA itabidi anyamaze kwani Bashe alitofautiana na RIZ mtoto wa mwenye kaya
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine nadhani tunajaribu kufanya vichuguu kuwa milima Kilimanjaro. Rostam ni nani hasa hata aweze kufanya nchi ishindwe kuwa salama kwa yeye kukosana na Kikwete? Kinachotokea na kilichotokea ni "DHAMBI" ya dhuluma Rostam na genge lake waliyowatenda kwa wananchi wenye dhiki na wasio na hatia, imeanza kuwatafuna, itaendelea kuwatafuna na wataendelea kutafunana wenyewe kwa wenyewe na wananchi wataendelea kubaki salama wasalimini!
   
 4. f

  fungamesa Senior Member

  #4
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yetu macho
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hatima ya uswahiba huu ni kuipeleka nchi hii pabaya. Hadi sasa hii triumvirate -- JK-RA-EL inaiweke mustakabali wa nchi hii katika hali ya wasiwasi mkubwa na Watz wenye akili timamu wanaona kwamba matatizo mengi ya kisiasa ya sasa hivi yanatokana na uswahiba wa utatu huu -- kwani matatizo hayo yanachangiowa na ufisadi ambao unaelekezwa katika uswahiba huu. Utatu huu umekuwa unahbusishwa na kashfa kubwa kubwa za ufisadi -- kuanzia tamko la Mwembe Yanga -- EPA, Richmond na mengineyo -- either kwa ujumla wao au kwa mmoja mmoja.

  Lakini hakuna kitu kinachoonyesha kuhusika kwa kikundi hiki na ufisadi kuliko mapungufu makubwa ya namna JK (kama kiongozi wa muhimili wa utawala) alivyoshughulikia kashfa mbili kubwa za ufisadi: Richmond -- kukwepa kutimiza kutimiza mapendekezo ya Kamati ya Bunge, na Kagoda -- kushindwa kumfikisha mhusika mahakamani kama vile wengine -- kwa sababu tu mhusika wa Kagoda ni RA.
   
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ndugu BORA MAISHA hapo kwenye Bold ni vema nikaeleweka sahihi, uliza yeyote yule anayeingia kwenye vikao vya juu vya CCM na Baraza la Mawaziri ndio utaelewa nguvu ya Rostam katika utawala wa Nchi hii, kwa taarifa yako hata viongozi wa usalama wa taifa wanamuogopa bingwa huyo wa kimafia, na kama haitoshi angalia anavyonyenyekewa na wazee wa CCM kama Msekwa na Kingunge, hitimisho RA ni hatari kwa usalama wa Taifa letu ana siri kubwa ya kuingia madarakani JK hivyo akicharuka nahisi Nchi itapata mshtuko.
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  wale wale tu. Huo urafiki hautaisha ndugu yangu. wanabebana wote. RA halipi kodi. na JK anapewa pesa za Campaign na RA.
   
Loading...