Ni nini hatma ya January na Nape katika siasa za Tanzania?

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
337
1,000
Kama ndoto eti kwa mara nyingine miamba iliyokuwa ikichipuka kwa kasi kuelekea kwenye kilele cha kufanikiwa kisiasa ipo nje tena kwenye mfumo.Si Wajumbe wa baraza la mawaziri tena.Wametoswa.

Sote tunatambua sababu hasa kilicho wafanya wawe nje ya mfumo.

Kama hali hiyo itaendelea hivyo kwa wao kuendelea kuwa mbali na mfumo ilhali ndoto zao na matamanio yao hayakuwa hayo je ni nini hatma ya wanaume hao waliopata ajali ya kisiasa ya kujitakia?!

Ni kweli Magufuli aliwasamehe kwa dhati?!

Na kama aliwasamehe kwa dhati kwa nini japo mmojawao hakumteua kuwa sehemu ya baraza lake la mawaziri?

NI IPI HATIMA YA HAO?!
 

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
564
1,000
Kwani Sisi wote ambao hatuko kwenye system/mfumo wa kiutawala kuna jambo tumemkosea mteuaji? Nape na January nadhani wako katika hatua nzuri tuu katika fani Yao... mawaziri hawafiki 25 na wabunge wako zaidi ya 350...Teuzi pekee wanazoweza pata Kwa SASA ni uwaziri au ubalozi...watu kuwasaidia au wao wenyewe kulalamika ni kukosa shukrani na kuwa na uroho wa madaraka..hii nchi ni yetu sote..nafasi walizonazo ni priveledge kubwa Sana..na bahati nzuri wamewahi kupata nafasi za juu zaidi hapo awali na sina uhakika kama walizipata Kwa merits.
 

Gallius

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,054
2,000
Hawa wameshazikwa kisiasa huwenda wakang'ara tena baada ya Mh. JPM kutoka madarakani maana wamekuwa kimya mno.
 

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
6,649
2,000
Watakuja kuibuka tu at the right time. Ndivyo siasa zilivyo

Huoni watu kama Kabudi na Bashiru Ally Kakurwa wameibuliwa tu ghafla kutokea “jalalani”?
Kwa hiyo Chuo kikuu cha DSM ndio imekuwa jalalani?
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,671
2,000
Sijui unauliza nini na nani? Kweli unavyowaona wana ufahamu wa kuendelea kuongoza chochote au lolote katika serikali? Hao walijikuza na kuamini wana uwezo, ukweli ni mbumbumbu wa ufahamu. Bado kuna wengine wamo ndani ya baraza kwa bahati tu na kazi yao kubwa huwa ni kusoma mitandaoni na kuja kuyasema wakiamini ndo ufahamu. Niambie kati ya hao wawili nani aliwahi kufanya la maana kwa nafasi yake.

Nchi lazima isafishwe.
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,671
2,000
walizaliwa kuwa kwenye siasa? wote wamekuwa kwenye siasa kwa migongo ya baba zao, sasa sioni shida, sema kwa vile hawana kazi yoyote ya taaluma yao.
NI watu ambao hawana taaluma yoyote ya kujivunia. sasa kama wanasubilia siasa iwaokoe, ni tatizo lao. Mtu unakwenda kusoma conflict resolution, halafu unaishia kuteta wabaya wako kwenye simu. Rubbish!
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,521
2,000
Watakuja kuibuka tu at the right time. Ndivyo siasa zilivyo

Huoni watu kama Kabudi na Bashiru Ally Kakurwa wameibuliwa tu ghafla kutokea “jalalani”?
Yaa ni kweli kama nape anafaa sana kurudishwa kile kitengo polepole alafu polepole apewe u katibu wa chama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom