Ni nini hatima ya zanzibar huru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini hatima ya zanzibar huru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zumbemkuu, Jul 10, 2011.

 1. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  wadau wenzangu hapa JF! nimekuwa najiuliza hi swali sana, kuwa ni nini kitatokea baada ya Zanzibar kuwa huru? nimejiuliza sana hilo swali kwakuwa znz inaunganiswa na visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba vyenye histori zinazotofautiana sana kisiasa, ukijumlisha na umbali unaotenganisha visiwa hivyo ndo utagundua kuwa NI HERI MUUNGANO HUU UNAOVUNJIKA KWA KUWA ULIANZA NA TOBO NA HATIMAYE VIRAKA NA MWISHO KUVUNJIKA KABISA KULIKO MPASUKO UTAKAOJITOKEZA WA NCHI HURU MBILI ZA UNGUJA NA PEMBA, HAPO NDO UTABIRI WA NYERERE UTAKAPOONEKANA WA MZANZIBARI NA MZANZIBARA.. hayo ni mawazo yangu tu wajameni, msinitoe roho nkashindwa kwenda taifa leo kushuhudia mnyama akirarua mtu.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  swala la muungano huu wetu linatutafuna sana......

  nimesoma pdf hii toka CIA nimejua kuwa muungano ni batili kabisa.kweli nyerere alimzidi karume ujanja...soma kuanzia page ya 118 hapo ndo utajua kuwa muungano ni batili

  http://www.foia.cia.gov/CPE/ESAU/esau-28.pdf
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  ndo nimemalizia kui'download, ngoja nikaisome, ila siwezi kuiamini sana CIA coz na wao ndo walokuwa wanapinga kwa nguvu zote ujamaa. so hawawezi wakamuandika nyerere kwa mazuri hata kidogo.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  we kasome ukimaliza niambie ili nikupe nyingine inayomuhusu kikwete...
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu kweli wewe umechanganyikiwa na bila shaka unahiji kwenda Samunge kwa Babu kupa kikombe labda unaweza pona.

  Mimi nilifikiri ungesema ni nini hatima ya tanganyika huru. Kwani ndani ya hili mmepotea Uraia wenu, Serikali yenu, Bendera yenu, Bunge lenu na hata jina lenu.

  Hili ni suala kubwa sana waDanganyika inawapasa kulifikiria na kulifanyia kazi.

  Zanzibar vyote wanavyo. sasa ni hatima gani unayoitaka.

  Mimi ninavyoona ukivunjika Muungano basi yaiotokea Sudan kuvunjika na kuunda Sudan ya kaskazini na kusini basi na Tanganyika yatatokea. sababu zitakuwa zile zile sawa na za Sudan ni udini na ukabila
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280  mkuu sitetei muungano huu japo nina amini katika UMOJA, ndo maana nchi zilizoendelea zinazidi kujiimarisha wkt sisi waafrika tunazidi kujitenga, kwa kifupi tunazidi kuwapa nafasi ya kututawala zaidi kwenye ulimwengu wa kisasa wa soko huria.siutetei muungano huu kwa sababu una manung'uniko mengi, ila hapo nilipo bold kwa kijani km ndo unachomaanisha, kweli fikra zako zipo kidini zaidi, ila its too late..maadam ushaakaa na kafiri kwa mitizamo yenu, basi umeshakula kitimoto...pole sana.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ndugu hujui kabisa siasa za kimataifa labda unajua siasa za kitongoji chako.

  Kifupi sababu kuu za kuvunjika suda ni UDINI na UKABILA. lakini lene impact kubwa kwa sasa ni UDINI. Sudan ya kaskazini ni Waislam na lugha yao ni kiarabu kama chetu na ni miongoni mwa nchi za Kiislam, lakini huku Kusini wao ni WAKRISTO ndio wakaleta chokochoko na hatimaye wamejitenga.

  Kwa wachambuzi wa siasa wanaona wazi sasa ukabila utachukua nafasi yake kwani kuna makabila matano makubwa lakini ni moja tu lililokuwa na wasomi wengi. hata ukisoma habari zilizoandikwa leo kwenye magazeti mbalimbali mgogoro tayari wanataka uwakilishi sawa katika barza lao la mawaziri, bunge na sehemu mbalimbali zak kazi. Je itawezekana.

  Tusubiri tutaona. Na hilo kama Tanganyika ikivunja muungano nanyi lazima liwatokeeeee lazima nchi igawike. Dalili zote zimeshaonekana. zanzibar tu anawabeba. wanaolijua hilo ndio wanalazimisha huo muungano.

