Ni nini hatma ya Pesa zetu zilizotafunwa na zinazotafunwa na Hawa wabunge 19? Watanzania tumefanywa wajinga kiasi hiki?

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Nimewaza sana hivi sisi watanzania ni wajinga kiasi hiki ,Tunakatwa kodi na Tozo ,tunaishi maisha magumu ili kulisha Wanasiasa ?

Ni takribani miaka 2 sasa tangu wabunge wa CHADEMA wanao daiwa kuingia bungeni kinyume na utaaratibu kuwepo bungeni .

Pesa zetu zinapigwa CHADEMA wamechukua zaidi ya miezi 18 kusikiliza rufaa ya Wabunge hao 19 bila sababu yoyote

Serikali kupitia Bunge iko kimya na kuendelea kulipa hayo mamilioni yanayodaiwa kulipwa kwa Hao wabunge kinyume cha sheria na utaratibu.

Ukiangalia kwa Umakini si CHADEMA wala Serikali yenye Uchungu na Hizi Pesa za Wananchi .

Hivi ni nani wa Kutusaidia sisi Wananchi pesa zetu zisiliwe kijinga hivi ? Maana ukiangalia ni kama maigizo tu ili ifike 2025 .
 
Sentensi ya kwanza imeniumiza sana, why watz tunafanywa mazuzu na watu wachache kuchezea jasho letu?

Wale jamaa wa majani ya maboga wamejisahau sana, wanadhani hii nchi ya bibi yao wanafanya wanavyojisikia, na hawajali wavuja jasho wanaowezesha wao na mavitambi yao watembelee zile v8.

Ipo siku watajuta, lakini itakuwa too late..
 
Usiilaumu CHADEMA.... Imefanya kinachostahili kufanyika na haina mawaa tena kwenye hilo na IMESHAMALIZANA NAO
Cha muhimu jiandae tu kisaikolojia kwakuwa hao watakuwa wabunge wa mbeleko mpaka 2025 kama mahakama nayo itatumika kisiasa
 
Kuna ukweli ila nia thabiti inatia shaka
 
Siku wakitimuliwa bungeni waje kushtakiwa kwa uhujumu uchumi ili iwe fundisho kwa uhuni kama huu kutokea mbeleni.
 
Tatizo siyo hela Kuliwa, akiondoka mdee na wenzake, anaingia Mukya na wenzake na hela itaendelea kuliwa tuu. Huwezi kuzuia hela kuliwa kinachogombewa ni nani wa kula hiyo pesa.
Kwa faida Gani? Ndio ujiulize Kwanzaa
 
Tukiambiwa katiba mpya tunasema katiba itamnufaisha Mbowe, acha pesa zipigwe kiholela
Kwani hii katiba tuliyonayo ndo inaruhusu hawa wabunge waendelee kuwepo bungeni??? Ishu nadhani ni kueshimu utawala wa kisheria ... hiyo katiba mpya ata ikipatikana kama haieshimiwi na wanaoivunja hawachukiliwi hatua apo amna faida yoyote ndugu yangu
 
Sentensi ya kwanza imeniumiza sana, why watz tunafanywa mazuzu na watu wachache kuchezea jasho letu?

Wale jamaa wa majani ya maboga wamejisahau sana, wanadhani hii nchi ya bibi yao wanafanya wanavyojisikia, na hawajali wavuja jasho wanaowezesha wao na mavitambi yao watembelee zile v8.

Ipo siku watajuta, lakini itakuwa too late..
Inaumiza sana
 
Kwani hii katiba tuliyonayo ndo inaruhusu hawa wabunge waendelee kuwepo bungeni??? Ishu nadhani ni kueshimu utawala wa kisheria ... hiyo katiba mpya ata ikipatikana kama haieshimiwi na wanaoivunja hawachukiliwi hatua apo amna faida yoyote ndugu yangu
Itapunguza mambo mengi sn
 
Nimewaza sana hivi sisi watanzania ni wajinga kiasi hiki ,Tunakatwa kodi na Tozo ,tunaishi maisha magumu ili kulisha Wanasiasa ?

Ni takribani miaka 2 sasa tangu wabunge wa CHADEMA wanao daiwa kuingia bungeni kinyume na utaaratibu kuwepo bungeni .

Pesa zetu zinapigwa CHADEMA wamechukua zaidi ya miezi 18 kusikiliza rufaa ya Wabunge hao 19 bila sababu yoyote

Serikali kupitia Bunge iko kimya na kuendelea kulipa hayo mamilioni yanayodaiwa kulipwa kwa Hao wabunge kinyume cha sheria na utaratibu.

Ukiangalia kwa Umakini si CHADEMA wala Serikali yenye Uchungu na Hizi Pesa za Wananchi .

Hivi ni nani wa Kutusaidia sisi Wananchi pesa zetu zisiliwe kijinga hivi ? Maana ukiangalia ni kama maigizo tu ili ifike 2025 .
Yaani ss tunakatwa tozo na kodi kwa ajili ya kulipa watu wasiositahili civid 19 hv ccm wanatuchukuliaje? Ccm janga la kitaifa tunataka katiba mpya
 
Kwani hii katiba tuliyonayo ndo inaruhusu hawa wabunge waendelee kuwepo bungeni??? Ishu nadhani ni kueshimu utawala wa kisheria ... hiyo katiba mpya ata ikipatikana kama haieshimiwi na wanaoivunja hawachukiliwi hatua apo amna faida yoyote ndugu yangu
Katiba mpya nzuri itasaidia.
Katiba tuliyonayo sasa hivi inafanya mifumo yote ya utawala na mahakama isiwe huru, mifumo yote inategemea maelekezo kwa aliyewateua, na wateuliwa wanawekwa kulinda maslahi ya chama tawala.
Bila katiba mpya ccm itawachezea wananchi vyovyote inavyo taka.
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Katiba mpya hapa naona bado haitakuwa na msaada sana
Ndugu yangu, tatizo katiba ya sasa ya Tz ina 'loopholes' nyingi ambazo kiasi kwamba haziwezi kumwajibisha mtu yeyote hata kama anafanya 'madudu' au kwenda kinyume na katiba na vipengele vingi ambavyo bado vinaruhusu watu kutowajibika kwa wananchi,maana wanajua hakuna kitu mnaweza kufanya...... kaazi kwelikweli......bitter truth'
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Back
Top Bottom