  Sasa nawashauri Tanganyika mjiulize hatma yenu ikoje mkivunja muungano?
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Niliwasikia wabunge wote from Z'BAR ktk mjadala mmoja CCM alisema muungano upo safi hauna shida na mwingine wa CUF alisema muungano haufai, una kasoro nyingi akasema tatizo ni CCM hawasikii malalamiko ya Z'bar akasikitika na kusema hivi sasa ccm "WANAJITA NI CHAMA CHA MUNGU" Muungano huu unaswa kufumuliwa na kuundwa upya kama tutakavyofanya suala la katiba ila kama ukifa Z'bar watkuwa na hali mbaya zaidi ingawa wao hawajui ni mtizamo wangu tu !!
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Labda watu wa Bara msiwe wanafiki. Serikali enu ya Tanganyika ipo wapi? nchi yenu ipo wapi? Je Iliyopata uhuru mwaka 1961, Dce 9 ni nchi gani? Je tanzania ilipata uhuru lini.

  Naomba mtafakari hayo kabla kujibu
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Niliwasikia wabunge wote from Z'BAR ktk mjadala wa BUNGE mmoja CCM ' 'alisema muungano upo safi hauna shida" na mwingine wa CUF alisema "muungano haufai, una kasoro nyingi akasema tatizo ni CCM hawasikii malalamiko ya Z'bar akasikitika na kusema hivi sasa ccm", "WANAJITA NI CHAMA CHA MUNGU" Muungano huu unaswa kufumuliwa na kuundwa upya kama tutakavyofanya suala la katiba ila kama ukifa Z'bar watakuwa na hali mbaya zaidi hata kama wanajifariji na muafaka wao kumbuka malumbano yao hayajaanza baada ya CUF kuzaliwa, Pemba walilalamika mno kuwa wamemezwa na Unguja hivyo malalamiko hayo yataendelea na watapenda wajitenge maana utamu wa dhami ya kujitenga/kugawanyika itaendelea kuwatafuna hatimaye kuwameza kabisa. ingawa wao hawajui.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280


  Barubaru,

  ..wa-Tanganyika waliridhia kupoteza "alama za utaifa" kwasababu waliamini ktk umoja wa Waafrika wote.

  ..imani hiyohiyo ndiyo iliyopelekea wa-Tanganyika wakajitoa muhanga kwenye ukombozi wa nchi mbalimbali kusini mwa Afrika.

  ..sidhani kama masuala ya udini yatakuja kutugawa wa-Tanganyika. tayari kuna mchanganyiko na muingiliano mkubwa baina ya watu wa imani za Kikristo na Kiislamu na pia wa makabila mbalimbali. sasa hivi si rahisi kukuta familia ya ki-Tanganyika isiyo na mchanganyiko wa kidini au kikabila.

  ..matatizo ya Sudan yametokana na viongozi wanaotokea Kaskazini kunzisha mfumo wa Sharia Law bila kuzingatia reality kwamba Sudan ina mchanganyiko wa watu wa dini na makabila mbalimbali.

  ..kinachohitajika Tanganyika ni kiongozi anayehubiri umoja baina ya wananchi wote. miaka ya karibuni tumepatwa na balaa ya kuwa na viongozi wanaokimbilia kwenye udini ili kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

  ..pia muungano ukivunjika wa-Tanganyika watakuwa na muda mrefu zaidi wa kushughulikia misuguano ya kidini inayoanza kujitokeza. sasa hivi serikali ina kamati ya kushughulikia "kero" za muungano[read za wa-zanzibar], badala ya kushughulikia kero za uchochezi na chuki za kidini zinazoenezwa nchini.


  NB:

  ..kuna wanaodai Waislamu wanakosa madaraka serikalini na uwepo wa wa-Zanzibari ktk nafasi mbalimbali ndiyo unawafanya watulie. kwa hoja hiyohiyo muungano ukivunjika nafasi zilizoshikwa na wa-Zanzibari watapewa Waislamu wa Tanganyika.

  ..bilioni 50 zinazotolewa bure kama gharama ya umeme wa Zanzibar zingeweza kujenga hospitali, vyuo vya ufundi, etc ktk mikoa inayosuasua kimaendeleo huku Tanganyika.


   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280


  mkuu nina hakika hujui falsafa tuliyojengewa wa bara na mwl. nyerere, keep this in your mind, hata siku moja makabila ya tanganyika hayawezi kuja kupigana, mimi ni msambaa na tunaishi mbeya, tumejenga mbeya na dadazangu wameolewa na wanyamwezi wa tabora, kaka zangu wameoa wangoni wa songea, kwa hili Nyerere alifanikiwa, ondoa kabisa hiyo ndoto ya ukabila au udini kwa watanganyika, udini unaaoonekana sasa unasababishwa na huu muungano na nyinyi wazenji.
   
 13. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280

  mkuu umemmaliza huyo jamaa kabisa, na hapo kwenye bold ya green ni ukweli usiopingika kuwa chokochoko za udini zinaletwa na wanzanzibar hapa bara, wakishaondoka hutasikia hiyo kitu tena.
   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe umetulia sana, hii nimependa sana big up " haya hawaelewi kabisa"
   
 15. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwanza nakuomba usishughlike sana hatma ya Zanzibar baada ya kujikomboa kutoka na mkoloni wetu Tanganyika. Siku mkiondosha majeshi yenu ya uvamizi ndio utakuwa ndio mwanzo wa uhuru wetu wa pili.

  Huyu huyu Nyerere ambae mnataka kumfanya Saint, ndie huyu huyu ambae alileta fitna za kuwagawa Wazanzibari kwa misingi ya ukabila na umajimbo. Kwa khofu zao, viongozi wetu wa wakati huo, waliingia mtegoni na kutufikisha hapa tulipo.

  Mimi sishangai, Nyerere huyu huyu alietufitinisha, ndie huyu huyu aliegeuka mtabiri na kueleza kuwa tutaendelea kubaguana baina yetu.

  Nataka nikuhakikishie kuwa kama alivyosema ndugu yangu Takashi, "zama za Nyerere zimekwisha" na wala msikae mkafikiria kuwa hilo litatokea Zanzibar. Generation ya viongozi tulionao ni nyengine na vijana wa sasa hawatazami tena nyuma.

  Nakubali kuwa wako wahafidhina wachache ambao kwa uroho wao, hata wakipewa rushwa ya kusamehewa deni la umeme la 50/- bilion, wako tayari kutusaliti. Pia liko kundi la wapenda posho. Lakini wote hao siku zao zinahesabika.

  Wakati mwengine huhisi mnatusanif na kutukejeli, pale mnaposema vunjeni au tangazeni kujitoa huku mkijua fika kuwa majeshi yenu yametuzingira kila pahala na wakiamua kutupiga, hufanya hivyo bila sababu za msingi.

  Suala la msingi ni kuwa hakuna hicho mnachofikiria na mkiondoka tu, basi Zanzibar itabiga hatua kuliko mnavyodhani.

  We cant wait to see your backs, Zanzibar for Zanzibaris.
   
 16. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280

  poa mkuu, hata mimi binafsi nimechoka kuwa mkoloni dhidi ya muafrika mwenzangu, nahitaji kubaki na tanganyika yangu, hii thred niliianzisha kwa maana tu ya kujaribu kufikisha mawazo yangu maana nina amini katika undugu. na sisi watanganyika kwa kuonyesha tunawajali na tunawapenda kama ndugu zetu tutaendelea kuipigia serikali makelele ili hatimaye wasikie kilio chenu.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wewe umesoma hiyo Ddf ni kitu gani kimepelekea wewe kusema Muungano ni batili?.. labda sherehesha hapa Muungano halali ni upi na tupe mfano wa Taifa lililotokana na Muungano halali maana upooona uharamu lazima kuna Uhalali..

  Nakuomba tu isome hiyo pdf vizuri toka mwanzo pamoja na kwamba hata wao CIA kuna mengi hawakuyafahamu wamekisiakisia tu kutokana na usiri mkubwa wa mapinduzi pamoja na Muungano lakini la muhimu nenda kasome Muungano wa states zote za Marekani kisha nambie Uhalali wake unatokana na kitu gani? lakini wenzetu sifa zote watampa Abraham Lincorn aliyeua maelfu ya watu na alomost kuwamaliza kabisa wahindi wekundu ktk kuunda Muungano ambao leo wanajivunia hata kama umejaa wahamiaji!

  Hawa hawa CIA hawajui kwa undani ushirikiano baina ya TANU na ASP kabla hata ya mapinduzi na kitu gani walikuwa wamekubaliana. Pia wala hawajui ushirikiano uliokuwepo baina ya Umma Party na baadhi viongozi wa ASP kina Hanga.

  Watu wengi sana wanamlaumu Nyerere kwa kupinga kuunganisha Umoja wa nchi za Kiafrika kaa alivyokusudia Nkurumah, lakini nadhani huu muunganano wa Tanganyika na Zanzibar ni ushahidi tosha wa Nyerere kuonyesha kwamba jambo lile lisingewezekana kabisa! Tumeshindwa ktk kila Taifa liloungana kabla ya Uhuru, Ethiopia imegawanyika na Eritrea, Somalia, Tunaelekea kuona mgawanyiko Sudan, Tanzania na pengine Libya yote kwa fikra kwamba tukiwa pekee tutaweza kuendelea hali uchovu wa nchi za Kiafrika unatokana na uvivu wetu wenyewe ktk uzalendo wa kuwa Responsible!

  Responsibility ni gonjwa la mtu mweusi, pengine niseme ni utamaduni wa kigeni ambao hatujawahi kuwa nao. Waafrika hatupendi kuchukua maamuzi magumu, kuchukua dhamana ya matendo yetu wenyewe, kukiri kwa moyo na kukubali makosa yetu wenyewe ni lazima kuwepo na sababu nje ya uwezo wetu - lazima awepo mchawi au mtu aloyesababisha lakini sio sisi wenyewe hata iwe kwa maendeleo yetu wenyewe.
  Mpe ndugu yako mamlaka ya kusimamia mali zako atakuibia na pengine yeye mwenyewe kufilisika (kuibiwa) lakini hatakubali makosa ya kumpa mamlaka mtu usiyemwamini wala yule aloiba kukubali kuiba isipokuwa wote walirubuniwa, makosa sii yao bali ni ya fulani! - Hii ni hulka ya waafrika kutochukua majukumu wenyewe kwa kutopenda kusimamia wenyewe vitu vyao bali kumkabidhi mtu mwingine ingawa hawamwamini vile vile.

  Ndio haya ya uwekezaji kwa wageni tunajua fika kwamba watatuibia lakini ni bora kuwapa wao kuliko sisi wenyewe tukikimbia responsibility! Leo hii ukimuuliza JK kwa nini nchi maskini? oooh sijui, niliyakuta matatizo nimeyarithi toka kwa Mkapa, wengine mnasema Nyerere ndiye alituweka ktk umaskini, wengine mkoloni basi tu ili mradi hakuna mtu anayekubali kwamba he is responsible! Uzalendo unaanzia kwa kuwa responsible na sii kutazama Muungano wa Nyerere kama vile mtu unataka kuona cheti cha harusi ya baba yako na mama yako ili ujue kama wewe ni mtoto halali au laa!
  Ujinga mtupu.....
   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mkuu mkandara mie nimeisoma hiyo PDF na sijaona huo uharamu, na kwa kuelewa wangu wa haraka haraka ulikuwa unaonyesha juhudi za nyerere ktk harakati zake za kuiunganisha afrika, ila kwa kuwa walioandika hawakutaka huo muungano, wamejaribu kila njia uonekane ni muungano wa haramu ili wajenge chuki kwa watu wa znz lakini bado hakuna uharamu wowote.
   
 19. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tanganyika haitaweza kugawanyika hata siku moja, sababu zipo nyingi mno eg ..mchanganyiko wa makabila kiasi kwamba wanaoa na kuolewa na makabila tofauti bila shida ..kuishi sehemu tofauti tofauti hata kujenga huko pasi tatizo kinyume na wazanzibari amabao hawataki watangayika wajenge huko mf kuchoma vibanda vya biashara vya wabara Z'bar ...Elimu ya wabara ipo juu wengi wameelimika kiasi kwamba mambo ya ukabila udini ni minor case kwao ndiyo maana Rais alipo sema TZ kuna udini wengi walireact kuonyesha kwamba udini haupo ila unafanywa uwepo. ...Umoja , mshikamano , ushirikiano ni mkubwa sana Bara ndiyo maana misibani, harusini, sherehe zote waanashirikiana pasi kujali ni mkristo au mwislam tofauti na Z'bar ambao walifikia kipindi hawazikani eti tofauti za itikadi wenzao kwenye matatizo tofauti zinawekwa pembeni '''' sijui nieleze lipi hadi muelewe ila MUUNGANO UKIFA Z'BAR NDIYO WATAADHILIKA kisiasa, kiumoja maana hatawapenda watu wadini ya kikristo baada ya kujiunga na OIC '''' MENGINE AMEELEZA KWA KINA JOKAKUU sasa muelewe msipende kuto elewa kihivyo au mna rembesha mjadala na ukweli mnaujua acheni basi tujadi mengine
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mama alikuwa muislam, ndugu zangu wote wa upande wa mama ni waislam, na hata jina langu la kwanza ni la kiislam hadi kupelekea watu kuhisi mimi nili'kigwangala jina la shule coz jina langu haliendani na dini yangu, mimi ni msambaa na tunaishi mbeya na kujenga mbeya, dada yangu kaolewa na mnyamwezi, kaka yangu kaoa mngoni, ukabila na udni kwenye familia yetu kwishney!
   
Loading...